Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

expand...
Mzee mmoja wa kichaga alikuwa anampa wasaa mwanae wa kiume kwenye harusi yake. Akamwambia "Mwanangu mimi sitaki kupindisha maneno. Nakuambia ukweli. Ukubali ukatae shauri yako. Akamwambia kwenye ndoa yako ukiona vituko vimezidi cheki mfukoni mwako au katika account yako ya benki.Ukiona mfuko uko vizuri na benki uko vizuri na bado vituko haviishi ujue wewe ndio tatizo.

Lakini ukiona mfukoni hauna kitu na benki hauna kitu na vituko haviishi tafuta hela. Ukishindwa muache mtoto wa watu aende. Kama ni wako atarudi. Kama sio wako sio wako tu hata ukeshe unaomba. Sikubaliani na "conclusion" ya huyu mzee wa kichaga lakini siwezi kumpinga kwa sababu ni mzee na ameona mengi.
 
Mimi nadhani mambo ya 50 50 ndo yanaleta shida sana, hvyo mwanaume unapo oa hakikisha uanakua mwanaume kweli kwani sie wanawake hua tunatabia ya kupima upepo tukitest tukiona tunaweza kuwaendesha basi tunafanya hvyo.

Ni wajibu kwa mwanaume asimamie abc zake anazotaka na kutimiza wajibu wake kwenye ndoa na mke ajua kabisa mume wangu ananipenda na anataka hivi na vile na nikicross huu mstari mume ndo itakua limit yake. Kwa kufanya hvi ninaamini mke hatosumbua na heshima itakuepo nawe mume pia utamuheshimu mke
 
Ukiona anavuruga amani yako kwa vitu visivyokua na maana kila siku kesi na drama zisizoishi piga chini bro. Hayo mambo ya kusema wanangu wataishi vipi achana nayo yatakufanya uwe mtumwa wake.
 
Unampa dudu la kutosha? Au ndio unamchafua chafua tu mtoto wa watu na hayo maji yako mazito?
 
Kila jambo lina chanzo chake wewe Kama mwanaume jaribu kuchunguza source ya vituko vyote hivyo ni nini ukishaelewa ndo utajua namna ya kudeal nayo. Unapotibu maradhi kwenye ndoa tibu Kama vile wafanyavyo madaktar wa hospital kwamba kila jambo deal nalo kwa hatua na kupima athar zake.
 
Tafuta chanzo kinachopelekea kuwa na tabia za kisumbufu...

Kama ni tabia, cheo kazini, marafiki, nduguze, menopause au wewe mwenyewe mwanaume umebadilika...
 
Kwa moyo wa dhati, naomba tulijadili hili kiutu uzima, huende tukaokoa maisha ya mtu mmoja.

Mimi nimeshindwa pakuanzia kwasababu umeficha mengi kwenye hili bandiko.

Ungefunguka vizuri tuelewe vurugu za aina gani na chanzo ni nini, ningetoa maoni kwa ufahamu walau kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom