ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,748
- 42,218
- Thread starter
- #101
Asante 🙏Ndio
Asante 🙏Ndio
Na usiombe ukakutana na mtu ambaye Elimu haijamkomboa halafu kuchanganya na roho mbaya na ubinafsi ndo ntajuta kumfahamu😜Kuna jambo huwa linanichanganya sana🤔
Je, elimu imekuongezea akili au imekuondolea upumbavu?
Kwa sababu nimeona watu wenye elimu za juu sana, vyeti vingi na majina marefu, lakini baadhi ya maamuzi yao yanakufanya ujiulize kama kweli elimu peke yake inatosha kumfanya mtu awe na akili
Unakuta mtu ni kiongozi ameshika nyadhifa mbali mbali ila ukitazama maamuzi yake unabaki na alama ya mshangao heh huyu si ni msomi?
Unajiuliza huyu elimu haikua na msaada kwake ?
Mbona anaamua,anaongea kama mjinga?
Wakati huo huo unakutana na mtu ambaye hakusoma sana au hakupata nafasi ya kusoma kabisa, lakini ana uwezo mkubwa wa kufikiri, kutatua matatizo na kuona mambo kwa upeo mpana kuliko hata baadhi ya wasomi
Hapo ndipo nikajiuliza, ni nini hasa kinachomfanya mtu aitwe genius na ni nini kinachomfanya aonekane mpumbavu?
Je, ni kiwango cha elimu?
Je, ni uwezo wa kufikiri?
Je, ni maamuzi anayofanya kila siku?
Au ni namna anavyojifunza kutokana na makosa yake?
Kwa mtazamo wangu, elimu inaweza kuongeza maarifa, lakini si lazima iondoe upumbavu
Maana kuna wasomi wapumbavu(hapa nisamehewe)
Na kutosoma sana si lazima kumfanye mtu akose akili
Wewe unaonaje?
Tofauti ya mtu mwenye akili nyingi na mpumbavu unaiona wapi?
Na elimu imekusaidia nini hasa kwenye hilo?
Chombezo( ni kua hata wapumbavu huzeeka)
ShesRise_1 🤚
It's Furahi deiiiiii💃
Umeongea vizuri sana kipenzi shukranKuna knowledge (maarifa) na kuna wisdom (hekima / ufahamu).
Maarifa ni taarifa.
Hekima / ufahamu ni mahusiano kati ya taarifa. Taarifa pro max.
Unaweza ukawa unajua A-Z (umesoma mavitabu mengi una mavyeti mengi)
lakini ni huna ufahamu, hujui M na A inaweza kuwa MA, hujui MA na MA inakuwa MAMA,
una taarifa nyingi lakini huoni uhusiano wa hizo taarifa, in which case huna taarifa kwa kiwango hicho ulichofikiri unacho,
Na kwa kutegemea kiwango cha taarifa ambacho tayari unacho, ukosefu wako wa ufahamu unakufanya kuwa mjinga, mjinga mjinga, au mpumbavu.
Ndomana hata Biblia inasema:
"Mtu yeyote anayedhani kwamba anajua kitu, bado hajui kama impasavyo kujua."
1Wakorintho.8.2.NENO2025
Mjinga ana taarifa kidogo. Ana matumaini ya kuwa na Hekima. mf. Mtoto au mtu mzima ambaye hakuwahi kupata hizo taarifa.
Mjinga mjinga ana taarifa za kumtosha lakini kaamua makusudi kuchagua ujinga kwasababu yeye mwenyewe hajawahi kupata madhara ya kumshtua
mf. Kijana wa hovyo, machawa wa viongozi waovu.
Mpumbavu hopeless case, ana taarifa nyingi sana lakini aidha ufahamu wake umefungwa makusudi na MUNGU au amechagua kwa hiari kuwa na B na A MA sio BA na ndo kashaamua
mf. Wakana Mungu, viongozi makatili / waovu, wahalifu waliokubuhu / watenda dhambi wasiotubu.
Hekima hutoka kwa Mungu ndomaana tumembiwa tumuombe. Unaweza ukajifunza herufi zote duniani A-Z kwa lugha zote na ushindwe kujua M na A ni MA kwasababu MUNGU kafunga ufahamu wako. Wewe hutojiona, atakuona anayejua kuwa M na A inakuwa MA.
Na Mungu alivyo sasa sijui tuseme ana sense of humor, au ndo katika kudhihirisha kuwa kuna tofauti ya Maarifa na Hekima ambayo hutoka kwa Mungu mwenyewe, kwa makusudi anachagua vinavyoonekana havistahili ili kuvishusha vinavyoona vinasatahili.
Ndiposa utakuta mtu ana mahela mengi lakini mjinga mjinga akili anaibia kwa maskini.
Au mtu ana PhD lakini mjinga mjinga akili anaibia kwa college drop out.
Au mtu mzee lakini mjinga mjinga, akili anapata kwa mjukuu wake.
Au mzuri sana lakini mjinga mjinga akili anakuja kuibia kwa ngolo kante.
"...Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika vyeo.
Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.
Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko,
ili mtu yeyote asijisifu mbele zake."
1Wakorintho.1.26-29.NENO2025
Yamewahi kukuta dear ?Na usiombe ukakutana na mtu ambaye Elimu haijamkomboa halafu kuchanganya na roho mbaya na ubinafsi ndo ntajuta kumfahamu😜
Asante sana mkuu karibu tena♥️Tofauti kubwa kati ya msomi na asiye msomi haipo tu kwenye vyeti, bali katika uwezo wa utatuzi wa changamoto, mtazamo wa kimaisha, na namna wanavyotumia maarifa wanayoyapata katika jamii.Hapa kuna mambo yanayowatofautisha kwa muhtasari:Uwezo wa Kufikiri (Upeo): Msomi mara nyingi huchanganua mambo kwa kina kabla ya kuchukua hatua na ana uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto. Asiye msomi huwa anategemea zaidi uzoefu wa kawaida wa maisha na mazoea.Kujitegemea na Fikra: Msomi ana uwezo wa kujenga hoja, kufanya maamuzi sahihi, na kufikiri kwa uhuru.Utatuzi wa Matatizo: Wasomi hutumia mbinu za kisayansi na utafiti kutatua migogoro, wakati wasio wasomi mara nyingi hutatua changamoto kwa kutumia busara za kitamaduni au maelekezo ya kawaida.
Ndio mara nyingi tu.Yamewahi kukuta dear ?
Kuna comment yako moja kila nikikuona naikumbuka nachekaa😅
Usihukumu, shida yako ubongo wako kuna namna ushanichukulia, ulifeli sanaLeo napata comment za madini tupu siku yangu imebarikiwa
Uzi wangu umebarikiwa
Hadi wewe makaveli10 umeongea point tupu 🙌😅
Acha basi 😅😅Ndio mara nyingi tu.
Ofisini kwetu Kuna mbaba mtu mzima na ni kiongozi,akikaa kimya hivi akiwa busy na computer utasema ni mtu wa heshima zake kwa wasiomfahamu.
Sasa muombe ushauri ndo utajua hili bonzo 😅na linapenda sana kuchongea wenzie kwa kuwa liko karibu na Boss Ili wafukuzwe KAZI.
Sasa mtu asipende makalio 😅Na kuna kiongozi mkubwa mmoja nina namba zake oyaaa 😅anaposti wadada wenye makalio makubwa mara nyingi sana na kuandika caption za ajabu sijawai ona. Ama anaposti vitu ambavyo kwa asilimia kubwa havina maadili.
Hata mimi kuna watu hua na waheshimu sana akipewa nafasi aongee heh unachokaNa anachaguliwa Kila kwenye uchaguzi sielewi jamani. Wako wengi na umeongea ukweli.
Mzee wa kuchezesha 😆Usihukumu, shida yako ubongo wako kuna namna ushanichukulia, ulifeli sana
👊"YULE LAST KING WA SCOTLAND SIO IDD AMIN WA UGANDA"
Ichukue hiyo.
Very strong mkuu!💪Kuna knowledge (maarifa) na kuna wisdom (hekima / ufahamu).
Maarifa ni taarifa.
Hekima / ufahamu ni mahusiano kati ya taarifa. Taarifa pro max.
Unaweza ukawa unajua A-Z (umesoma mavitabu mengi una mavyeti mengi)
lakini ni huna ufahamu, hujui M na A inaweza kuwa MA, hujui MA na MA inakuwa MAMA,
una taarifa nyingi lakini huoni uhusiano wa hizo taarifa, in which case huna taarifa kwa kiwango hicho ulichofikiri unacho,
Na kwa kutegemea kiwango cha taarifa ambacho tayari unacho, ukosefu wako wa ufahamu unakufanya kuwa mjinga, mjinga mjinga, au mpumbavu.
Ndomana hata Biblia inasema:
"Mtu yeyote anayedhani kwamba anajua kitu, bado hajui kama impasavyo kujua."
1Wakorintho.8.2.NENO2025
Mjinga ana taarifa kidogo. Ana matumaini ya kuwa na Hekima. mf. Mtoto au mtu mzima ambaye hakuwahi kupata hizo taarifa.
Mjinga mjinga ana taarifa za kumtosha lakini kaamua makusudi kuchagua ujinga kwasababu yeye mwenyewe hajawahi kupata madhara ya kumshtua
mf. Kijana wa hovyo, machawa wa viongozi waovu.
Mpumbavu hopeless case, ana taarifa nyingi sana lakini aidha ufahamu wake umefungwa makusudi na MUNGU au amechagua kwa hiari kuwa na B na A ni MA sio BA na ndo kashaamua
mf. Wakana Mungu, viongozi makatili / waovu, wahalifu waliokubuhu / watenda dhambi wasiotubu.
Hekima hutoka kwa Mungu ndomaana tumembiwa tumuombe. Unaweza ukajifunza herufi zote duniani A-Z kwa lugha zote na ushindwe kujua M na A ni MA kwasababu MUNGU kafunga ufahamu wako. Wewe hutojiona, atakuona anayejua kuwa M na A inakuwa MA.
Na Mungu alivyo sasa sijui tuseme ana sense of humor, au ndo katika kudhihirisha kuwa kuna tofauti ya Maarifa na Hekima ambayo hutoka kwa Mungu mwenyewe, kwa makusudi anachagua vinavyoonekana havistahili ili kuvishusha vinavyoona vinasatahili.
Ndiposa utakuta mtu ana mahela mengi lakini mjinga mjinga akili anaibia kwa maskini.
Au mtu ana PhD lakini mjinga mjinga akili anaibia kwa college drop out.
Au mtu mzee lakini mjinga mjinga, akili anapata kwa mjukuu wake.
Au mzuri sana lakini mjinga mjinga akili anakuja kuibia kwa ngolo kante.
"...Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika vyeo.
Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.
Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko,
ili mtu yeyote asijisifu mbele zake."
1Wakorintho.1.26-29.NENO2025
Sasa ndugu yangu cousin realMamy kupenda makalio makubwa ni shida?Na kuna kiongozi mkubwa mmoja nina namba zake oyaaa 😅anaposti wadada wenye makalio makubwa mara nyingi sana na kuandika caption za ajabu sijawai ona. Ama anaposti vitu ambavyo kwa asilimia kubwa havina maadili.
Umefeli pakubwa 🤣😂, pole pia 🤣😂Mzee wa kuchezesha 😆
Nilichukua zile akili za selfika
👊
Sijafeli mjomba tuliaaa🤫Umefeli pakubwa 🤣😂, pole pia 🤣😂
Igweee😅 sawa sawaMsibani ukileta akili za harusini watu watakushangaa, kila mahala pana mazungumzo yake.
Sijasema kwamba elimu ni mbaya isipokuwa elimu ipo limited yaani wameweka kiwango Cha juu kuhitimu ni PHD kwamba huyu ndo mwenye akili nyingi na kama ndo ivyo kwanini hakijawekwa kigezo kwamba ili uwe rais wa nchi lazima uwe na PHD? Na vip kuhusu wale ambao hawana elimu kabisa Lakini Wana mafanikio makubwa?Asante sana
Elimu inaweza kukusaidia kufikia mafanikio yako kwa urahisi zaidi
Mf: ukasomea udaktari elimu hiyo itakupa ajira na mwisho kipato kwa urahisi zaidi na mwisho kufikia mafanikio yako unayotaka
Maxnce mello huenda elimu yake ilichangia pakubwa kuweza kufungua kufungua hii platform
We unadhani angefunguaje platform kama hii bila kujifunza namna ya kuiendesha
Hili swali uliloniuliza ndio maada yangu inafanania huko mkuuSijasema kwamba elimu ni mbaya isipokuwa elimu ipo limited yaani wameweka kiwango Cha juu kuhitimu ni PHD kwamba huyu ndo mwenye akili nyingi na kama ndo ivyo kwanini hakijawekwa kigezo kwamba ili uwe rais wa nchi lazima uwe na PHD? Na vip kuhusu wale ambao hawana elimu kabisa Lakini Wana mafanikio makubwa?
Umefeli pakubwa, niamini mimi.. ila sio suala..Sijafeli mjomba tuliaaa🤫
Igweee😅 sawa sawa
Nimekubari mkuu😁Umefeli pakubwa, niamini mimi.. ila sio suala..
Acha basi mtumishi😅😅Usiamini haya ya mtandaoni.
Maisha hayahitaji userious kiasi hiko..
Wengine kwenye VIKAO VYA KUSULUHISHA NDOA, na mambo tofauti tofauti, tunaaminiwa kutoa maamuzi ya mwisho.
Tuendelee kifurahia JF.