Ufahamu vs Akili: Tofauti Halisi

Ufahamu vs Akili: Tofauti Halisi

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
702
Reaction score
1,646
INTELLIGENCE vs KNOWLEDGE! (UFAHAMU DHIDI YA AKILI

Ufahamu (au intelligence) ni kitu ambacho mtu au mnyama au kiumbe hai yeyote anazaliwa nacho, hafundishwi na yeyote.
Intelligence ni tofauti na akili.

Akili ni yale maarifa aliyo nayo mtu kwa kufundishwa.
Akili ni zao la jamii iliyokuzunguka.

Huwezi kuwa na akili zaidi ya jamii iliyokuzunguka, lakini unaweza kuwa na Intelligence kuliko jamii iliyokuzunguka kwa sababu Intelligence unazaliwa nayo, ni kipawa chako, lakini akili unaingiziwa.
Kama ukiondoa kichwani mwako mambo yote ulofundishwa na wazazi, waalimu, jamii yako nk., kile utakachobakia nacho ni intelligence, yaani ufahamu wako ambao ndio wewe mwenyewe halisi.
Intelligence ni kitu ambacho kinamsaidia mtu kuishi katika mazingira yake.
Hata mti una intelligence, ukiona maji yamepungua, unapukutisha majani. Bila kufanya hivyo, hautaweza kuishi, utakufa!

Wanyama hawana akili, lakini wana Intelligence.
Kile kitendo cha mnyama dume kunusa mkojo wa jike na kutambua kwamba jike lipo tayari kupandwa, hiyo ni intelligence, sio akili.
Ndio maana Intelligence ni bora kuliko Akili.
Kwa hiyo, Intelligence unazaliwa nayo, haufundishwi na mtu; kinachofundishwa ni elimu ambayo huwa tunaiita knowledge.
Hiyo knowledge ndio akili yenyewe.

Mfano, umeme ukizima ghafla nyumbani wakati mnaangalia mpira pale sebuleni, lazima mtaulizana pale kama kuna mtu yeyote kati yenu mwenye AKILI ya kurekebisha hali hiyo.

Akitokea mtu 'akakorokochoa' vitu pale na umeme ukawaka, tunasema ana akili kwa sababu ya ile KNOWLEDGE fulani aliyowahi kuipata mahali kuhusiana na suala zima la Elimu ya umeme, iwe formal au informal.
Hii knowledge ni elimu na ndiyo hufundishwa.

Kwa hiyo usichanganye kati ya intelligence na knowledge/ akili (maarifa)
Knowledge huzaliwi nayo, bali unafundishwa, lakini intelligence unazaliwa nayo.
Kwa kadiri unavyoongeza knowledge, ndivyo unavyopoteza au kudumaza intelligence yako.
Wasomi karibu wote wanatumia knowledge (elimu) ili kufanikiwa, wakati wale ambao hawajaenda shule kabisa wanatumia intelligence ili kufanikiwa.

Wengi wa wasioenda shule wana nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko wale walioenda shule kwa sababu Intelligence ni bora kuliko Knowledge.

Ukiondoa ajira asilimia kubwa ya wasomi watakufa kwa presha, lakini wasiosoma wataendelea kupeta kama kawaida kwa sababu wao maisha yao hayategemei knowledge, yanategemea Intelligence!
Hata hivyo, wasomi (wenye elimu) na wasiosoma (wasio na elimu), tatizo lao wote ni moja.

Msomi knowledge yake imeharibiwa na EGO na huyu ambaye hajasoma intelligence yake naye imeharibiwa na EGO pia.

Kumbuka kwamba EGO ni mafundisho ya jamii inayomzunguka msomi na ambaye hajasoma.
Wote hawapo salama dhidi ya EGO.
Wote wameharibiwa na EGO.
Ingawa wale ambao hawajasoma EGO yao ni ndogo, wasomi EGO yao ni kubwa zaidi.
 
Wanyama wana ufahamu kweli, ila kuna kitu kinaitwa "instinct" nitatafuta maana yake kwa kiswahili. Nafikiri ufahamu ukizidi unaitwa genius. Hivi mtoto anapizaliwa nani anamfundisha kuwa nyonyo ni chakula? Kwa nini analia? Kila binadamu anazaliwa na "innate ideas "
 
Hapo kwa mtoto umegusa penyewe👇
Kila mtu amewahi kuwa mtoto mchanga na tunaamini mtoto mchanga ni dhaifu anategemea kila kitu kutoka kwa wakubwa wanaomzunguka
Mtoto anapozaliwa anakuwa na uwezo maradufu na anajua katika Ile maana halisi ya kuwa mtu. Mtoto anapozaliwa anakuwa na nguvu chanya full kwasababu hana matukio wala hana hofu wala hana chuki kama walizonanazo wakubwa ambao ndo hugeuka kuwa walimu wake unafundishwa na uliemzidi uwezo tegemea uwezo wako kushuka mtoto mchanga ana maono yanayotokana na uhalisia aliobeba kama mtu kamili ndio maana mtoto ndogo tena Yule ambae hajaanza hata kufungua macho akaona anaweza kumjua mtu mbaya. Inaweza kushangaza Mtoto ndogo aliyezaliwa Leo hulia sana kila anaposhikwa na wachawi au wanga. Usiku wewe unayejiona bora kupitia ukubwa ulionao huoni ubaya wala uhisi chochote yaani umepoteza hadi uwezo wa kuhisi Lakini mtoto mchanga hubaini na kuona kile ambacho wewe hukioni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom