Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

Mkuu gfsonwin,kwa kifupi Halmashauri ni ile Serikali inayoongoza sehemu husika. Manispaa ni moja ya vyeo vya sehemu za kiutawala katika nchi.Vipo kama hivi:
1.Kijiji
2.Mji Mdogo
3. Mji
4.Manispaa
5.Jiji
Mtu aweza kutafsiri 'Halmashauri' kama 'Serikali ya...' Mfano, 'Halmashauri ya Mji Mdogo Kibaha' ikimaanisha 'Serikali ya Mji Mdogo Kibaha'. Hivyobasi, Halmashauri huwepo kwenye vyeo vyote ya kiutawala vya sehemu za kiserikali. Sasa waweza kuwa na sentensi kama Halmashauri ya Kijiji cha....na kadhalika
 
Last edited by a moderator:
Na Mji ambao haujafikia ukubwa wa kiwango cha manisapaa unaitwaje?

Kabla ya kua Manispaa huo mji utakua ni Halmashauri ya Mji na ukitoka Manispaa huo mji utakua Jiji. Mfano; Jiji la Arusha hapo nyuma ulikua ni mji wa Arusha yaani Halmashauri ya mji wa Arusha, ikaja ikawa Manispaa na sasa ni Jiji, hapo ni kuweka Halmashauri ya........Mji, Manispaa, Jiji. Hata Vijiji vitakuja kua Majiji lakini zote hizo ni halmashauri.
 
somo zuri mno japo wengine wanzuga kujua na ukweli hawafahamu chochote na hsa waliompinga mtoa mada
 
Hakuna tofauti kati ya Halmashauri na Manispaa, isipokuwa umekata maneno kwa sababu jina sahihi ni Halmashauri ya Manispaa ya ...... ie Mkoa wa Kigoma kuna Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji (Kigoma/Ujiji Municipal Council-KUMC), Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (Kigoma District Council - KDC), kuna Kibondo DC,Kasulu DC nk.
Sasa Tofauti ya Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Manispaa nafikiri ndio kusudio la msingi la swali lako, ipo hivi manispaa inapewa baada ya kuwa na vyanzo vya kujiendesha yenyewe angalau kwa asilimia fulani zaidi 30% (sina uhakika sana), pili idadi ya watu kwa eneo yaani population per unit area, watu wamesongamana kiasi gani, concetration per urea.
Kwa sababu idadi ya watu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ni kubwa ukilinganisha na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji lakini msongamano wa watu katika eneo dogo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni kubwa kuliko la Halmashauri ya wilaya ya Kigoma. Naomba nifafanue hapo kwenye msongamano ie unaweza kuta KDC watu 100 wanakaa kwenye wastani wa mita za eneo 1000 lakini lakini KUMC watu 100 wanakaa kwenye eneo la 500, na ndio maana utaona Halmashauri za manispaa nyingi zipo mjini, kwa mfano Dar es Salaam kuna Halmashauri za manispaa tu na hakuna Halmaahauri za wilaya yaani Kinondoni, Ilala and Temeke municipal Council.
Vile vile kuna wilaya hapo tusichanganye vyote viwili yaani Halmashauri ya Manispaa na wilaya zinaweza kuwa katika wilaya moja ie Kigoma/Ujiji Municipal Council and Kigoma District Council zote zipo KIGOMA DISTRICT.

Nimekupata vizuri mkuu big up
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Kwanza napenda kutofautiana na mtazamo wako.
Kwa mtazamo huu basi kila anayepost kitu humu ndani ya JF ni mvamizi.... Maana huyu pamoja na mimi hatukulijua hili, na wewe pamoja na wengine hamyajui mengine na mmeshawahi kuomba kufahamishwa hapa JF. Hivyo basi kama hoja yako kila anayeuliza kitu hapa JF ni mvamizi, basi naungana na wewe maana wote wavamizi... Otherwise tutakutafutia post zako ulizowahi kutaka kujuzwa kitu ili tujuwe nawe ulishawahi kuwa mvamizi kwenye eneo lipi. Kufahamu kwako maana ya halmashauri (kama kweli unafahamu, maana wengine huwa ni mbwembwe tu) kusikupe superiority complex ya kukupelekea kusema muuliza swali kavamia wakati ametusaidia wengi tu kwa swali lake.
 
somo zuri mno japo wengine wanzuga kujua na ukweli hawafahamu chochote na hsa waliompinga mtoa mada
Ni kweli mkuu, maana hapa duniani kuna watu wanajifanya wanajuwa kumbe hamna kitu, na mbaya zaidi hawajui kama hawajui na wanavyozisi kuelezea maana ya hicho wanachodhani kuwa wanajuwa ndivyo wanavyozidi kutuonyesha jinsi gani hawajui. Ila wa aina hii ni wa kuwapa ukweli tu hata kama utawaume.... JF kiboko yao na ni shule kwa wote kwa namna inayoumiza, inayofurahisha au mchanganyiko.
 
Hatimaye nimeelewa sasa...

Mapendo.
 
Tatizo serikali haijaweka vizuri mitaala ya somo la uraia au civic education. Watanzania wote tunaishi na kupata huduma kupitia halmashauri za vijiji, wilaya, miji, manispaa na majiji. Leo hii mlipa kodi kwenye halmashauri hizo akiuliza Halmashauri ni nini, inatokana na upungufu wa mtaala wa somo la uraia. Wengi wetu nilivyoona kwe mada hii ni kwamba hawajui hata tofauti ya serikali kuu na halmashauri. Ni kama hawajawahi hata kujua kuna wenyeviti wa kijiji au mtaa, kuna madiwani, na kuna wabunge. Haya yote yanatakiwa kusomwa kabla ya kuhitimu darasa la saba. KOSA NI SERIKALI YA CCM. TUAMKE, TUCHUKUE NCHI YETU ILI TUTOE ELIMU BORA HATA KWA SISI WANA JF.
 
Naomba nikuunge mkono, kwa kuongezea zaidi hivi ili hawa vijana waweze kuelewa.

Halmashauri ya Kijiji
Halmashauri ya Mji
Halmashauri ya Wilaya
Halmashauri ya Manispaa
Halmashauri ya Jiji.
Na mimi naongezea ifuatayo ingawa sio rasmi lakini ni halmashauri kamili:
Halmashauri ya kichwa chako, hapa kila mtu ana halmashauri yake mwenyewe.
Kama walivyosema wadau wengi, Halmashauri ni mamlaka inakuwa na kiongozi pamoja na wajumbe, kiongozi aweza kuitwa meya au m/kiti; na manispaa ni eneo la utawala katika mfumo serikali za mitaa na mamlaka inayoongoza serikali za mitaa katika eneo fulani la manispaa ndo huitwa halmashauri ya manispaa na kiongozi wake ni meya wajumbe ni madiwani pamoja na wataalamu katika hiyo manispaa mfano daktari mkuu wa manispaa, mhandisi mkuu wa manispaa, mkurugenzi mtendaji wa manispaa huyu ni mjumbe lakini ndo link kati ya serikali kuu na serikali ya mitaa na mara nyingi ndo mwajiri wa wataalamu katika manispaa husika.
 
Naona walimu mmeshuka vizuri sn; lakni km mtoa mada hapo juu na mm km mpitiaji wa thread hii; nimechanganyikiwa kidogo na majibu yenu waungwana; je kuna yeyote anayeweza kusummarize mada hii? Naona Kibirizi una nondo funguka tena pls
 
Hivi ukisema Halmashauri ya Manispaa na Manispaa ni kitu kimoja au tofauti?
 
Hivi ukisema halmashauri ya manispaa na manispaa ni kitu kimoja au tofauti

Ni Sawa Tu Na Kusema Mchezaji Simon Msuva Wa Yanga Na Klabu Kongwe Ya Mpira Wa Miguu Na Isiyo Na Maendeleo Nchini Tanzania / Duniani Ya Yanga. Umeelewa?
 
Back
Top Bottom