Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,046
Reaction score
12,545
Wadau naomba kuelimishwa, manake hili swali nimesikia watagazaji wanaulizana. Wenyewe hawana uhakika na wanatofautiana tu mitazamo hapa.
Kuna mmoja anasema Manispaa inaweza kuwa ndani ya Halmashauri.
Mwingine anasema Halmashauri inakuwa ndani ya Manispaa.

Kwa uelewa wangu Manispaa ni matokeo ya Halmashauri kuwa advanced tokana na Ongezeko la watu n.k

Which is which?
 
Uelewa wako ni sahihi kabisa.

Sasa Mkuu, ni vigezo gani vingine (licha ya Population growth) vinatumika ili kuipandisha hadhi Halmashauri kuwa Manispaa? Je inwezekana kwa eneo moja ndani ya wilaya kuwa Manispaa na rest ya wilaya ikabakia kuwa Halmashauri?

Kwa mfano: Inawezekana Kariakoo kuwa Manispaa halafu the rest of Ilala kuendelea kuwa Halmashauri au ni lazima Wilaya nzima ipande cheo?
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Nyote uelewa wenu mnafikiri kwa kutumia masaburi, Manispaa ni ngazi ya kimaendeleo na Halmashauri ni neno la kimamlaka, Ndo maana kuna Halmashauri hadi za Majiji
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa? 1. Halmashauri ya mji 2. Halmashauri ya manispaa 3. Halmashauri ya Jiji N.K
Ndiyo maana nimeleta hili swali ili nieleweshwe. Kama ningekaa kimya nisingepata kuyaelewa haya, na ningewapotosha na wengine. Thanks for sharing waungwana...
 
Wadau naomba kuelimishwa, manake hili swali nimesikia watagazaji wanaulizana.
Wenyewe hawana uhakika na wanatofautiana tu mitazamo hapa.
Kuna mmoja anasema Manispaa inaweza kuwa ndani ya Halmashauri.
Mwingine anasema Halmashauri inakuwa ndani ya Manispaa.
Kwa uelewa wangu Manispaa ni matokeo ya Halmashauri kuwa advanced tokana na Ongezeko la watu n.k
Which is which?
manispaa ni eneo la kiutawala wa kiserikali ya mitaaa lenye uwezo wa kujiendesha kwa sheria na utawala wake lakini usio wa kijiamulia kila jambo moja kwa moja ( semi autonomy) na mara nyingi eneo hili la utawala lina tengwa kwa kuzingatia idadi ya watu na huduma za watu ktk eneo husika. msingi wa hadhi ya manispaa nikuwa lazima eneo lifikie idadi fulani ya watu ambayo ni zaidi ya ile iliyowekwa kwa mji.idadi hii ya watu ktk manispaa inapozidi eneo hupandishwa hadhi na kuwa jiji.
halmashauri ni mamlaka inayoongoza na kusimamia haya maeneo ya kiserikali za mitaa. kwahiyo msimamizi wa kijiji, mji , manspaa na jiji ndiyo hiyo mamlaka inayoitwa halmashauri ya kila eneo kama nilivyotaja
 
Na Mji ambao haujafikia ukubwa wa kiwango cha manisapaa unaitwaje?

unaitwa Halmashauri ya mji (mf. Halmashauri ya Mji kibaha)
pia kwa uelewa wangu mdogo,eneo kubwa hasa ktk wilaya linaweza kuwa more advanced likapewa status ya kuwa mamlaka ya mji mdogo (mf. Kibaigwa,Makambako)
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Nadhani wewe ndo una matatizo. Mtoa hoja analengo zuri la kuelimisha jamii. Na nilivyokuona hata wewe mwenyewe hujui utofauti huo, hivyo tulia uelimishwe!
 
Hakuna tofauti kati ya Halmashauri na Manispaa, isipokuwa umekata maneno kwa sababu jina sahihi ni Halmashauri ya Manispaa ya ...... ie Mkoa wa Kigoma kuna Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji (Kigoma/Ujiji Municipal Council-KUMC), Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (Kigoma District Council - KDC), kuna Kibondo DC,Kasulu DC nk.
Sasa Tofauti ya Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Manispaa nafikiri ndio kusudio la msingi la swali lako, ipo hivi manispaa inapewa baada ya kuwa na vyanzo vya kujiendesha yenyewe angalau kwa asilimia fulani zaidi 30% (sina uhakika sana), pili idadi ya watu kwa eneo yaani population per unit area, watu wamesongamana kiasi gani, concetration per urea.
Kwa sababu idadi ya watu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ni kubwa ukilinganisha na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji lakini msongamano wa watu katika eneo dogo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni kubwa kuliko la Halmashauri ya wilaya ya Kigoma. Naomba nifafanue hapo kwenye msongamano ie unaweza kuta KDC watu 100 wanakaa kwenye wastani wa mita za eneo 1000 lakini lakini KUMC watu 100 wanakaa kwenye eneo la 500, na ndio maana utaona Halmashauri za manispaa nyingi zipo mjini, kwa mfano Dar es Salaam kuna Halmashauri za manispaa tu na hakuna Halmaahauri za wilaya yaani Kinondoni, Ilala and Temeke municipal Council.
Vile vile kuna wilaya hapo tusichanganye vyote viwili yaani Halmashauri ya Manispaa na wilaya zinaweza kuwa katika wilaya moja ie Kigoma/Ujiji Municipal Council and Kigoma District Council zote zipo KIGOMA DISTRICT.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri

Wengine wamemkejeli aliyeuliza lakini kichwani ziro kabisa..
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Sio kila member anajua kilakitu. Ndio maana ame post ili afahamishwe
 
Halafu huyu muliza swali atakuwa shabiki wa chadema.Kwa akili alizokuwa nazo lazima niamini hivyo
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Naomba nikuunge mkono, kwa kuongezea zaidi hivi ili hawa vijana waweze kuelewa.

Halmashauri ya Kijiji
Halmashauri ya Mji
Halmashauri ya Wilaya
Halmashauri ya Manispaa
Halmashauri ya Jiji.
 
Back
Top Bottom