Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Hakuna anaye jua kila kitu
 
manispaa ni eneo la kiutawala wa kiserikali ya mitaaa lenye uwezo wa kujiendesha kwa sheria na utawala wake lakini usio wa kijiamulia kila jambo moja kwa moja ( semi autonomy) na mara nyingi eneo hili la utawala lina tengwa kwa kuzingatia idadi ya watu na huduma za watu ktk eneo husika. msingi wa hadhi ya manispaa nikuwa lazima eneo lifikie idadi fulani ya watu ambayo ni zaidi ya ile iliyowekwa kwa mji.idadi hii ya watu ktk manispaa inapozidi eneo hupandishwa hadhi na kuwa jiji.
halmashauri ni mamlaka inayoongoza na kusimamia haya maeneo ya kiserikali za mitaa. kwahiyo msimamizi wa kijiji, mji , manspaa na jiji ndiyo hiyo mamlaka inayoitwa halmashauri ya kila eneo kama nilivyotaja
Na pia wanaangalia uwezo wa kujimudu kimapato anagalau kwa asilima 70/- ya mapato ya ndani.
 
Bado sijaelewa kabsa hizi tofauti, msaada tafadhali
Anza kusoma post zote toka ukurasa wa kwanza wz uzi huu mpaka ukurasa wa mwisho. Utaelewa. Mimi nimeelewa kwa kusoma ukurasa wa kwsnza tu wa uzi huu. Ila kama unataka kuwa deep kjjua tofauti ya halmashAUri na manispaa, basi fuata maelezo yangu hapo juu kwenye post hii.

karibu.
 
Ok asante sana mkuu!! Ngoja nifuatile
Anza kusoma post zote toka ukurasa wa kwanza wz uzi huu mpaka ukurasa wa mwisho. Utaelewa. Mimi nimeelewa kwa kusoma ukurasa wa kwsnza tu wa uzi huu. Ila kama unataka kuwa deep kjjua tofauti ya halmashAUri na manispaa, basi fuata maelezo yangu hapo juu kwenye post hii.

karibu.
 
VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MIJI, MANISPAA NA JIJI:

Vigezo vya ujumla

i. Jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa Wananchi kuwa mgumu

kwa sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au Visiwa.

ii. Kuwepo kwa miundombinu inayohitajika kwa eneo la utawala kuanzishwa,

iii. Kuwepo kwa mtandao wa barabara za uhakika kuunganisha Makao Makuu

ya eneo la utawala lililoanzishwa na maeneo mengine yenye kuhitaji

kuhudumiwa na Makao Makuu,

iv. Uwezo wa Serikali wa kuanzisha eneo jipya la utawala,

v. Utayari wa Wananchi kuchangia uanzishaji wa eneo la utawala.

Aidha, ili maeneo hayo yaweze kuanzishwa/ kupandishwa hadhi vimewekwa

vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007 (The Urban

Planning Act No 8 of 2007) Kipengele cha Tano cha Jedwali la Tano (Item

number 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-

Vigezo vya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo (Township

Authority)

Mamlaka ya Mji Mdogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Mamlaka

za Wilaya. Mamlaka hizi zinaanzishwa pale ambapo palikuwa ni Kijiji ambacho

kimeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Waziri mwenye dhamana

ya Serikali za Mitaa amepewa madaraka ya kutangaza Kijiji au Vijiji vilivyofikia

sifa zilizowekwa kuwa Mamlaka za Miji Midogo.

Vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa:

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua elfu kumi (10,000);

ii. Kuwe na huduma za jamii zifuatazo: Shule ya Sekondari, Kituo cha Afya

na Mahakama ya Mwanzo;

iii. Kuwe na Soko pamoja na Maduka ya rejareja yasiyopungua matano (5);na

iv. Eneo liwe ni Makao Makuu ya Kata au Tarafa.

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Mji (Town Council)

i. Kuwe na watu wasiopunga 30,000.

ii. Mji uwe na uwezo wa kujiendesha angalau kwa asilimia 50% ya bajeti

yake.

iii. Mji uwe na kiwango cha juu cha utoaji huduma ya hospitali, kuwe na

shule ya Sekondari, kuwe na angalau maduka ya rejareja yenye leseni

yasiyopungua 50, Kituo cha Polisi na pawe na Makao makuu ya Tarafa.

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Manispaa

i. Kuwe na watu wasiopungua laki moja (100,000)

ii. Kuwe na watu wasiopungua laki moja (100,000)

iii. Asilimia 30% ya wakazi wake wawe katika ajira isiyohusiana na kilimo

(Non agricultural Sector)

iv. Kuwe na walau kiwanda kikubwa kimoja (Manufacturing industry)

v. Kuwe na viwanda kadhaa vya “Processing

vi. Asilimia Sabini (70%) ya matumizi ya Manispaa yatokane na vyanzo vya

mapato ya Halmashauri (Own Sources).

vii. Kuwepo na huduma za jamii zifuatazo:-

 Kituo cha Elimu ya Watu Wazima;

 Hospitali ya Rufaa;

 Chuo Kikuu;

 Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa;.na kiwe ni Kituo cha Taasisi za

Kimataifa (Mult National organization.)

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Jiji

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua laki tano (500,000);

ii. Kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia tisini na tano (95%) kwa

mapato yake ya ndani; na

iii. Kuwepo sifa nyingine zaidi ya sifa za kawaida za Manispaa kama vile

maeneo ya kihistoria, maeneo ya utalii; Makao Makuu ya Mkoa; kituo cha

shughuli za Kimataifa na nyinginezo.
 
Ni kweli vigezo vipo wazi. Hata hivyo, kigezo cha kiuchumi hakizingatiwi kwa kuwa mapato yote ya uhakika yanachukuliwa na Central Government na hivyo hata uendeshaji wake unategemea central government. Jambo lililo wazi uwepo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa umesaidia kusogeza huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya eneo husika.
 
VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MIJI, MANISPAA NA JIJI:

Vigezo vya ujumla

i. Jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa Wananchi kuwa mgumu

kwa sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au Visiwa.

ii. Kuwepo kwa miundombinu inayohitajika kwa eneo la utawala kuanzishwa,

iii. Kuwepo kwa mtandao wa barabara za uhakika kuunganisha Makao Makuu

ya eneo la utawala lililoanzishwa na maeneo mengine yenye kuhitaji

kuhudumiwa na Makao Makuu,

iv. Uwezo wa Serikali wa kuanzisha eneo jipya la utawala,

v. Utayari wa Wananchi kuchangia uanzishaji wa eneo la utawala.

Aidha, ili maeneo hayo yaweze kuanzishwa/ kupandishwa hadhi vimewekwa

vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007 (The Urban

Planning Act No 8 of 2007) Kipengele cha Tano cha Jedwali la Tano (Item

number 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-

Vigezo vya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo (Township

Authority)

Mamlaka ya Mji Mdogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Mamlaka

za Wilaya. Mamlaka hizi zinaanzishwa pale ambapo palikuwa ni Kijiji ambacho

kimeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Waziri mwenye dhamana

ya Serikali za Mitaa amepewa madaraka ya kutangaza Kijiji au Vijiji vilivyofikia

sifa zilizowekwa kuwa Mamlaka za Miji Midogo.

Vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa:

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua elfu kumi (10,000);

ii. Kuwe na huduma za jamii zifuatazo: Shule ya Sekondari, Kituo cha Afya

na Mahakama ya Mwanzo;

iii. Kuwe na Soko pamoja na Maduka ya rejareja yasiyopungua matano (5);na

iv. Eneo liwe ni Makao Makuu ya Kata au Tarafa.

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Mji (Town Council)

i. Kuwe na watu wasiopunga 30,000.

ii. Mji uwe na uwezo wa kujiendesha angalau kwa asilimia 50% ya bajeti

yake.

iii. Mji uwe na kiwango cha juu cha utoaji huduma ya hospitali, kuwe na

shule ya Sekondari, kuwe na angalau maduka ya rejareja yenye leseni

yasiyopungua 50, Kituo cha Polisi na pawe na Makao makuu ya Tarafa.

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Manispaa

i. Kuwe na watu wasiopungua laki moja (100,000)

ii. Kuwe na watu wasiopungua laki moja (100,000)

iii. Asilimia 30% ya wakazi wake wawe katika ajira isiyohusiana na kilimo

(Non agricultural Sector)

iv. Kuwe na walau kiwanda kikubwa kimoja (Manufacturing industry)

v. Kuwe na viwanda kadhaa vya “Processing

vi. Asilimia Sabini (70%) ya matumizi ya Manispaa yatokane na vyanzo vya

mapato ya Halmashauri (Own Sources).

vii. Kuwepo na huduma za jamii zifuatazo:-

 Kituo cha Elimu ya Watu Wazima;

 Hospitali ya Rufaa;

 Chuo Kikuu;

 Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa;.na kiwe ni Kituo cha Taasisi za

Kimataifa (Mult National organization.)

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Jiji

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua laki tano (500,000);

ii. Kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia tisini na tano (95%) kwa

mapato yake ya ndani; na

iii. Kuwepo sifa nyingine zaidi ya sifa za kawaida za Manispaa kama vile

maeneo ya kihistoria, maeneo ya utalii; Makao Makuu ya Mkoa; kituo cha

shughuli za Kimataifa na nyinginezo.
Noted
 
Umeandika mengi lakini moja kubwa unalichanganya ni hili la hadhi ya jiji.
Bila kuathiri uwepo wa wilaya haiwezekani kwa wilaya kuwa na halmashauri itakayoitwa jiji.
Jiji ni hadhi ya kukua kwa mkoa pekee. Na halmashauri ya jiji hujengwa na halmashauri za wilaya ama manispaa kama ilivyo kwa Dares salaam.
Halmashauri ya wilaya inaweza kukua na kuwa manispaa na sio jiji.
Vipi ilala kwa sasa?? Naona ni tofauti na ulichoandika hapa.
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K
Acha ubinafsi... Toa elimu ku prove u-great thinker wako.

Wengine tumo humu kwa imani ya kuvuna knowledge toka kwa ma- genius kama wewe... Sasa genius ukianza kudemka kwa mipasho siye kina kajambanani tutafanya kazi gani sasa?!
 
Back
Top Bottom