Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

Ndugu yangu awamu ya tano ilipoingia madarakani kazi kubwa ya M/K CCM Taifa alifanya mabadiliko makubwa ya Wakuu wa Wilaya/Mikoa ambapo wale wazamani wengi wao walikuwa ni Makada Watiifu wa ccm. Sasa hawa wapya wengi wao sio wanasiasa bali walikuwa na majukumu yao mengine nje ya chama. Na uteuzi wao ni zawadi waliopewa na Mkuu kutokana na kazi waliofanya nakumpelekea Mkuu kufurahi. Hii ndiyo maana wamejawa na viburi. Na hata kwa baadhi ya Mawaziri wana tatizo hilo lakutokuwa na Maadili ya chama chao.
 
Tatizo la mgongano ni lilelile lililompa huyu mkuu wa mkoa cheo kutoka ukuu wa wilaya. Ili upandishwe cheo ni lazima uonyeshe masifa mengi sana na huwezi kujulikana kama huna drama drama za ajabu. Hivyo tatizo sio mkuu wa mkoa bali ni utamaduni mpya wa kutafuta vyeo. Hii ndiyo TZ mpya CCM oyee😆
 
Tatizo lipo kwa Mamlaka ya Uteuzi sio kwa wateuliwa

1) Principle of chain of command
Rais Au Waziri kuwasiliana Moja kwa Moja na DC na kumruka RC Ni Makosa , RC nae kuwasiliana Moja kwa Moja Na Rais bila ya kupitia kwa PM Au Waziri w Tamisemi Ni Makosa Pia Na ndicho kilichotokea,

2) Job description; haijawa clear kwa Kila Mtu kujua wajibu wake Na kwa Nani Ana report

3) Zamani nafasi Kama hizi Za RCs na DCs walikuwa wanapewa watu ambao tayari wana exposure ya kutosha Na kujua namna Serikal inavyofanya kazi Mf. Wakurugenzi wa Halmashauri wastaafu au Wakuu wa Idara ambao wanajua namna Serikal inavyofanya kazi

Paul Makonda, Ally Happy wameanzia Moja kwa Moja wameanza ajira ya kwanza wakiwa ma DC ni Sawa Na dereva kuanza Safar yake ya kwanza Kwenye Safar Za kimataifa Halafu umshangae Kwanini kasimama Kwenye 'Zebra'
Mbona joketi hana mambo ya Ali hapi na Makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RC Gambo mara nyingi amekuwa anatabasamu sana hata ukimkorofisha ,sasa pale DC kaonyesha nidhamu mbaya au dharau kwa mwenzake na RC kawa mpole sasa credit c kapata RC .hongera Gambo
 
Tulishasema kuwa kwa mikoa ambayo upinzani umeshamili na watu kujitambua ccm kuiongoza watapata tabu sana angalia Kilimanjaro angalia Arusha angalia Iringa na Mbeya moto unafukuta
Nimeona wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi wakiongelea kwa hisia tukio la Mkuu wa Mkoa Arusha ndugu yangu Mrisho Mashaka Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha ndugu yangu Gabriel Daqaro.

Bahati nzuri hawa wote ni marafiki zangu tofauti ni kuwa Dc wa Arusha siyo mwanasiasa kabisa lakini wote wawili wanafanana kuwa ni watu Wapole machoni pa watu.

Nakumbuka mwaka 2016 Mh Rc Arusha aliwahi kupatikana na tukio kama ili dhidi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye kwa sasa ni mkuu wa Mkoa Manyara Mdogo wangu Alexander Pastory Mnyeti ambapo Mheshimiwa Gambo aliamua kumtimua kwenye kikao.

Sijajua nini kinampata Mheshimiwa Mrisho Gambo sijui ule mwili wake Mdogo watendaji wa chini yake wanamdharau au sijui tatizo ni nini?

Matukio kama Haya inaonyesha jinsi ambavyo watendaji wa serikali hawaelewani na kama hawaelewani maana yake achievement inakuwa ndogo.

Hivi karibuni tulimsikia Waziri Mkuu akiwaagiza mawaziri kwenda mkoa wa Kilimanjaro kusuluhisha mgogoro kati ya Mkuu wa Mkoa na madc wake.

Kwa mantiki hii inayoonyesha kuwa kuna shida kubwa ya mahusiano ya kikazi kati ya hawa makamisaa.

Ningewaomba wanaccm tufanye utafiti sana kabla ya kuongea na kushutumu upande wowote.

Katibu mkuu wa ccm Dr Bashiru Ally aliwahi kutamka mikoa ambayo hakuna mahusiano mazuri ya kiutendaji kati ya chama na Serikali.

Mkoa wa kwanza ilikuwa Mara, Arusha, Dar es salaam na Mbeya lakini kiujumla mahusiano ya Viongozi hayako sawa sehemu nyingi.

Utakuta Madc hawaelewani na maded Marc na makatibu Tawala mikoa Marc na ofisi za chama hawaelewani mbaya zaidi siku hizi wanachama wengi wa ccm ni wafuasi wa Viongozi.

Wanachama wengi wa ccm siku hizi wanashabikia Viongozi kuliko chama.

Kwahiyo kila kiongozi kwa nafasi yake ametengeneza wafuasi wake.

Leo ukitaka kukosoa utendaji wa Viongozi ndani ya chama na serikali utaambiwa una wivu na matusi ya wafuasi utayaoga.

Na hata ili la Arusha wafuasi wa Viongozi wako busy kutetea wapambe wao suala maadili ya Viongozi wa chama hakuna anayejali.

Na hii tabia ya wafuasi wa Viongozi imetamalaki mpk kwenye ngazi ya maamuzi kila kiongozi ana Godfather wake Ndiyo maana hukawii sasa hivi ndani ya chama matamko ya wanachama hayaishi hata kama hayana tija kwa chama au taifa ili mradi aonekane.

Kusema ukweli mahusiano ya kikazi kati ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wasaidizi ina shida siyo mazuri sana.

Na Frey Cosseny

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wakitoana ngeu poa tu
Ukoo Wa Kambale huo kila mtu ana Sharubu...


Kila Mtu anajivunia kuwa karibu na mamlaka ya Uteuzi.

DC (mwana Kitengo) ana mvimbia RC (miongoni mwa watoto wapendwa wa Baba).

Uzuri wote ni magamba so ni heri tu wakiendelea kuparangana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Frey kumbuka UCHOMAJI WA MASHULE, ma-RC VIJANA WATATU ni JANGA
 
Back
Top Bottom