Kurmodosla
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 330
- 202
Mambo ya ngoswe mwachieni ngoswe
Frey kumbuka UCHOMAJI WA MASHULE, ma-RC VIJANA WATATU ni JANGA
Mimi nimenote msitari mmoja wanachama wa ccm ni wafuasi wa viongozi si wafuasi wa chama
Sent using Jamii Forums mobile app
Wapambe wanasema tofauti
Ukoo wa kambale.Yes. Wanachelewesha maendeleo sababu ya malumbano. Kulikoni wanatunishiana misuli?
Nimeona wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi wakiongelea kwa hisia tukio la Mkuu wa Mkoa Arusha ndugu yangu Mrisho Mashaka Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha ndugu yangu Gabriel Daqaro.
Bahati nzuri hawa wote ni marafiki zangu tofauti ni kuwa Dc wa Arusha siyo mwanasiasa kabisa lakini wote wawili wanafanana kuwa ni watu Wapole machoni pa watu.
Nakumbuka mwaka 2016 Mh Rc Arusha aliwahi kupatikana na tukio kama ili dhidi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye kwa sasa ni mkuu wa Mkoa Manyara Mdogo wangu Alexander Pastory Mnyeti ambapo Mheshimiwa Gambo aliamua kumtimua kwenye kikao.
Sijajua nini kinampata Mheshimiwa Mrisho Gambo sijui ule mwili wake Mdogo watendaji wa chini yake wanamdharau au sijui tatizo ni nini?
Matukio kama Haya inaonyesha jinsi ambavyo watendaji wa serikali hawaelewani na kama hawaelewani maana yake achievement inakuwa ndogo.
Hivi karibuni tulimsikia Waziri Mkuu akiwaagiza mawaziri kwenda mkoa wa Kilimanjaro kusuluhisha mgogoro kati ya Mkuu wa Mkoa na madc wake.
Kwa mantiki hii inayoonyesha kuwa kuna shida kubwa ya mahusiano ya kikazi kati ya hawa makamisaa.
Ningewaomba wanaccm tufanye utafiti sana kabla ya kuongea na kushutumu upande wowote.
Katibu mkuu wa ccm Dr Bashiru Ally aliwahi kutamka mikoa ambayo hakuna mahusiano mazuri ya kiutendaji kati ya chama na Serikali.
Mkoa wa kwanza ilikuwa Mara, Arusha, Dar es salaam na Mbeya lakini kiujumla mahusiano ya Viongozi hayako sawa sehemu nyingi.
Utakuta Madc hawaelewani na maded Marc na makatibu Tawala mikoa Marc na ofisi za chama hawaelewani mbaya zaidi siku hizi wanachama wengi wa ccm ni wafuasi wa Viongozi.
Wanachama wengi wa ccm siku hizi wanashabikia Viongozi kuliko chama.
Kwahiyo kila kiongozi kwa nafasi yake ametengeneza wafuasi wake.
Leo ukitaka kukosoa utendaji wa Viongozi ndani ya chama na serikali utaambiwa una wivu na matusi ya wafuasi utayaoga.
Na hata ili la Arusha wafuasi wa Viongozi wako busy kutetea wapambe wao suala maadili ya Viongozi wa chama hakuna anayejali.
Na hii tabia ya wafuasi wa Viongozi imetamalaki mpk kwenye ngazi ya maamuzi kila kiongozi ana Godfather wake Ndiyo maana hukawii sasa hivi ndani ya chama matamko ya wanachama hayaishi hata kama hayana tija kwa chama au taifa ili mradi aonekane.
Kusema ukweli mahusiano ya kikazi kati ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wasaidizi ina shida siyo mazuri sana.
Na Frey Cosseny
Sent using Jamii Forums mobile app
Rc anaejielewa ni wa Tabora pekee yake wengine mizingo.....
Anaeona nimeandika pumba, anyooshe mkono juu, jifanye unajikuna
RC wa Arusha kama sikosei ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera. Ana sura ya upole lakini ni mkorofi.Gabriel Qadaro mkuu wa wilaya wa Arusha ni mtu makini na muadilifu ni kijana aliyepikwa na siyo mwanasiasa. Mafunzo aliyolipitia ni ya moja jumlisha moja ni mbili. Mara nyingi ni mtu wa kuchagua maneno na hapendi mbwembwe kwenye utendaji anafikiri kabla ya kutenda na anahakikisha ana taarifa sahihi kuhusu jambo husika. Mkuu wa mkoa wa Arusha ni mtu wa mihemeko japo ni darling wa watawala kwa hulka yake ya kupenda sifa. Ni msema hovyo kama ilivyokuwa kule Korogwe alipomtukana mwanadada yule mwanasheria ya halmashauri Korogwe kuhusu degree yake. Vilevile aliwahi kutoa matamshi ya kibaguzi wenye Baraza la UVCMM mkoa wa Pwani kwamba raisi hawezi kutoka kazkazini. Ushauri wangu ni kwamba viongozi watakuja na kupita lakini Tanzania itasimama daima hivyo basi tuijali Tanzania kuliko hawa viongozi wasema hovyo. Tusipotilia hili matamanio litatugharimu kama taifa huko tuendako.