Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

RC wa Arusha kama sikosei ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera. Ana sura ya upole lakini ni mkorofi.

DC anaonekana anavumilia mengi kutoka kwake wakati kamera zikiwa mbali na wao wawili.

Ngosha anapenda hulka za huyo RC tatizo ni kwamba dhamana ni kitu chenye mipaka ya muda.
Rc mtoto wa Ilala mchikichini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RC wa Arusha kama sikosei ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera. Ana sura ya upole lakini ni mkorofi.

DC anaonekana anavumilia mengi kutoka kwake wakati kamera zikiwa mbali na wao wawili.

Ngosha anapenda hulka za huyo RC tatizo ni kwamba dhamana ni kitu chenye mipaka ya muda.
Dc mtoto wa Rchuga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi wakiongelea kwa hisia tukio la Mkuu wa Mkoa Arusha ndugu yangu Mrisho Mashaka Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha ndugu yangu Gabriel Daqaro.

Bahati nzuri hawa wote ni marafiki zangu tofauti ni kuwa Dc wa Arusha siyo mwanasiasa kabisa lakini wote wawili wanafanana kuwa ni watu Wapole machoni pa watu.

Nakumbuka mwaka 2016 Mh Rc Arusha aliwahi kupatikana na tukio kama ili dhidi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye kwa sasa ni mkuu wa Mkoa Manyara Mdogo wangu Alexander Pastory Mnyeti ambapo Mheshimiwa Gambo aliamua kumtimua kwenye kikao.

Sijajua nini kinampata Mheshimiwa Mrisho Gambo sijui ule mwili wake Mdogo watendaji wa chini yake wanamdharau au sijui tatizo ni nini?

Matukio kama Haya inaonyesha jinsi ambavyo watendaji wa serikali hawaelewani na kama hawaelewani maana yake achievement inakuwa ndogo.

Hivi karibuni tulimsikia Waziri Mkuu akiwaagiza mawaziri kwenda mkoa wa Kilimanjaro kusuluhisha mgogoro kati ya Mkuu wa Mkoa na madc wake.

Kwa mantiki hii inayoonyesha kuwa kuna shida kubwa ya mahusiano ya kikazi kati ya hawa makamisaa.

Ningewaomba wanaccm tufanye utafiti sana kabla ya kuongea na kushutumu upande wowote.

Katibu mkuu wa ccm Dr Bashiru Ally aliwahi kutamka mikoa ambayo hakuna mahusiano mazuri ya kiutendaji kati ya chama na Serikali.

Mkoa wa kwanza ilikuwa Mara, Arusha, Dar es salaam na Mbeya lakini kiujumla mahusiano ya Viongozi hayako sawa sehemu nyingi.

Utakuta Madc hawaelewani na maded Marc na makatibu Tawala mikoa Marc na ofisi za chama hawaelewani mbaya zaidi siku hizi wanachama wengi wa ccm ni wafuasi wa Viongozi.

Wanachama wengi wa ccm siku hizi wanashabikia Viongozi kuliko chama.

Kwahiyo kila kiongozi kwa nafasi yake ametengeneza wafuasi wake.

Leo ukitaka kukosoa utendaji wa Viongozi ndani ya chama na serikali utaambiwa una wivu na matusi ya wafuasi utayaoga.

Na hata ili la Arusha wafuasi wa Viongozi wako busy kutetea wapambe wao suala maadili ya Viongozi wa chama hakuna anayejali.

Na hii tabia ya wafuasi wa Viongozi imetamalaki mpk kwenye ngazi ya maamuzi kila kiongozi ana Godfather wake Ndiyo maana hukawii sasa hivi ndani ya chama matamko ya wanachama hayaishi hata kama hayana tija kwa chama au taifa ili mradi aonekane.

Kusema ukweli mahusiano ya kikazi kati ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wasaidizi ina shida siyo mazuri sana.

Na Frey Cosseny

Sent using Jamii Forums mobile app

Kikawaida na kwa nchi ambayo mifumo ya kiutawala iko strong, kasoro na tofauti za viongozi kama hizi zinaweza kuonekana mapema sana na kurekebishwa kabla hazijaibuka hadharani...

Ni kweli kabisa, kitendo cha mdogo (DC) kutofautiana hadharani na aliye juu yake (RC) tena wote wakiwa meza kuu kama inavyoonekana kwenye video clip inayotembea kwenye mitandao ya kijamii, ni kweli inaashiria kuna jambo kubwa haliko sawa....

Wakati mwingine sisi wengine huku nje raia wa kawaida tunaweza bila shaka yoyote kuthibitisha kuwa hizi ndizo dalili za ufalme uliofitinika....

Ipo siku Rais atapingwa hadharani na IGP ama CDF wake na ndipo hapo ufalme unapokuwa umeanguka rasmi..
 
Namaanisha wandani (wasiri) wake.
Hivi kati ya Gambo na huyu nani ana siri na Rais
IMG-20190106-WA0111.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rc anaejielewa ni wa Tabora pekee yake wengine mizingo.....

Anaeona nimeandika pumba, anyooshe mkono juu, jifanye unajikuna
Kuna yule aliyesifiwa na Rais, somebody Amos he's the best! Hata jinsi anavyowatreat upinzani utadhani sio mteule wa jiwe.
 
Msisahau kuwa mrisho gambo aliipata hiyo nafasi baada ya kumfanyia figisu Ntibenda
 
Ki ufupi kwenye clip sikuona kosa la Gambo ambalo lingemfanya DC kuwa na hasira za aina ile labda kama kulikuwa na tofauti zao hapo kabla hawajaingia kwenye kikao.

DC hana busara
 
RC mwenye vimelea vya uongozi pekee Tanzania ni "Mtaka" Simiyu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika Mtaka Anthony ni kiongozi Mwenye karama na sifa zote za uongozi.

Hawa wengine type ya kina Bashite, Hapi na Mgambo wa Arusha wanabebwa na mbeleko ya mfumo wa kifuasi na kiki tu.
 
Back
Top Bottom