Nini maana ya maneno haya?

Nini maana ya maneno haya?

mzee, wewe si ndio mleta uzi??

basi pambana na swali.

Kilichinifanya nikuulize ni aina yya swali lako

Hakuna mahali nimesema mama katupwa,sasa nikadhani kuna mtu mwingine kasema hivyo ndio maana nikakuuliza!
 
Kilichinifanya nikuulize ni aina yya swali lako

Hakuna mahali nimesema mama katupwa,sasa nikadhani kuna mtu mwingine kasema hivyo ndio maana nikakuuliza!
basi usijali kiongozi, haya jibu swali kama lilivyoulizwa...
 
basi usijali kiongozi, haya jibu swali kama lilivyoulizwa...

Sasa mkuu nitajibuje kitu ambacho sijakisema?

Kwenye mada yangu sijasema mama katupwa sasa nitajibu nini?
 
Ngoja nijitwike mimba tena ya Mapolomoko (unajua aliishia darasa la sita hata kuandika vizuri hajui?) halafu nione utafanyaje. tena mshua unamtegea sana maza kwenye kulea
Naapa kwa jina la mama na baba yangu sijawahi kumlaumu mama yako kwa lolote hata pale ulipofeli mitihani yako ya kidato cha kwanza.........
Nimekuwa nikiwajibika pale ninapohisi nina mchango katika jambo lolot ambalo halikuenda sawa katika familia au hata katika shughuli zangu za kawaida. Kwa hiyo naamini hilo ulilosema hapo juu niko nalo mbali mwanangu

Toka hapa na wewe, lione. Nilirisiti na nikafaulu!
Afadhali .........!!
 
Last edited by a moderator:
Mwana -------- huwa mzigo kwa mamaye hii ni kwasababu toka asili ya uumbaji jukumu alilopewa mwanamke kuwa

MSAIDIZI wa mwanaume, wote tunajua baba ni kiongozi mkuu wa familia na mama ni msaidizi, Baba anatoa muongozo

mama kazi yake kama msaidizi ni kutekeleza,na pia kiongozi huyu aweza kuwa na madhaifu lakini mama kama msaidizi

ni kusaidia zile sehemu ambazo kuna udhaifu aweze kuzikacover,ndiyo maana mwana akiwa -------- mzigo

unamwangukia yeye kwamba inawezekana yeye kama msaidizi alishindwa kuziba pengo liloshindwa kusimamiwa na baba.


Lawama lazima zimwangukie Mama Kwa mwana kuwa -------- kwasababu Muumbaji mwenyewe alitaka iwe hivyo kwa jukumu

alilompa,kwanini alichukua mbavu na si kiungo kingine? kazi ya mbavu ni kuvilinda viungo muhimu kama moyo,figo

maini n,k visiharibike,kazi nyingine ni kuwezesha upumuaji kwenda sawa,na mwisho kukamilisha umbo zima la mwili

liwe katika muonekano mzuri,hapa jukumu zima la mwanamke katika familia liko hapa,jambo haliko sawa lazima liwe

mzigo kwake,hapa ni ushahidi tosha kwamba mwanaume ana madhaifu mengi sana lakini madhaifu hayo yanafichwa na

mwanamke anaposimamia vyema jukumu lake,na hii hupelekea kuwa na familia bora.


Katika sehemu nyingine ya Biblia inasema Mungu ameumba jambo jipya duniani kwamba MWANAMKE ATAMLINDA

MWANAUME,hii ni sababu tosha kwamba mambo yakienda mlama lazima iwe mzigo wake,yeye kama mlinzi anapaswa

kuhakikisha kila mmoja ndani ya familia yuko vizuri,baba kama mtawala anaweza asione kitu kwamba adui

kashambulia familia yao lakini yeye mama kama mlinzi ni rahisi kuona kwamba himaya yao imevamiwa.


Sehemu nyingine inasema ajipatiaye MKE apata kitu CHEMA,hii ni dhahiri kabisa MWanaume anapopata mke mwema

amepata kitu safi kinachomfaa kwa ustawi wa maisha yake na kizazi chake,hapa mambo yakiwa mlama lazima iwe mzigo

kwa mama kwamba si kitu chema kwa familia.


Mithali 31:10-11 unasema... Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato

Mithali 31:27-29 inasema...Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.


Hizo ndizo sifa za mke mwema,kwanza moyo wa mumewe umemuamini/ anaaminika kwamba atalea na kuongoza mambo ya

familia vizuri,pili ni jukumu lake kama msaidizi na mlinzi kuangalia njia za watu wa nyumbani mwake,mwisho

akiweza lazima asifiwe na hapa hata ule mstari wa kwamba mwana mwenye hekima humfurahisha babaye unapatikana

hapa kwasababu mama amesimamia vyema jukumu lake na pia baba atamsifu atamwambia nimeona wanawake wengine

wakifanya mengi lakini wewe umewapita wote, na akishindwa basi itakuwa mzigo kwake na pia inasindikiza ule

mstari mwingine usemao MWANAMKE -------- HUBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE si kwa maana ya kuachana

baba na mama tu bali na mambo kama haya ya malezi,akishindwa kuwa mwelevu lazima iwe mzigo kwake na familia

yake itabomoka.
 
KWA MTAZAMO WANGU:

kwanini maandiko haya yalisemwa na kwanini yaliwekwa
katika mtazamo wangu mm naona kuwa wazazi wote ni vyema wakatambua umuhimu wa kuwalea watoto wao katika kicho cha kumpendeza Mungu na kusikiliza yale mausia yao wazazi ndipo suala zima la upotokaji au ukiukwaji wa mitoto inakuja pale inapokuwa imebalehe kwani haisikilizi tena yale mausia wala yale mafundsho wayapatayo lkwa wazazi wanakengeuka ndipo suala zima la hayo maandiko yanayosema kuwa mtoto -------- ni mzigo kwa mamaye bali mwenye hekima ni furaha kwa babaye hivyo yule mtoto ambaye amekengeuka anakuwa mwiba kwa mama bali mwenye hekima anakuwa kwa babaye sijui kwanini hii msemo imekuwa hivi inanishangaza sana kwani majukumu mengi ya kukifyatua hicho kitoto kilikuwa mkononi mw amama na kukkilea ni mama sasa nashanga kuona kuwa anakuwa mwiba/mzigo kwa mama
 
Mimi nadhani mtoto akiwa na tabia njema na maadili na mafanikio pia anafanya familia hasa baba awe na furaha na pengine ajivunie sbb baba ndiye kichwa ca=ha familia, innapokuwa kinyume inakuwa shida hasa kwa mama sababu kihistoria mama ndiye mlezi wa familia, hiyo ya kuwa mzigo maana yake ita muwia vigumu na kumfanya mama kama mlezi kutumia effort kubwa kumrudisha mtoto huyo kwenye mstari.

Mtazamo wangu tuuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom