Wana JF wenzangu naomba tuungane katika jambo hili...

Wana JF wenzangu naomba tuungane katika jambo hili...

Status
Not open for further replies.

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Natumaini kwa uwezo wa Mwenye Enzi Mungu wote hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.

Nia na madhumuni ya kuanzisha uzi huu ni kutaka kumuunga mkono nduguyangu na shemeji yangu Elli pamoja na uongozi mzima wa jamii Forum kuhusianana uamuzi wao wa kuandaa hafla fupi ya kuwatembelea wagonjwa pale Ocean Road na kuto msaada.

Awali hafla hiyo ilipangwa kufanyika siku ya sikukuu ya sabasaba, lakinikutokana na maandalizi kutokamilika waandaaji waliahirisha na kuamua hafla hiyofupi ifanyike siku ya sikukuu ya nane nane yaani siku ya Ijumaa ya tarehe 8/8/2014.

Kiwango cha chini kabisa cha kuchangia ili kukamilisha hafla hii ambapofedha hizo zitatumika Kununulia mahitaji muhimu kwa wagonjwa waliolazwa paleOcean Road ni shilingi 20,000, lakini si vibaya kama kwa wale wenye uwezowataongeza kwani mahitaji ni mengi lakini kwa kujitolea kwa kiwango hichonaamini tutamudu kufikisha ujumbe kwa wagonjwa na uongozi wa hospitali hiyo kwambauongozi wa jamii Forum pamoja na sisi wadau wake tunawajali na tunashirikinao kwenye madhila yao.

Mpaka sasa maandalizi muhimu yamekwishafanyika ikiwepo kupata kibali chakutembelea hospitali hiyo ili kuwasilisha misaada hiyo.

Michango yote itumwe kwa namba hii hapa 0765-949146 na wotewatakaochangia ID zao zitawekwa katika uzi huu kama kumbukumbu lakini hatutajakiwango cha fedha zilizochangwa kwa kila mtu.

Naamini kwamba siyo wote watakaochangia watajitokeza siku hiyo katikakushiriki kwenye hafla hiyo, kwa sababu wengine wanaweza kuwa wametingwa nashughuli zao za kila siku na bila kuwasahau wale ndugu zangu wa mikoani.

Nawaomba sana tena sana tushirikiane katika jambo hili maana kutoa nimoyo na si utajiri, wenzetu wanahitaji misaada kutokana ha hali zao, na wotehapa hakuna anayejua kwamba kesho ataamka akiwa katika hali gani kwani mitindoya maisha tunayoishi pamoja na vyakula tunavyokula vyote hivyo vinatuwekakatika hatari ya kupata ugonjwa huo wa kansa.

Ndugu zangu ambao tumekuwa tukishirikiana katika ile mikutaniko yetu yaLEO TUPO HAPA PUB, nawaombeni tuungane katika jambo hili. Najua kabisahamtatuangusha kwani mara nyingi tumekuwa pamoja na hapa nitawataja wachachekwa msisitizo:

UP DATE:

Mpaka sasa tumeshapokea michango ya wadau wafuatao:

1. Jamii Media ( Jamii Forum)
2. AshaDii
3. Elli
4. Mtambuzi
5. Everlenk
6. TANMO
7. Power to the People
8. Neylu
9. miss chagga
10. Zion Daughter
11. Asnam
12. sister
13. Fixed Point
14. Babu DC Dark City
15. NANDERA
16. sosoliso
17. Ruttashobolwa
18. Husninyo
19. amu
20. tinna cute ( AshaDii to confirm)
21. lin ( AshaDii to confirm)
22. jouneGwalu
23. Nameless
24. monaco

UP DATE - 5/8/2014

Wakuu kwa kuwa tunajipanga sasa kununua mahitaji kamati ya maandalizi imeamua mwisho wa kupokea michango ni kesho.

Tunaomba wale ambao waliahidi kutuma michango yao wafanye hima ili tukamilishe zoezi hili kwa ufanisi.

Ahsanteni sana

Kaka zangu Asprin, KakaKiiza, Jiwe Linaloishi, Mwita Maranya, Ruttashobolwa jouneGwalu, TANMO, Bigirita, The Boss, ayanda, Superman, sosoliso, DARKCITY, Mwanyasi, Matola, Mentor, Pasco, Himidini, Mr Rocky, LiverpoolFC Mungi, kitalolo, PakaJimmy, Don Mangi, Filipo, Mzee wa Rula, Kaizer

Dada zangu wapendwa, snowhite, cacico, Fixed Point, gfsonwin madameB, KOKUTONA, Arabela, farkhina, lara 1, kashesho, miss chagga miss neddy, miss strong, Karucee, Tina, charminglady, Zion Daughter sister, Paloma, Nivea, Neylu, mwallu, Preta, marejesho, Nyamayao , Kaunga, Ennie

Bila kuwasahau wanangu kina, Asnam, @King'ast, MwanajamiiOne Husninyo, Lisa na wengineo ambao nimewasahau kutokana na kughafilika lakininia na madhumuni yangu ni kutaka ujumbe huu umfikie kila mdau wa jamii Forumwakiwemo wale wasomaji wetu ambao kila uchao lazima wapitie mtandao huu nakujifunza kupitia uzoefu na habari motomoto.

Naomba tuungane jamani…………..
 
Last edited by a moderator:
wazo zuri sana ila nataka kujua je ni lazima mtu achangie hela? Vipi michango ya inkind haifai kwa watu walio karibu? Na kwa mawazo yangu nadhani msingeweka limitation ya mchango (20,000) minimum. Kwa hiyo wenye elf 5, 10, 15 vp hawa? Na ingekuwa bora muweke namba zote voda, tigo, na airtel maana kuna kwingne unakuta kuna airtl money zaid ya mpesa and the like.
 
Ahsante kwa ushauri ....
Elli nakuomba uje hapa kwa ufafanuzi tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa ushauri ....
Elli nakuomba uje hapa kwa ufafanuzi tafadhali
Mpwa wangu kilambalambila haina sababu yoyote ya kuchangia pesa kama huna, waweza kutoa hata materials tu maana imani yetu ni kwamba japo wagonjwa wale mahitaji yao ni very selective lakini hayalingani hivyo kama hawatumii sabuni aina fulani lakini kuna mwingine atakua anaitumia au nguo au chochote kile chenye msaada kwao.

Tukumbuke kuwa kuna wengine wako na wasaidizi wao ambao wao hawana masharti, hivyo tunaweza kupeleka tu. Mchango hauna kiwango ni kadiri MUNGU atakavykujaalia tu
 
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi
 
Last edited by a moderator:
Naomba niwe radhi kutoa mchango huu kaka Mtambuzi.
Unajua kutoa misaada ni jambo jema sana mbele za Mungu.
Tumefanya sana matumizi LTHP.....sasa ni zamu ya kupeleka matumizi yetu kwa wahitaji mbalimbali.
Tuko pamoja.....nitawasilisha mchango wangu mara moja.
......BTW Shikamoo Kaka
 
Last edited by a moderator:
Kweli Kongosho hapo naona majanga!
Ishiiiiiiiiii hii ni supu ya nyama za binadamu, kama wewe huwezi kung'ong'osa mfupa kunywa mchuzi na utokee mlango uleeee! Mbona mkeo huwa tunakuwaga nae hapa.

Ishiiiiiiiiii hii ni supu ya nyama za binadamu, kama wewe huwezi kung'ong'osa mfupa kunywa mchuzi na utokee mlango uleeee! Mbona mkeo huwa tunakuwaga nae hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom