Ee, huo msemo nao ni mgeni kwangu. Kala muamala? Mimi najua ukituma au kutoa pesa benki hapo unakuwa umefanya muamala. Kiswahili kinakua haraka!Wanamaanisha mtoa mada kala muamala..
Kha! Huo tena msemo mpya. Chai bubu? Salalee!hii yenyewe umeleta ni chai bubu tuu
Ametuletea chai ya MapapaiMleta mada ametupanga.
Loo, mnazidi kunichanganya. Mnaitoa wapi hiyo misemo? Ametupanga? Mi najua tu kupanga foleniMleta mada ametupanga.
Mtanivunja mbavu jamani. Chai ya mapapai? Hiyo itakuwa chai au juisi.Ametuletea chai ya Mapapai
Habari ya kutengeneza au kutunga iliyojaa uongo ambao mtoa mada hujitahidi kuifanya ya kweliWakuu, poleni na majukumu. Naomba kuuliza nini maana ya maneno haya kama yanavyotumika hapa JF:
1. Chai ya moto
2. Chai ya tangawizi
3. Chai kavu
Nimeyaona yakitumiwa na wachangiaji wa nyuzi mbalimbali ila mimi sielewi wanamaanisha nini wanapoyatumia. Naomba kujuzwa ili twende pamoja
Umewahi husianisha kati ya kinachoitwa chai na kilichoandikwa?
Laa. Nimeachwa kwenye mataa.Hii nayo mbona kama chaiView attachment 1788883
Kapitie tena kule thread ya Kula kimasihara, soma pages hata page 3 za mwisho kisha ukiona maelezo ya mtu yameqotiwa kuwa ni chai ,jiulize wewe kwa upande unaonaje ? Kama chai kadhaa za kule hautaelewa kuwa ni chai ,basi unasafari ndefuLaa. Nimeachwa kwenye mataa.
Asante sana, mkuu. Nimeridhika na jibu lako. Hao wengine walikuwa wananichora tu.chai ni story za kutunga... sasa watu huongeza vionjo vingine mfano: hii ya leo mbona haina vitafunwa, au chai haina sukari kabisa, au umejaza tangawizi, kulingana na vionjo tuu vya mwandish, shabaha ya kusema chai ni mhusika ametoa hadithi ambayo haina uhalisia..
Nimeishaelewa, mkuu, maana ya chai. Wachangiaji wote wa mwanzo walikuwa wananionjesha chai baridi.Kapitie tena kule thread ya Kula kimasihara, soma pages hata page 3 za mwisho kisha ukiona maelezo ya mtu yameqotiwa kuwa ni chai ,jiulize wewe kwa upande unaonaje ? Kama chai kadhaa za kule hautaelewa kuwa ni chai ,basi unasafari ndefu