Nini maana ya Makonda ‘kuwanyima watu haki ya kuishi’ kunakosemwa na serikali ya Marekani?

Tumeridhika na Utanzania wetu, kaeni na umarekani wenu, kamwe hatutauza utu wetu kwenu,Naipenda Tanzania nitabaki Mtanzania hata nikingia marekani nitarudi Tanzania, kwanza naingia kufanya nini???Long Live Paul Makonda, Hakika kweli tunapiga hatua siku zote ukiona hawa marekani wamenza kukupiga vita vya vikwazo ujue taifa lako linaendelea.....

Hatutaki ushoga, wala hatupashani Taarifa na mashoga
 
Katazo hili kwa kiasi kikubwa tunaweza kusema ni kuhusu kauli zake kwenye mambo ya ushoga. Tangu atoe lile tamko la kukurupuka, nchi za Magharibi hazikufurahishwa kabisa.

Haya mengine wameyaweka tu kwani wanajua wangesema tu ni ushoga basi wananchi wengi wange-react negatively! Tusidanganyane eti wamekasirishwa na manyanyaso yake kwa raia. All in all, wakulaumiwa hapa ni rais mwenyewe.

Huyu Makonda alikwishaonyesha kabisa ni mtu asiye na busara ya uongozi, hafanyi kazi yoyote bali ni msanii na mabovu mengine mengi lakini kwa sababu anazojua aliyemteua hataki kumwondoa. Hata wananchi wengi wa Tanzania hawampendi na Makonda mbaya zaidi anasababisha chuki kati ya serikali na wananchi.

Yaani ubongo wake umejaa uji uji!
 
Tumeridhika na Utanzania wetu, kaeni na umarekani wenu, kamwe hatutauza utu wetu kwenu,Naipenda Tanzania nitabaki Mtanzania hata nikingia marekani nitarudi Tanzania, kwanza naingia kufanya nini???Long Live Paul Makonda, Hakika kweli tunapiga hatua siku zote ukiona hawa marekani wamenza kukupiga vita vya vikwazo ujue taifa lako linaendelea.....

Hatutaki ushoga, wala hatupashani Taarifa na mashoga
Hii semina ya kuambizana mueneze hoja ya ushoga kwenye mitandao ya kijamii kwamba ndo sababu mmeipiga kwa siku ngapi na mmelipwaje jomba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unakiri hadharani kwamba Makonda ameua watu kama Marekani ilivyofanya kwa jenerali wa Iran ?
A crackdown on freedom of expression has been on the rise since President John Magufuli came into office in 2015.

Human rights groups also accuse Mr Magufuli of repressing political dissent, detaining human rights activists, and muzzling the media.
 
Hatuna cha kupoteza eti kwa kumzuia RC Makonda kwenda Marekani. Kwanza wajiulize tangu Rais wetu John Pombe Magufuli aingie madarakani alishawahi kwenda ubarozi wa Marekani nchini kuomba Viza ya kuingia Marekani? Ukweli ni kwamba hajawahi kwahiyo RC Makonda aende Marekani kutafuta nini ambacho bosi wake haoni haja?
Hamna cha kupoteza lakini 20/12/2019 RC alipopata refusal ya kuingia USA machozi yalimtoka.
 
Makonda ni Israil mtoa roho, usiombe ukatishe kwenye 18 zake.
IMG-20141102-WA0010.jpg


Mzee Warioba popote ulipo pokea salamu yangu
 
Ina maana makonda amewahi kuwa? Alimuuwa nani ? Hii dunia ina siri sana . lakini mwisho wa siku Mungu akiamua kukuumbua anakuumbua.
 
.
Katika sababu zilizotajwa kwa Makonda kuzuiliwa kwenda Marekani ni "kuwanyima watu haki ya kuishi na usalama wao" Hi ni sentensi nzito kwa watu wanaofikiria mambo kwa umakini, kwa kuwa unapomnyima mtu haki ya kuishi ina maana huyo mtu haishi tena, hayuko hai tena kwa kuwa umeondoa haki yake ya kuishi, au umemnyima haki yake ya kuwa hai - umemuua. Hilo ndilo wanalosema USA juu ya Makonda.

Watu wengi wanafikiria kwamba Makonda amezuiliwa kwenda USA kutokana na msimamo wake juu ya suala la ushoga, lakini ni wazi kutokana na kauli ya USA kwamba kuna zaidi ya hilo. Je kuna mambo ambayo Watanzania tumefumbwa kwa muda mrefu sana na serikali yetu lakini USA wana taarifa zote?

Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusiana na watu kuuwawa, kutekwa na majaribio ya kuuwawa ncini ambazo serikali haijawa wazi sana kuzieleza au kuonyesha kuwa inayafanyia kwa uzito upelelezi wa hayo matukio. Kuna dalili basi, kwamba hawa USA wana ufahamu wa haya mambo kuliko tunavyofikiria.

Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi. Lakini kwa sasa, Makonda kutuhumiwa kwamba amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi ni jambo kubwa sana!

Reference:Makonda apigwa 'stop' kuingia Marekani

View attachment 1343097


Jr
 
Sasa kumnyima Visa ya kuingia Marekani ndo watazuia juhudi zake na serikali kupiga vita madawa ya kulevya na genge la madawa ya kulevya paomoja na ushoga? Ataendelea tena kwa saana kwasababu amewashika pabaya! Moja ya mikakati ya USA ni kuungana na magenge ya uhalifu wa kimataifa kuzinyongonyeza nchi masikini ili wapore mali na utajiri wa nchi za kiafrica. Moja ya mbinu inayozitumia marekani ni pamoja na kusupport magenge ya madawa ya kulevya kuingizwa katika nchi masikini kuharibu vizazi ili kutengeneza mwanya wa kuzipora rasilimali zao!
Kichwa unacho Ila akili nina wasiwasi Kama unayo, hakuna sehemu kwenye taarifa ya USA inazungumza juu ya hoja ya madawa, na kwa wajinga wasiofatilia ndiyo wanaamini juu ya upambanaji feki wa madawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani jaribuni kunielewa. Mimi hata siku moja sikatai kuwa jamaa anatumia madaraka vibaya, ni msanii na hakuna kazi yoyote anayofanya zaidi ya kujionyesha, na pia amelewa madaraka. Issue yangu ni kuwa pamoja na haya madhambi yoooote asingekuwa ameropoka suala la ushoga wala wasingemgusa.
Kuna watu kibao ambao hawajapigwa ban ila wamepinga ushoga na kuchukua hatua,ushoga hapa sio issue!
 
Back
Top Bottom