Nini maana halisi ya kuzini (You shall not commit adultery)

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
10,087
16,013
Rejea kichwa cha habar,

Nimesoma maana nzima ya amri hiyo kutoka maeneo mbalimbali,kwa lugha ya wenzetu na pia lugha yetu, ikimaanisha,..adultery ni sexual relation ambayo atleast mmoja wa wahusika ni mtu aliye kwenye ndoa..

Sasa swali langu ni kwamba; je, kwa hawa ma girl friend na ma boy friend ambao bado hawajaingia kwenye ndoa wanapofanya hilo tendo,je wanafanya makosa?..

Ni kweli mtu akishajihalalisha kwa watu na mashahidi tena kwa document za ndoa mkaoana,na kukubaliana kwa maandish kua huyu ni wangu na sitokwenda kwingine, then anapovunja masharti hayo ni kweli anafanya makosa..

Sasa mim na GF wangu ambao hatujafunga ndoa tunapofanya mchezo huu tuna makosa gani au tunamkosea nani na kuna ubaya gani?
 
Inategemeana na imani yako,kwa mfano mkristu au muislam huamini kuwa uasherati ni dhambi na mashahara wa dhambi ni mauti,yaani kifo na adhabu ya milele motoni,ila kama unaimani tofauti na hivyo basi hufanyi kosa,soo ninafsi yako na unavyo amini.
 
Uasherati ni dhambi?..na kosa lake ni nin mi kuridhiana na dem wangu tena kwa furaha zote.
Kama hauamini katika imani yeyote, basi ni halali yako kuona sio dhambi....
Hivo unaweza hata kuiba kisha ukaona sio dhambi kwasababu hukua nacho hivo umeiba umepata
 
Hio ni definition ya wazungu
Kwao kusex kabla ya ndoa kwa gf na bf ni sawa ila usi sex na mtu aliepo kwenye ndoa.

Japo sisi waislam anaezini akiwa katika ndoa hukum yake ni kifo ila anaezini akiwa hajaoa au kuolewa apigwe viboko 80.
Tofauti ya mzinifu alieoa na asie oa ipo.

Laiti tungejua ubaya na madhara ya zinaa,tusingekua tunajianika humu jf kila mtu ajue maovu yetu.
 
Kwa mujibu wa ukristu, kufanya mapenzi kabla Hujafunga ndoa ni kuzini. Pia imekatazwa hata kumtamani mwanamke asiye mke wako.
 
Kama hauamini katika imani yeyote, basi ni halali yako kuona sio dhambi....
Hivo unaweza hata kuiba kisha ukaona sio dhambi kwasababu hukua nacho hivo umeiba umepata
Ubaya wa kufanya uko wap?..nafaham ubaya wa kuiba,kwamba mwenzio ametafta chake wew ukichukue,hapo maelewano kutakua hakuna kat ya pande mbili,..sasa kufanya tendo na dem wangu tena wote tumeridhia kuna ubaya gan?..anyways,..when you come up with religious factors that significantly keep you away frm questioning,ndo majib kama haya yanakuja,sauwa bwana.
 
Inategemeana na imani yako,kwa mfano mkristu au muislam huamini kuwa uasherati ni dhambi na mashahara wa dhambi ni mauti,yaani kifo na adhabu ya milele motoni,ila kama unaimani tofauti na hivyo basi hufanyi kosa,soo ninafsi yako na unavyo amini.
Mi nadhan tafsiri ya kwanza kabsa kabla ya vile vitabu vya zaman kutafsiriwa ilimaanisha kuzini manake ni kama ile niliyoiweka pale mwanzo,ila,hii ishu ya tafsiri na lugha nyiiingi ndo zmeleta mkanganyiko huu,
 
Hio ni definition ya wazungu
Kwao kusex kabla ya ndoa kwa gf na bf ni sawa ila usi sex na mtu aliepo kwenye ndoa.

Japo sisi waislam anaezini akiwa katika ndoa hukum yake ni kifo ila anaezini akiwa hajaoa au kuolewa apigwe viboko 80.
Tofauti ya mzinifu alieoa na asie oa ipo.

Laiti tungejua ubaya na madhara ya zinaa,tusingekua tunajianika humu jf kila mtu ajue maovu yetu.
Hao wazungu ndo walikuja fundisha ukristu huku africa..anyways ,kwa muslims sina uhakika saana na hizo adhabu..mpaka leo sijaona ubaya wa kufanya mapenz na gf wangu,tena wote tukirudhia kwa furaha,anyways
 
Tatizo una judge vtu kwa mtazamo wako.
Wakati dini imekuja kumpa mwanadam mfumo kamili wa maisha.
Ingekua maisha ni kuamua,basi watu wangelala na mama zao,Dada zao n.k
 
Kwa mujibu wa ukristu, kufanya mapenzi kabla Hujafunga ndoa ni kuzini. Pia imekatazwa hata kumtamani mwanamke asiye mke wako.
Ukiangalia hiz dhambi nyingne ni kwel ziko logical,..kwa mfano hyo ya kutaman mal/mke wa mwenzio,au kuiba etc,i see the impact,kwamba kuna madhara dhahir kabsa hutokea baada ya kufanya hizo dhambi,..ila kwa gf na bf ambao wameridhiana ,kiukwel kwa tafsir ya kuzini sion kama ni kosa lolote.
 
Hao wazungu ndo walikuja fundisha ukristu huku africa..anyways ,kwa muslims sina uhakika saana na hizo adhabu..mpaka leo sijaona ubaya wa kufanya mapenz na gf wangu,tena wote tukirudhia kwa furaha,anyways
Tatizo una judge vtu kwa mtazamo wako.
Wakati dini imekuja kumpa mwanadam mfumo kamili wa maisha.
Ingekua maisha ni kuamua,basi watu wangelala na mama zao,Dada zao n.k
 
Ungefurahi mtu akazini na dadako ama mamako (iwapo ni mjane)? Kwa sababu tu wamekubaliana kufanya hilo tendo. Huo ni uchafu. Na kutakuwa hakuna tofauti kati ya binadamu na mnyama.
 
Tatizo una judge vtu kwa mtazamo wako.
Wakati dini imekuja kumpa mwanadam mfumo kamili wa maisha.
Ingekua maisha ni kuamua,basi watu wangelala na mama zao,Dada zao n.k
Hii ndio point sasa.,..kiukwel ku commit adultery mana yake ni sexual relationshp ambayo the least member lazma awe mwana ndoa,.ila tasfiri nyingne za uasherat i think came as bylaws na zmewekwa na binadam kutokana na matokeo yake kuonekana watu ambao hawako kwenye ndoa wakifanya haya matendo kiholela yana madhara,so they put a law and regulation..ili kua na control.kuepusha mambo kama hayo uliyotaja...though ukifanya kwa calculated risk sidhan kama ni dhambi,ni sawa na pombe/ulevi tuu.
 
Hao wazungu ndo walikuja fundisha ukristu huku africa..anyways ,kwa muslims sina uhakika saana na hizo adhabu..mpaka leo sijaona ubaya wa kufanya mapenz na gf wangu,tena wote tukirudhia kwa furaha,anyways

Aiseee! umewahi kuwa na girl friend wangapi? Ukweli unabaki pale pale, kufanya mapenzi/matusi kabla hujaoa/olewa ni dhambi. (Usizini amri ya sita). Madhara yake ni pamoja na magonjwa mengi tu unayoyasikia.
Kuna mwingine atasema toka aanze kuiba hajaona madhara na anafurahia wizi... hii haikusafishi. Kutofuata amri za Mungu ni dhambi.
 
Back
Top Bottom