Nini maana halisi ya kuzini (You shall not commit adultery)

Magonjwa hata ndani ya ndoa yanapatikana

Ndio hapo chacha kijana mdogoooo, hujaoa/hujaolewa unaanza kuumwa magonjwa ya ndoani,,,kisa! kukukimbilia mambo.... kuzini.... kuvunja amri ya sita. wengine hata kwenda kutibiwa huwa shida inabidi ujifiche fiche kwa aibu maana hata wazazi wako watajua umezini....

Acheni uzinzi
 
Kitendo chochote cha kukutanisha vizalio vyenu nje ya NDOA ni dhambi!
Haahahaaa....

Mkuu mimi nisaidie tu maana ya uasherati na ningefurahi ungequote vitabu vitakatifu vinavyozungumzia uasherati na hukumu yake.
 
Nipe tafsiri ya ndoa kwa mujibu was vitabu vya dini

Kwa Mujibu wa Uislam:

Ndoa ni Muunganiko wa hiyari unaohusisha na Jimai wa Watu wa jinsia mbili tofauti ambao wanaruhusiwa kisheria kuoana na wakaoana kwa kufuata Sheria na Taratibu za kiislam!
 
1) Ongezeko la Watoto wa Mitaani

2) Kusambaa kwa Magonjwa ya Zinaaa

3) Kukosekana Mapenzi ya dhati/ uhakika. Ni sawa na kufanya Biashara na Mtu bila ya Mkataba Hata Kama unapata faida lakin Wasiwasi haukosekani
Watoto wanaongezekaje mitaani kwani wazazi wao wanakufa?
Magonjwa ya zinaa yapo hata kwa wanandoa njia za maambukizi ni nyingi
Mapenzi ya dhati labda wewe ndio uliyakosa ila watu wanafurahi na wanapendana kama kawa
 
Kwa Mujibu wa Uislam:

Ndoa ni Muunganiko wa hiyari unaohusisha na Jimai wa Watu wa jinsia mbili tofauti ambao wanaruhusiwa kisheria kuoana na wakaoana kwa kufuata Sheria na Taratibu za kiislam!
Imeandikwa wapi mkuu ebu nipo kwa evidence
 
Soma vitabu vifiatavyo,,,,,, Galatia 5:19
Warumi 13:13
Ezekiel 23:27
Luka 15:13
Matendo ya mitume 15:20
Matwndo ya mitume 15:29......


Ukisoma haya utaelewa sana lakini pia, Lile linaitwa tendo la ndoa, sasa kama ni tendo la ndoa si linafanywa na wenye ndoa? Ninyi ndoa yenu ni ipi?
 
Watoto wanaongezekaje mitaani kwani wazazi wao wanakufa?
Magonjwa ya zinaa yapo hata kwa wanandoa njia za maambukizi ni nyingi
Mapenzi ya dhati labda wewe ndio uliyakosa ila watu wanafurahi na wanapendana kama kawa

Hayo ni Madhara ya Zinaa

Ulichofanya Wewe ni kulinganisha na Maisha ya Ndoa na baadhi ya exception ni vitu viwili Tofauti!

Ni sawa na kuuliza Madhara ya kushiriki Ngono katika Umri Mdogo kwa Msichana nikikujibu ni Pamoja na kupata Mimba zisizo tarajiwa ukaja na hoja Mbona Wewe ulikuwa unashirki katika umri Mdogo na mpaka Leo hujapata Mimba!

Kama unaona Zinaa haina Madhara huo ni mtazamo wako kutokana na uzoefu wako
 
Uasherati ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile,unaitwa pia ufiraji
Ulawiti au ufiraji ni mwanamume kulala mwanamume mwenzake kwa mfano wa mwanamke. Hali kadhalika kwa mwanamume mwanamke kinyume na maumbile. Wote hawa sehemu yao ni moto wa milele.
 
Back
Top Bottom