Nini kinachofanya JK asiteuwe RC mpaka leo??

Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya waliogombea ubunge na kukataliwa na wananchi hawafai tena kushika ofisi za kiutawala tena!! kikwete asifanye kosa hilo kuwarudisha kwa mlango wa nyuma na kuwapa ofisi za umma. Hiyo inawahusu mawaziri walioshindwa kwenye uchaguzi!
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Wapo Dodoma tangia juzi wanapeana semina na kushauriana na kila aliyefanikiwa kuchakachua kura na kumpa kura nyingi mkuu atapewa mkoa mzuri kama majiji.Wakurugenzi wa wilaya nao wanabadilishwa muda si mrefu ili kulipana fadhila kwa wale waliochakachua vizuri kura 2010.Arusha,Shy mjini,Hai,nyamagana n.k lazima wabadilishwe.
 
Kinachonisikitisha ni kwamba rais wetu mwenyewe aliahidi kuwa kabla ya mwaka 2011 haujatimia angeshafanya uteuzi huo. Hii inadhiirisha ni mwongo au sijui ni mtu ambaye sio mtimiza ahadi(unreliable president). Mbaya zaidi hata kama aliahirisha kutea baraza basi angewataarifu wananchi why? Huo ndio uwajibikaji!
 
kwani waliopo nani aliteua?
au ni lazima kila anapo chaguliwa raisi ateue ma-RC wengine?

Kwa kuchelewa anavunja sheria gani?
 
hai ded alifukuzwa kwenye kampeni kwa ajili ya mbowe, hata ivo aaliyeletwa hakuhimili kumtangaza kimbita wa ccm ! moto mkali pale, hata apelekwe nani hakuna ujanja
 
Tusitake kukuza mambo hapa! Kwanza sheria haisemi kwamba kila baada ya uchaguzi wateuliwe wengine na wala sheria haisemi ukomo wa muda wa kuteua wakuu hao. Hakuna shughuli zinazolala kwa sababu Makatibu Tawala ambao ndiyo watekelezaji wakubwa wa maamuzi na masuala yote ya utawala wapo na wanachapa mzigo kama kawaida. Isije kuwa kuna watu wana maslahi na uteuzi huo ndiyo maana wanatia shinikizo hapa JF!
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Katiba haitamki kuwa mara baada ya uchaguzi Rais anatakiwa kuteua wakuu wa mikoa. Ameshateua baraza la mawaziri na mwanasheria mkuu basi. Wakuu wa mikoa na wa wilaya anaweza akaenda nao hawa hawa alionao mpaka pale atakapoona kuna haja ya kufanya mabadiliko. Someni katiba. Mnataka katiba mpya wakati hii iliyopo hamuijui.
 
Jk huwa ananifurahishaga hapo tu.yani ni mwoga hadi wa kivuli chake mwenyewe.kunywa baba si umelikoroga mwenyewe?
 
Jk huwa ananifurahishaga hapo tu.yani ni mwoga hadi wa kivuli chake mwenyewe.kunywa baba si umelikoroga mwenyewe?
Nimeipenda hii ikibdi balaza lake la mawazili,makamba RA Wamsaidie kulinywa shuwain
a
 
Jamaa mbishi istoshe ubishi wala haumsaidii.Is just easy ;anaitisha balaza anawaelekeza jamaa kuacha mchezo mchafu kwasababu wadau wamestikia tale.Anavyorasimisha ndiyo anavyoharibu mambo.Akina nani...kwanini hawamwambii,....lakini inawezeka wanamshauri vizuri ila yeye ndiyo kichwa cha mbuzi mkia kuungua.Na anaungua hasa,nani wa kumweleza wakati yeye ndiyo wa mwisho kuingia kwenye mkutano.
 
JENERALI ULIMWENGU: Wakuu wa Mikoa na Wilaya wachaguliwe na Wananchi, wasiteuliwe na Rais
 
JK kwa sasa hana amani, anajua kile kiti alichokikalia alikichakachua. Mwangalieni vizuri anapoongea siku hizi hana furaha wala kujiamini kama zamani. Sasa anajua wale wasiomuunga mkono wanasubiri awateme kwenye U-RC na U-DC watokomee zao kwenye vyama vingine. Anashindwa aamue nini, amegundua kuwa wananchi hawamtaki maana kura hakupata.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom