Kwa nini unajipa ujuzi usio nao?
Unajua vikao vyote vya kuunda ACT na kuweka mikakati ya kujiimarisha kwake vilifanyika lini, wapi, na nani alikuwapo?
Ila bro umenifanya nicheke kinoma. Ok umeshinda boss wangu🙏Lazima ucheke.
Wewe ndiye uache ligi za kujivika omniscience.
Ninatofautiana. Fatma ni KOL katika jamii , usimlinganishe na Bambo, Nick wa Pili au Steve Nyerere.Swali ni, kwa nini mna expectations zote hizi kwa Fatma Karume, mtu ambaye si mfanyakazi wa serikali wala mpigiwa kura na watu, kwa nini mnamfanya kama some pillar of society?
Hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.Tarehe iliyosajiliwa ACT ni 5 Mei 2014, takriban miaka 10 iliyopita, na kililazimika kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka uliofuata, yaani 2015. Fatma anadai kuwa aliwashauri ACT washiriki uchaguzi huo miaka 10 iliyopita, lakini hakuna mahali popote kumbukumbu hiyo imewekwa rasmi (japo iwe ni kweli au la, hakuna uthibitisho wowote zaidi ya kauli yake binafsi, hivyo inabaki kuwa hoja ya upande mmoja, yaani subjective).Sasa hoja yako ni ipi hasa? Unataka kusema kuwa Fatma alikuwa akisubiri kwa muda wote huo ili awashauri ACT washiriki uchaguzi, kwenye mikutano yao waliyoamua kususia? (ambapo hata hivyo hakuna ushahidi unaoonesha kuwa hayo mazungumzo yalifanyika). Je, aliwashauri kushiriki uchaguzi mara baada ya chama kuanzishwa? It doesn't make sense, umeingia mjini kirahisi hapa!
Bit she is till a private citizen.Ninatofautiana. Fatma ni KOL katika jamii , usimlinganishe na Bambo, Nick wa Pili au Steve Nyerere.
Fatma ametokea katika majukwaa ya Kitaifa na Kimataifa akizungumzia masuala ya nchi yetu.
Ametumia utaalam wake wa sheria ku shape or sway public opinion.
Ni kwa mantiki hiyo, watu hawamwangalii kama Pillar of society, wanahoji integrity and credibility yake aliyoijenga mwenyewe kupitia forum tofauti.
Hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.
Na hivyo, leo kusema Fatma amebadilika kwa sababu anakataa hoja ya kutoshiriki/kuzuia uchaguzi si kitu chenye ukweli, kwa sababu Fatma anasema hajawahi kuwa na falsafa hizo.
Hakuna mahali alipolazimishwa kuwa mwanaharakati kama tunavyotarajia sisi, lakini misingi ya haki ni ile ile kwa wote. Ndiyo, uamuzi wa CHADEMA kususia chaguzi ni mojawapo ya mikakati ya kupigania haki zile zile ambazo wananchi wamekuwa wakinyimwa katika chaguzi.Kwa upande wake, yeye amesisitiza kushiriki katika chaguzi hizo hizo ambazo mara kadhaa zimekiuka haki za Watanzania. Hizi ndizo chaguzi zilizomwingiza madarakani Magufuli, ambaye baadaye alimpinga kwa nguvu kubwa. Hii inaleta maswali ,Je, mwanaharakati anayelipwa? Maana huwezi kuendelea kupigania haki huku ukipuuzia chanzo kikuu cha ukosefu wa haki hizo.Bit she is till a private citizen.
Ana haki ya ku disengage from activism.
Kwa nini watu wanalazimisha awe activist, tena sio tu awe activist, bali awe activist vile wanavyotaka wao, hata pale anaposema kwamba falsafa zake hazikubaliani na hizo activism kama za kukataa kushiriki uchaguzi?
Hakuna ofisi ya kiserikali wala ya kuchaguliwa na wananchi inayoitwa public figure. Hata Diamond Platnumz ni public figure.Hoja ya kutoshiriki uchaguzi ilianza lini hasa, ilhali waliokuwa waanzilishi wa harakati hizi hapo awali walishiriki uchaguzi? Sawa, huenda falsafa yake binafsi ni kushiriki uchaguzi daima. Lakini swali la unaisimamiajaje falsafa ya kushiriki katika mchakato uliojaa wizi wa kura, mauaji, na utapeli wa kisiasa? Ni kweli, huo unaweza kuwa msimamo wa maisha yake binafsi, na hatuna sababu ya kuingilia maisha yake ya faragha. Hata hivyo, kwa kuwa ni public figure na aliwahi kushika nafasi ya juu kama Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kuna umati mkubwa wa watu wanaomtazama kama role model wa uongozi na uadilifu. Kwa msingi huo, tuna kila haki ya kumkosoa anapokwenda kinyume na misingi ya haki.
Halazimishwi kubadilisha msimamo wake, lakini asitumie kichaka cha 'falsafa' kama kisingizio cha kushirikiana na wahuni wa mchakato wa uchaguzi. Kauli ya 'No Reforms, No Election' si falsafa ni movement/hamasa ya kisiasa yenye lengo la kuwazuia watawala kuendelea kunyima wananchi haki yao kupitia chaguzi zisizo huru na haki. Unapotaja 'falsafa', ni falsafa gani hasa unayozungumzia?Kwa nini mnalazimisha kila mtu akubali No Reforms, No Election hata kama kifalsafa hakubaliani na hoja hiyo?
Kimsingi Tanganyika tumetekwa,Kuna haja gani ya kuungana huku unaliwa kibogaLakini mbona inaonekana kama yeye mwenyewe ndiye anayetoa taswira ya udini kwa namna alivyojenga hoja zake dhidi ya shutuma alizozitoa Gwajima? Badala ya kujibu kwa msingi wa hoja au ushahidi wa kimantiki, hoja zake zinaonekana kujengwa juu ya misimamo inayogusa hisia za kidini.
Huo ni mtazamo wako wa kifalsafa.Halazimishwi kubadilisha msimamo wake, lakini asitumie kichaka cha 'falsafa' kama kisingizio cha kushirikiana na wahuni wa mchakato wa uchaguzi. Kauli ya 'No Reforms, No Election' si falsafa ni movement/hamasa ya kisiasa yenye lengo la kuwazuia watawala kuendelea kunyima wananchi haki yao kupitia chaguzi zisizo huru na haki. Unapotaja 'falsafa', ni falsafa gani hasa unayozungumzia?
Mwanamke hafai kuwa nguzoUsiwaamini wanawake....! Usikute amesha mpata Mwanaume m CCM na anampenda, lazima abadili msimamo hasa katika umri wake Mwanaume ni pipi tamu sana.
Naomba nichukulie hizo 'falsafa' zako kama mifano ya kujifunza tu, kwa sababu hazina uhalisia katika mazingira ya Tanzania. Hazifanyi kazi hapa, na hakuna dalili kuwa zitawahi kufanya kazi kwa misingi ya namna hiyo. Hiyo mifano unayotoa inabaki kuwa matukio ya kipekee (outliers) au bahati nasibu (coincidence) isiyoakisi hali halisi ya kisiasa nchini.Huo ni mtazamo wako wa kifalsafa.
Kuna mitazamo mingi tofauti kifalsafa.
Kwa mfano.
Kuna watu mtazamo wao ni kushiriki uchaguzi kwa wingi sana mpaka wezi wa kura washindwe kuiba. Wanasema wizi wa kura unakuwa rahisi kwenye chaguzi zenye margin ndogo. Watu wengi wakijitokeza kupiga kura na kulinda kura zao, kama asilimia kubwa sana imekataa CCM, CCM watashindwa kuiba kura. Hivi ndivyo Wenje alivyomshinda Lau Masha Nyamagana despite CCM kujaribu kuiba kura.
Sasa kwa nini unataka kumlazimisha mtu mwenye mtazamo tofauti na wako afanye unavyotaka wewe?
Hiyo ndiyo demokrasia?
Mkuu,Naomba nichukulie hizo 'falsafa' zako kama mifano ya kujifunza tu, kwa sababu hazina uhalisia katika mazingira ya Tanzania. Hazifanyi kazi hapa, na hakuna dalili kuwa zitawahi kufanya kazi kwa misingi ya namna hiyo. Hiyo mifano unayotoa inabaki kuwa matukio ya kipekee (outliers) au bahati nasibu (coincidence) isiyoakisi hali halisi ya kisiasa nchini.
Nina uhakika unaelewa vizuri kilichotokea kwenye chaguzi za 2015 na 2020 jinsi mchakato ulivyokumbwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kidemokrasia.
Kushikilia falsafa hizo kwa namna isiyoangalia muktadha, kama anavyofanya Fatma, ndicho kinachomfanya aonekane kama tapeli wa kisiasa mtu anayejificha kwenye misingi ya falsafa isiyotekelezeka huku akipuuza uhalisia wa mateso ya wananchi.
Pia Watanzania wengine wana tabia fulani ya projection.
Projection ni nini? Ni tabia fulani ya kumuwekea mtu baki matarajio yako.
Yani mtu hujakaa naye, hujamuuliza anataka nini, lakini unakuwa unalazimisha tu kuwa huyu lazima atakuwa anafikiri kama mimi.
Siku akipata nafasi ya kufunguka na kukueleza kwamba yeye hafikirii kama wewe, unaumia, unamtukana, unamsema huyu msaliti.
Msaliti kivipi? Kwani mlikubaliana mfikirie sawa?
Nimeliona hili sana Peter Madeleka alivyoondoka CHADEMA na kwenda ACT. Kuna watu wamemsema kama vile walikubaliana naye afe mwanachama wa CHADEMA.
Fatma Karume kasema yeye msimamo wake siku zote ni kushiriki kwenye uchaguzi. Aliishauri ACT takriban miaka 10 iliyopita kushiriki kwenye uchaguzi. Hiyo ilikuwa kabla ya No Reforms No Election. Na hata leo anaendelea na msimamo wake huo huo.
Sasa kuna watu wasiomjua wanasema siku hizi kabadilika, wakati yeye anasema huu ndio msimamo wake na kashautoa takriban miaka 10 iliyopita huko.
Watu wengine wanapenda sana kulazimisha kila mtu afikirie kama wao.
Oh bwayHoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.
Na hivyo, leo kusema Fatma amebadilika kwa sababu anakataa hoja ya kutoshiriki/kuzuia uchaguzi si kitu chenye ukweli, kwa sababu Fatma anasema hajawahi kuwa na falsafa hizo.
Mkuu,Mkuu,
Fatma ana haki ya kuishi maisha anayoyataka yeye. Hiyo ni haki ya kibinadamu. Ipo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.
Wewe kama mwanaharakati wa kusimamia haki inakupasa uielewe hii haki.
Kwa nini unamlazimisha asiishi maisha anayoyataka yeye, aishi maisha unayotaka wewe aishi?
Hapana mkuu.