GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa nini unajipa ujuzi usio nao?

Unajua vikao vyote vya kuunda ACT na kuweka mikakati ya kujiimarisha kwake vilifanyika lini, wapi, na nani alikuwapo?

Tarehe iliyosajiliwa ACT ni 5 Mei 2014, takriban miaka 10 iliyopita, na kililazimika kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka uliofuata, yaani 2015. Fatma anadai kuwa aliwashauri ACT washiriki uchaguzi huo miaka 10 iliyopita, lakini hakuna mahali popote kumbukumbu hiyo imewekwa rasmi (japo iwe ni kweli au la, hakuna uthibitisho wowote zaidi ya kauli yake binafsi, hivyo inabaki kuwa hoja ya upande mmoja, yaani subjective).Sasa hoja yako ni ipi hasa? Unataka kusema kuwa Fatma alikuwa akisubiri kwa muda wote huo ili awashauri ACT washiriki uchaguzi, kwenye mikutano yao waliyoamua kususia? (ambapo hata hivyo hakuna ushahidi unaoonesha kuwa hayo mazungumzo yalifanyika). Je, aliwashauri kushiriki uchaguzi mara baada ya chama kuanzishwa? It doesn't make sense, umeingia mjini kirahisi hapa!
 
Swali ni, kwa nini mna expectations zote hizi kwa Fatma Karume, mtu ambaye si mfanyakazi wa serikali wala mpigiwa kura na watu, kwa nini mnamfanya kama some pillar of society?
Ninatofautiana. Fatma ni KOL katika jamii , usimlinganishe na Bambo, Nick wa Pili au Steve Nyerere.

Fatma ametokea katika majukwaa ya Kitaifa na Kimataifa akizungumzia masuala ya nchi yetu.
Ametumia utaalam wake wa sheria ku shape or sway public opinion.

Ni kwa mantiki hiyo, watu hawamwangalii kama Pillar of society, wanahoji integrity and credibility yake aliyoijenga mwenyewe kupitia forum tofauti.
 
Tarehe iliyosajiliwa ACT ni 5 Mei 2014, takriban miaka 10 iliyopita, na kililazimika kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka uliofuata, yaani 2015. Fatma anadai kuwa aliwashauri ACT washiriki uchaguzi huo miaka 10 iliyopita, lakini hakuna mahali popote kumbukumbu hiyo imewekwa rasmi (japo iwe ni kweli au la, hakuna uthibitisho wowote zaidi ya kauli yake binafsi, hivyo inabaki kuwa hoja ya upande mmoja, yaani subjective).Sasa hoja yako ni ipi hasa? Unataka kusema kuwa Fatma alikuwa akisubiri kwa muda wote huo ili awashauri ACT washiriki uchaguzi, kwenye mikutano yao waliyoamua kususia? (ambapo hata hivyo hakuna ushahidi unaoonesha kuwa hayo mazungumzo yalifanyika). Je, aliwashauri kushiriki uchaguzi mara baada ya chama kuanzishwa? It doesn't make sense, umeingia mjini kirahisi hapa!
Hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.

Na hivyo, leo kusema Fatma amebadilika kwa sababu anakataa hoja ya kutoshiriki/kuzuia uchaguzi si kitu chenye ukweli, kwa sababu Fatma anasema hajawahi kuwa na falsafa hizo.
 
Ninatofautiana. Fatma ni KOL katika jamii , usimlinganishe na Bambo, Nick wa Pili au Steve Nyerere.

Fatma ametokea katika majukwaa ya Kitaifa na Kimataifa akizungumzia masuala ya nchi yetu.
Ametumia utaalam wake wa sheria ku shape or sway public opinion.

Ni kwa mantiki hiyo, watu hawamwangalii kama Pillar of society, wanahoji integrity and credibility yake aliyoijenga mwenyewe kupitia forum tofauti.
Bit she is till a private citizen.

Ana haki ya ku disengage from activism.

Kwa nini watu wanalazimisha awe activist, tena sio tu awe activist, bali awe activist vile wanavyotaka wao, hata pale anaposema kwamba falsafa zake hazikubaliani na hizo activism kama za kukataa kushiriki uchaguzi?
 
Hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.

Na hivyo, leo kusema Fatma amebadilika kwa sababu anakataa hoja ya kutoshiriki/kuzuia uchaguzi si kitu chenye ukweli, kwa sababu Fatma anasema hajawahi kuwa na falsafa hizo.

Hoja ya kutoshiriki uchaguzi ilianza lini hasa, ilhali waliokuwa waanzilishi wa harakati hizi hapo awali walishiriki uchaguzi? Sawa, huenda falsafa yake binafsi ni kushiriki uchaguzi daima. Lakini swali la unaisimamiajaje falsafa ya kushiriki katika mchakato uliojaa wizi wa kura, mauaji, na utapeli wa kisiasa? Ni kweli, huo unaweza kuwa msimamo wa maisha yake binafsi, na hatuna sababu ya kuingilia maisha yake ya faragha. Hata hivyo, kwa kuwa ni public figure na aliwahi kushika nafasi ya juu kama Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kuna umati mkubwa wa watu wanaomtazama kama role model wa uongozi na uadilifu. Kwa msingi huo, tuna kila haki ya kumkosoa anapokwenda kinyume na misingi ya haki.
 
Hakuna mahali alipolazimishwa kuwa mwanaharakati kama tunavyotarajia sisi, lakini misingi ya haki ni ile ile kwa wote. Ndiyo, uamuzi wa CHADEMA kususia chaguzi ni mojawapo ya mikakati ya kupigania haki zile zile ambazo wananchi wamekuwa wakinyimwa katika chaguzi.Kwa upande wake, yeye amesisitiza kushiriki katika chaguzi hizo hizo ambazo mara kadhaa zimekiuka haki za Watanzania. Hizi ndizo chaguzi zilizomwingiza madarakani Magufuli, ambaye baadaye alimpinga kwa nguvu kubwa. Hii inaleta maswali ,Je, mwanaharakati anayelipwa? Maana huwezi kuendelea kupigania haki huku ukipuuzia chanzo kikuu cha ukosefu wa haki hizo.
 
Hoja ya kutoshiriki uchaguzi ilianza lini hasa, ilhali waliokuwa waanzilishi wa harakati hizi hapo awali walishiriki uchaguzi? Sawa, huenda falsafa yake binafsi ni kushiriki uchaguzi daima. Lakini swali la unaisimamiajaje falsafa ya kushiriki katika mchakato uliojaa wizi wa kura, mauaji, na utapeli wa kisiasa? Ni kweli, huo unaweza kuwa msimamo wa maisha yake binafsi, na hatuna sababu ya kuingilia maisha yake ya faragha. Hata hivyo, kwa kuwa ni public figure na aliwahi kushika nafasi ya juu kama Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kuna umati mkubwa wa watu wanaomtazama kama role model wa uongozi na uadilifu. Kwa msingi huo, tuna kila haki ya kumkosoa anapokwenda kinyume na misingi ya haki.
Hakuna ofisi ya kiserikali wala ya kuchaguliwa na wananchi inayoitwa public figure. Hata Diamond Platnumz ni public figure.

Na kwenye urais wa TLS, Fatma alishaondoka.

Kwa nini mnataka kumfanya awe hostage afanye siasa za activism, tena kwa mtazamo wenu tu, bila kuheshimu kwamba watu tofauti wana falsafa tofauti, na wanatakiwa kuwa na uhuru wa kufanya siasa wanavyotaka, au kuamua kutofanya siasa kabisa, na hiyo ndiyo maana ya demokrasia?

Kama nyie mlivyo na uhuru wa kufanya kampeni za No Reforms, No Election?

Hamuelewi wapi hapo?

Kwa nini mnalazimisha kila mtu akubali No Reforms, No Election hata kama kifalsafa hakubaliani na hoja hiyo?
 
Ukweli ni kwamba wazanzibar na waislam wote wameungana na samia. Angalia matamko ya mashehe na ya wazanzibari. Viongozi wa waislam wanachanganya dini na siasa na kutoa kauli za kichochezi lakini hakuna anaewachukulia hatua.

Maneno yale yangetamkwa na kiongozi wa kanisa angeambiwa anachanganya dini na siasa.
 
Kwa nini mnalazimisha kila mtu akubali No Reforms, No Election hata kama kifalsafa hakubaliani na hoja hiyo?
Halazimishwi kubadilisha msimamo wake, lakini asitumie kichaka cha 'falsafa' kama kisingizio cha kushirikiana na wahuni wa mchakato wa uchaguzi. Kauli ya 'No Reforms, No Election' si falsafa ni movement/hamasa ya kisiasa yenye lengo la kuwazuia watawala kuendelea kunyima wananchi haki yao kupitia chaguzi zisizo huru na haki. Unapotaja 'falsafa', ni falsafa gani hasa unayozungumzia?
 
Lakini mbona inaonekana kama yeye mwenyewe ndiye anayetoa taswira ya udini kwa namna alivyojenga hoja zake dhidi ya shutuma alizozitoa Gwajima? Badala ya kujibu kwa msingi wa hoja au ushahidi wa kimantiki, hoja zake zinaonekana kujengwa juu ya misimamo inayogusa hisia za kidini.
Kimsingi Tanganyika tumetekwa,Kuna haja gani ya kuungana huku unaliwa kiboga
 
Halazimishwi kubadilisha msimamo wake, lakini asitumie kichaka cha 'falsafa' kama kisingizio cha kushirikiana na wahuni wa mchakato wa uchaguzi. Kauli ya 'No Reforms, No Election' si falsafa ni movement/hamasa ya kisiasa yenye lengo la kuwazuia watawala kuendelea kunyima wananchi haki yao kupitia chaguzi zisizo huru na haki. Unapotaja 'falsafa', ni falsafa gani hasa unayozungumzia?
Huo ni mtazamo wako wa kifalsafa.

Kuna mitazamo mingi tofauti kifalsafa.

Kwa mfano.

Kuna watu mtazamo wao ni kushiriki uchaguzi kwa wingi sana mpaka wezi wa kura washindwe kuiba. Wanasema wizi wa kura unakuwa rahisi kwenye chaguzi zenye margin ndogo. Watu wengi wakijitokeza kupiga kura na kulinda kura zao, kama asilimia kubwa sana imekataa CCM, CCM watashindwa kuiba kura. Hivi ndivyo Wenje alivyomshinda Lau Masha Nyamagana despite CCM kujaribu kuiba kura.

Sasa kwa nini unataka kumlazimisha mtu mwenye mtazamo tofauti na wako afanye unavyotaka wewe?

Hiyo ndiyo demokrasia?
 
Usiwaamini wanawake....! Usikute amesha mpata Mwanaume m CCM na anampenda, lazima abadili msimamo hasa katika umri wake Mwanaume ni pipi tamu sana.
Mwanamke hafai kuwa nguzo
 
Huo ni mtazamo wako wa kifalsafa.

Kuna mitazamo mingi tofauti kifalsafa.

Kwa mfano.

Kuna watu mtazamo wao ni kushiriki uchaguzi kwa wingi sana mpaka wezi wa kura washindwe kuiba. Wanasema wizi wa kura unakuwa rahisi kwenye chaguzi zenye margin ndogo. Watu wengi wakijitokeza kupiga kura na kulinda kura zao, kama asilimia kubwa sana imekataa CCM, CCM watashindwa kuiba kura. Hivi ndivyo Wenje alivyomshinda Lau Masha Nyamagana despite CCM kujaribu kuiba kura.

Sasa kwa nini unataka kumlazimisha mtu mwenye mtazamo tofauti na wako afanye unavyotaka wewe?

Hiyo ndiyo demokrasia?
Naomba nichukulie hizo 'falsafa' zako kama mifano ya kujifunza tu, kwa sababu hazina uhalisia katika mazingira ya Tanzania. Hazifanyi kazi hapa, na hakuna dalili kuwa zitawahi kufanya kazi kwa misingi ya namna hiyo. Hiyo mifano unayotoa inabaki kuwa matukio ya kipekee (outliers) au bahati nasibu (coincidence) isiyoakisi hali halisi ya kisiasa nchini.

Nina uhakika unaelewa vizuri kilichotokea kwenye chaguzi za 2015 na 2020 jinsi mchakato ulivyokumbwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kidemokrasia.

Kushikilia falsafa hizo kwa namna isiyoangalia muktadha, kama anavyofanya Fatma, ndicho kinachomfanya aonekane kama tapeli wa kisiasa mtu anayejificha kwenye misingi ya falsafa isiyotekelezeka huku akipuuza uhalisia wa mateso ya wananchi.
 
Mkuu,

Fatma ana haki ya kuishi maisha anayoyataka yeye. Hiyo ni haki ya kibinadamu. Ipo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Wewe kama mwanaharakati wa kusimamia haki inakupasa uielewe hii haki.

Kwa nini unamlazimisha asiishi maisha anayoyataka yeye, aishi maisha unayotaka wewe aishi?
 
My brother Pundit,save ur breath..
Pia Watanzania wengine wana tabia fulani ya projection.

Projection ni nini? Ni tabia fulani ya kumuwekea mtu baki matarajio yako.

Yani mtu hujakaa naye, hujamuuliza anataka nini, lakini unakuwa unalazimisha tu kuwa huyu lazima atakuwa anafikiri kama mimi.

Siku akipata nafasi ya kufunguka na kukueleza kwamba yeye hafikirii kama wewe, unaumia, unamtukana, unamsema huyu msaliti.

Msaliti kivipi? Kwani mlikubaliana mfikirie sawa?

Nimeliona hili sana Peter Madeleka alivyoondoka CHADEMA na kwenda ACT. Kuna watu wamemsema kama vile walikubaliana naye afe mwanachama wa CHADEMA.

Fatma Karume kasema yeye msimamo wake siku zote ni kushiriki kwenye uchaguzi. Aliishauri ACT takriban miaka 10 iliyopita kushiriki kwenye uchaguzi. Hiyo ilikuwa kabla ya No Reforms No Election. Na hata leo anaendelea na msimamo wake huo huo.

Sasa kuna watu wasiomjua wanasema siku hizi kabadilika, wakati yeye anasema huu ndio msimamo wake na kashautoa takriban miaka 10 iliyopita huko.

Watu wengine wanapenda sana kulazimisha kila mtu afikirie kama wao.
20250707_205353.jpg
 
Hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Fatma, hakuna sehemu ambapo Fatma aliwahi kuwa sehemu ya wanaharakati waliofikiri kutoshiriki uchaguzi ni wazo zuri.

Na hivyo, leo kusema Fatma amebadilika kwa sababu anakataa hoja ya kutoshiriki/kuzuia uchaguzi si kitu chenye ukweli, kwa sababu Fatma anasema hajawahi kuwa na falsafa hizo.
Oh bway
 
Mkuu,

Fatma ana haki ya kuishi maisha anayoyataka yeye. Hiyo ni haki ya kibinadamu. Ipo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Wewe kama mwanaharakati wa kusimamia haki inakupasa uielewe hii haki.

Kwa nini unamlazimisha asiishi maisha anayoyataka yeye, aishi maisha unayotaka wewe aishi?
Mkuu,

Ni wapi hasa amelazimishwa? Naona unakaza fuvu tu kutetea.

Huyo unayesema anaishi maisha yake binafsi anatumia majukwaa ya wazi yanayofuatiliwa na umma. Hawezi kutumia majukwaa hayo kuwatetea wazi wahuni wa kisiasa halafu watu wakae kimya, eti kwa sababu sasa anaishi binafsi.

Anapojitokeza hadharani na kutoa kauli zenye athari kwa wjamii, lazima atambue kuwa atawajibika kwa maoni yake mbele ya umma si kwa kivuli cha maisha binafsi.
 
My brother Pundit,save ur breath..

View attachment 3397626
Hapana mkuu.

You guys need to save your breaths on trivial matters of looking at personalities emotionally and focus on important issues.

Who is Fatma Karume anyway?

Kwa nini Fatma Karume anaangaliwa kama savior Messiah fulani hivi?

Akikwambia ameona mbinu hii haifai tena utasemaje? Utamlazimisha aifuate mbinu ambayo anaona haifai?
 
Back
Top Bottom