GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ila tabia ya mtu kutoa maoni tofauti alafu wale tuliokuwa tunamwamini ndo tukawa wa kwanza kumdhihaki inaonesha ni namna gani hatuna subira.
Ukihisi mtu amekwenda tofauti na ulivyomzoea, mpe muda kwanza, sio kumshutumu haraka vile.

Lakini pia, sisi tunaotick October, tushajua udhaifu wenu😀. Nyie jamaa kwa kunata na biti hamjambo, sasa na sisi tunawapa vitu kila baada ya siku mbili mpaka mnatoka kwenye agenda yenu bila kujijua, jifunzeni kubaki kwenye mstari, mengine yawapite kama hamjayaskia, sisi huku tuna watu wa propaganda, tukiona mmetulia, tunawawekea inshu, paaaaa😀, wote mnajaa then sisi tunapitisha chap jambo flani. Ester tulimtuma ila mlituweza vile hamkushadadia kiviiiile😀😀😀.
Jifunzeni kubaki kwenye mambo yenu, mnakuwa na vitu vya msingi sana ila hamtulii😀.
Na sisi hatuchoki, sasa ivi bado mnanata na biti ya arise and shine, povu linawatoka kila upande, ikikalibia kesi ya bosi wenu tunatupia jambo jingine then huku hakimu anahairisha kesi mpaka october😀😀😀.

Jifunzeni kutulia kwenye inshu zenu, kila saa kufatafata mambo yetu tu... ndio maana hamuendelei. Tumewasimamisha mikutano ya kisiasa, badala ya kuendelea na kampeni yenu kwenye mitandao nyie mnakomaa leo mama kaenda komoro, mara majaliwa kaachia ngazi, inawahusu nini kwani, ndio agenda yenu?
Hamna akili hiyo, usitake kujifanya kwamba ni mambo mnapanga. Hata hivyo maamuzi ya mahakama hayaangalii michango ya mitandaoni, kama mahakama imefikia hapo basi ujue hakuna mahakama bali ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Kwani huyo mama kwenda Comoro ni ili apoteze watu kwenye mijadala? Na ameenda kama mwanaccm au rais wa nchi?
 
Hivi karibuni, Fatma Karume ameonekana kubadili mwelekeo wa mijadala yake ya kisiasa kwa namna ambayo imeibua maswali miongoni mwa watanzania, hasa wale wanaoamini katika harakati za mageuzi ya kweli.

Mwanzo, alivamia vikali kauli za Askofu Gwajima aliyekuwa anapinga matukio ya utekaji na ukiukwaji wa haki unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola, akimtuhumu kuwa anatafuta "attention" ya kisiasa, licha ya kwamba hoja za Gwajima zilikuwa na uzito wa kulinda utu na uhuru wa raia.

Sasa, ameibukia tena kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akizibeza juhudi za CHADEMA na sera yao ya "No Reforms, No Elections", akikariri kuwa kusitisha uchaguzi ni kosa la jinai. Kauli hii imechukuliwa na wengi kama kejeli isiyoakisi hali halisi ya mazingira ya kisiasa nchini, ambapo haki za msingi, uhuru wa kisiasa na uhuru wa kutoa maoni vinaendelea kukandamizwa.

Cha kushangaza zaidi, kauli hizi za Fatma Karume zinatolewa wakati ambapo Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani na mwanasheria mwenzake, yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambayo kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa. Hali hii imezidi kuzua maswali: je, Fatma Karume bado yupo upande wa watetezi wa haki, au amebadili msimamo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika wazi?

Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Hayati John Magufuli, Fatma Karume alijitokeza kuwa mmoja wa sauti thabiti zilizokuwa zikikemea dhuluma, ukandamizaji, na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika utawala wa sasa, ambao nao umeonesha mwelekeo wa kukiuka misingi ya demokrasia, sauti yake imekuwa ya mashaka, wakati mwingine ikisikika kama ya kukubaliabiana na mfumo badala ya kuukosoa.
Je, ni mabadiliko ya kiitikadi? Ni mkakati wa kisiasa? Au kuna mambo ya ndani zaidi ambayo bado hayajawekwa wazi kwa umma? Kwa vyovyote vile, hatua na kauli za Fatma Karume zinahitaji tafakari, hasa kwa wale wanaoamini katika dhana ya "principled activism" yaani, kupigania haki bila kujali nani yuko madarakani.
Screenshot_20250613-122647~2.png
 
Unahakikishaje kuwa Fatma hakuishauri ACT isisusie chaguzi na mambo ya uongozi wa jamii kama alivyosema?
ACT miaka 10 iliyopita ndio ilikuwa imeanzishwa, haikuwa na watu wa kuifanya wasusie chochote, usitake kulazimisha. Ulitakiwa useme aliwashauri CUF na sio ACT boss wangu.
 
Haya ni matokeo ya Mgogoro wa ndoa yake nadhani amekuwq promised
 
ACT miaka 10 iliyopita ndio ilikuwa imeanzishwa, haikuwa na watu wa kuifanya wasusie chochote, usitake kulazimisha. Ulitakiwa useme aliwashauri CUF na sio ACT boss wangu.
Sasa yeye mwenyewe kasema ACT, si CUF.

Unatakaje niseme CUF na si ACT?

Unanifundishaje natakiwa jusema hiki na si kile?

Wewe ni nani ujue ninachotaka na ninachotakiwa kusema ni kipi?
 
Sasa yeye mwenyewe kasema ACT, si CUF.

Unatakaje niseme CUF na si ACT?

Unanifundishaje natakiwa jusema hiki na si kile?

Wewe ni nani ujue ninachotaka na ninachotakiwa kusema ni kipi?
Nilikwambia umeingizwa mjini kirahisi. 10yrs back ACT was nothing. Labda kama unataka kuleta ubishi wa mshipa.
 
Nilikwambia umeingizwa mjini kirahisi. 10yrs back ACT was nothing. Labda kama unataka kuleta ubishi wa mshipa.
ACT haikuanza kutoka sifuri ilianza kwa watu walewale waliojuana na kufuatiliana siku nyingi kina Jussa na wenzake kumeguka CUF.

Mbona unafanya trolling sasa?
 
ACT haikuanza kutoka sifuri ilianza kwa watu walewale waliojuana na kufuatiliana siku nyingi kina Jussa na wenzake kumeguka CUF.

Mbona unafanya trolling sasa?
Ni kweli, ila haikuwa miaka 10 iliyopita.
 
Ni kweli, ila haikuwa miaka 10 iliyopita.
Kwa nini unajipa ujuzi usio nao?

Unajua vikao vyote vya kuunda ACT na kuweka mikakati ya kujiimarisha kwake vilifanyika lini, wapi, na nani alikuwapo?
 
Kwa nini unajipa ujuzi usio nao?

Unajua vikao vyote vya kuunda ACT na kuweka mikakati ya kujiimarisha kwake vilifanyika lini, wapi, na nani alikuwapo?
Vilifanyika muda mfupi kabla ya Maalim Seif kujiondoa na wafuasi wake iliyokuwa CUF. Na hiyo sio miaka 10 iliyopita.
 
Unajua vikao vyote? Vyote kabisa? Kweli?
 
Mtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?

Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
alipokua anawatetea chadema alikua safi

leo kawageuka basi ni "teja"?

sometimes chadema should grow up na kuacha emotions

cha kujua ni kwamba hakuna mwanadamu loyal wa chochote,akibadilika achaneni nae endeleeni ya yenu

hii kugeuka emotional like little bitches ni theater of public spectacle!
 
Kwa nini unajipa ujuzi usio nao?

Unajua vikao vyote vya kuunda ACT na kuweka mikakati ya kujiimarisha kwake vilifanyika lini, wapi, na nani alikuwapo?

Unajua vikao vyote? Vyote kabisa? Kweli?
Nimecheka kwa nguvu 😂😂. Acha league zisizo na kichwa wala miguu.
 
Back
Top Bottom