GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Fatma ni mwanasiasa?
Kwani mwanasiasa ni nani ? Au unadhani wanasiasa n8 kadi ya chama tambua tofauti ya
1)mwanasiasa
2)mwana chama wa chama cha siasa ...
Kuwa mwana siasa ni kitendo cha mtu kujiusisha na mambo ya siasa kwa namna yoyote ile ...hivyo hata wapiga kura ni wanasiasa kwa hicho kitendo chao cha kwenda kupigia kura wana siasa.
 
Kwani na Wewe kelele unapiga za nini na ligi zizoisha wakati unajua ni haki yake kulingana na mtazamo na akili yake
Mimi napiga kelele kwa sababu mna ji contradict.

Mnapigania haki na demokrasia, halafu mtu akitumia haki yake na demokrasia kukataa No Reforms, No Election, mnamshambulia.

Hamuoni kuwa hii ni contradiction?
 
Hivi karibuni, Fatma Karume ameonekana kubadili mwelekeo wa mijadala yake ya kisiasa kwa namna ambayo imeibua maswali miongoni mwa watanzania, hasa wale wanaoamini katika harakati za mageuzi ya kweli.

Mwanzo, alivamia vikali kauli za Askofu Gwajima aliyekuwa anapinga matukio ya utekaji na ukiukwaji wa haki unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola, akimtuhumu kuwa anatafuta "attention" ya kisiasa, licha ya kwamba hoja za Gwajima zilikuwa na uzito wa kulinda utu na uhuru wa raia.

Sasa, ameibukia tena kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akizibeza juhudi za CHADEMA na sera yao ya "No Reforms, No Elections", akikariri kuwa kusitisha uchaguzi ni kosa la jinai. Kauli hii imechukuliwa na wengi kama kejeli isiyoakisi hali halisi ya mazingira ya kisiasa nchini, ambapo haki za msingi, uhuru wa kisiasa na uhuru wa kutoa maoni vinaendelea kukandamizwa.


View attachment 3397840
Moja ya post ya Fatma Karume

Cha kushangaza zaidi, kauli hizi za Fatma Karume zinatolewa wakati ambapo Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani na mwanasheria mwenzake, yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambayo kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa. Hali hii imezidi kuzua maswali: je, Fatma Karume bado yupo upande wa watetezi wa haki, au amebadili msimamo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika wazi?

Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Hayati John Magufuli, Fatma Karume alijitokeza kuwa mmoja wa sauti thabiti zilizokuwa zikikemea dhuluma, ukandamizaji, na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika utawala wa sasa, ambao nao umeonesha mwelekeo wa kukiuka misingi ya demokrasia, sauti yake imekuwa ya mashaka, wakati mwingine ikisikika kama ya kukubaliabiana na mfumo badala ya kuukosoa.

Je, ni mabadiliko ya kiitikadi? Ni mkakati wa kisiasa? Au kuna mambo ya ndani zaidi ambayo bado hayajawekwa wazi kwa umma? Kwa vyovyote vile, hatua na kauli za Fatma Karume zinahitaji tafakari, hasa kwa wale wanaoamini katika dhana ya "principled activism" yaani, kupigania haki bila kujali nani yuko madarakani.
Fatma kinachomsumbua ni uzanzibari tu. hata Salum Mwalimu baada ya tu ya Mama kushika hatamu na yeye misimo yake yake ilihama jumla. tatizo Uzanzibar tu.
 
ACT miaka 10 iliyopita ndio ilikuwa imeanzishwa, haikuwa na watu wa kuifanya wasusie chochote, usitake kulazimisha. Ulitakiwa useme aliwashauri CUF na sio ACT boss wangu.

CUF wameinunua ACT baada ya CUF kuporwa na CCM. kigumu ni kipi kufahamu hapo?
 
Pia Watanzania wengine wana tabia fulani ya projection.

Projection ni nini? Ni tabia fulani ya kumuwekea mtu baki matarajio yako.

Yani mtu hujakaa naye, hujamuuliza anataka nini, lakini unakuwa unalazimisha tu kuwa huyu lazima atakuwa anafikiri kama mimi.

Siku akipata nafasi ya kufunguka na kukueleza kwamba yeye hafikirii kama wewe, unaumia, unamtukana, unamsema huyu msaliti.

Msaliti kivipi? Kwani mlikubaliana mfikirie sawa?

Nimeliona hili sana Peter Madeleka alivyoondoka CHADEMA na kwenda ACT. Kuna watu wamemsema kama vile walikubaliana naye afe mwanachama wa CHADEMA.

Fatma Karume kasema yeye msimamo wake siku zote ni kushiriki kwenye uchaguzi. Aliishauri ACT takriban miaka 10 iliyopita kushiriki kwenye uchaguzi. Hiyo ilikuwa kabla ya No Reforms No Election. Na hata leo anaendelea na msimamo wake huo huo.

Sasa kuna watu wasiomjua wanasema siku hizi kabadilika, wakati yeye anasema huu ndio msimamo wake na kashautoa takriban miaka 10 iliyopita huko.

Watu wengine wanapenda sana kulazimisha kila mtu afikirie kama wao.
Kuna kitu kimoja unakisahau pamoja na kuwa na Uhuru WA kuchagua upande. Kumbuka kunauchaguzi Kwa wakati Fulani na mazingira Fulani na taaluma yako lazima uonekane mwehu au umenunuliwa. Critical thinking. Swala la wakati huu na mazingira tuliyonayo unaweza simama Kwa watu ukasema okutoba tunatiki na kuzilinda kweri kabisa pamoja na kuwa na Uhuru wa kuchagua ni wako tukuoni kabisa kutoka Moyoni upo Sawa Kwa CCM hii kwamba utazilinda kulaaaaaq????
 
Kuna kitu kimoja unakisahau pamoja na kuwa na Uhuru WA kuchagua upande. Kumbuka kunauchaguzi Kwa wakati Fulani na mazingira Fulani na taaluma yako lazima uonekane mwehu au umenunuliwa. Critical thinking. Swala la wakati huu na mazingira tuliyonayo unaweza simama Kwa watu ukasema okutoba tunatiki na kuzilinda kweri kabisa pamoja na kuwa na Uhuru wa kuchagua ni wako tukuoni kabisa kutoka Moyoni upo Sawa Kwa CCM hii kwamba utazilinda kulaaaaaq????
Sasa hapo ndipo pagumu kwa sababu kuna tofauti za kifalsafa. Kuna mtu mwingine anakwambia nyie ndio mpo upande mbaya kwa sababu mnasusia uchaguzi na hamuwezi kuuzuia. Bora mshiriki mkiibiwa mta document na kuonesha dunia hapa tumeibiwa kutakuwa na ushahidi wa ku discredit CCM.

Msiposhiriki kabisa mnawapa ushindi wa mezani CCM wa kupita bila kupingwa hata mkisema wameiba kura mkiulizwa wameiba kura ipi, wapi, hamuwezi kuweka ushahidi.
 
Mkuu!
Kwa kutumia akili ya kawaida tu, mtu anayesimamia kushiriki uchaguzi chini ya sheria hizi kandamizi, bila kuzikosoa wala kuzipinga, huoni kama kwa njia moja au nyingine anatoa uhalali kwa wale wahuni waliotunga sheria hizo?

Au ndiyo falsafa hiyo!?

Chadema mumeshiriki mara ngapi uchaguzi kwa sheria hizi hizi?
 
Kilichofanyika
Kizimkazi kajiunganisha na family ya Karume ,kwakifupi wale kwasasa ni wanafamily moja so kutegemea kusikia tofauti ya tunachokisikia nilazima itakuwa ni ndoto ya kutisha
 
Back
Top Bottom