Nini kilimuua Profesa Hubert Kairuki?

Nini kilimuua Profesa Hubert Kairuki?

1. Mheshimiwa Prof Kairuki ndie mwasisi wa Hospitali Maarufu nchin na duniani kwa TIBA na MAFUNZO kwa fani za utabibu. Nilitaka kufahamu je nini sababu ya kifo chake?.

2. Je ni ajali ya ghafla? Kama ni ugonjwa ilikuaje bingwa katika fani ya utabibu kiwango chake hakupata matibabu yenye ubora kwa haraka?

**Hakika ameacha taasisi imara ya kupigiwa mfano.

Pumzika kwa amani Profesa
Prof Hubert Kairuki, alikuwa ni Daktari wa Binadamu Bingwa wa Magonjwa ya Akina Mama mwenye maono ya mbali. Nakumbuka kabla ya kuanzisha Hospitali alikuwa akipiga part time katika pale Burhani iliyopo mtaa wa Kaluta.
Na hiyo hospitali yake ilipoanza ilikuwa katika jengo la kawaida la ghorofa 1 na nakumbuka 1987 nilihudumiwa na Prof Mselle wa BIochemistry akiwa ni Registrar.
Hatimaye ndoto zake zimetimia, safari ya miaka 39 iliyopita
 
Prof Hubert Kairuki, alikuwa ni Daktari wa Binadamu mwenye maono ya mbali. Nakumbuka kabla ya kuanzisha Hospitali alikuwa akipiga part time katika pale Burhani iliyopo mtaa wa Kaluta.
Na hyo hospitali ilipoanza ilikuwa katika jengo la ghorofa 1 na nakumbuka 1987 nilihudumiwa na Prof Mselle wa BIochemistry akiwa ni registrar.
Hatimaye ndoto zake zimetimia, safari ya miaka 39 iliyopita
naam na sasa ana Hospital pamoja na chuo cha uuguzi na udaktari ,Herbert kairuki memorial university
 
Wazawa wanapokua na ndoto kubwa zenye kutishia maslahi ya wakusudiwa kuwa ma don,unaingizwa kwenye black list patern!

Reginald Mengi,Rama wa kariakoo hao,super Sami,n.k hayo ni baadhi ya wazawa ambao wamewahi kuingia kwenye Kashi Kashi au kulalamika plus kuhofia uhai wao!!

Hatujui maono yake yalitishia kiasi Gani wafadhili wakuu wa tiba hapa bongo!!

Nawaza,kama kawaida yangu!!
 
Prof Hubert Kairuki, alikuwa ni Daktari wa Binadamu Bingwa wa Magonjwa ya Akina Mama mwenye maono ya mbali. Nakumbuka kabla ya kuanzisha Hospitali alikuwa akipiga part time katika pale Burhani iliyopo mtaa wa Kaluta.
Na hiyo hospitali yake ilipoanza ilikuwa katika jengo la kawaida la ghorofa 1 na nakumbuka 1987 nilihudumiwa na Prof Mselle wa BIochemistry akiwa ni Registrar.
Hatimaye ndoto zake zimetimia, safari ya miaka 39 iliyopita
Majibu na Shuhuda kama hizi ndiyo zinatakiwa hapa.
Kwa niaba nashukuru mkuu
 
Mfano Bora kabisa kwa jamii yetu namna ya kuendesha taasisi
Watoto hawakugombea "kuuza Kila mtu afe na chake"
Mkewe akiwa Senior Nurse pale Muhimbili walihakikisha wanasomesha watoto ambao kwa sasa chini ya uangalizi wa Mama na Bodi imara wamefanya mambo makubwa mno.

Mtoto mjengeshe shule kichwani matofali, mchanga na sementi atatafuta mwemyewe. Ukijenga nyumba yako kwa watoto wasiojielewa wataishia kuipiga bei na kugawana mpunga na wala hawatakukumbuka kabisa.
 
Back
Top Bottom