Nini kilimsibu Haruna Moshi?

wakuu nimewasoma, ukweli inasikitisha sana na ninamuonea huruma BOBAN, kutoka timu iliyo qualify kushiriki michuano ya UEFA na kuamua kurudi ligi yetu ya nyumbani ni anguko kubwa sana kimaendeleo, nafikiri hii inadhihirisha kukosa mshauri wa karibu, huenda kisaikologia hayuko fine, maana haiingii akilini hata kidogo,
 
...Kwa mujibu wa maelezo ya wakala wake Damas Ndumbaro, Haruna alikatisha mkataba wake na hiyo timu aliyokuwa akichezea huko Sweden kwa sabau kubwa mbili 1. Haoni kama kuna maslahi kuendelea kuichezea hiyo timu kwa nikipato apatacho kwa mtazamo wake ni kidogo 2. Kiwangi cha soka sweden haoni kama ni cha ushindani ingawa kuna maelezo kuwa hiyo timu ime-qualify kucheza kombe la ulaya????!!!!

Lakini kwa maoni yangu nilichoona kwa upande wa Haruna ni upeo mdogo wa kujua mambo na pia kukosa dhamira ya kucheza soka la ushindani. Haruna yeye hataki kukatwa kodi kwenye mshahara wake (pay as you earn), alitafutiwa nyumba lakini akatakiwa alipie kodi mwenyewe.

Nimegundua wachezaji wetu wengi wa soka wana akili finyu sana (sitaki kuzungumzia elimu hapa) maana kama ni elimu akina George Weah walipiga soka ulaya na hawakuwa na elimu sana au akina Kanu, Toure. isipokuwa wanakosa dhamira ya kweli kutaka kucheza soka ulaya na pia kukosa malengo. Hivi kwa timu kuweza kupata tiketi ya kucheza ubingwa wa ulaya si ndio ilikuwa njia ya yeye kuonyesha umahili wake ili aonekane na hatimaye kupata timu kubwa zaidi na hatimaye kupata mkataba wenye maslahi zaidi??

Kwa hiyo Haruna ameona bora kurudi simba...Kweli akilini nywele!!!
A%20S%2039.gif
A%20S%2039.gif
:frusty::frusty:

Huyu mchezaji amewakilisha tabia za Watanzania wengi hasa wanajiita wafanyabiashara wenye tabia ya kutokupenda kulipa kodi. Si ajabu kumkuta mtua anamiliki nyumba, ana gari lakini hana faili lake la kodi TRA.

Hata walioajiriwa wengi nao wanamawazo yanayofanana na huyu mchezaji, utakuta unamlipa mtu mshahara kuliko hata mfanyakazi wa serikali mwenye elimu sawa au juu yake bado anakujia, tunaomba utulipe allawansi ya chakula cha mchana, yaani hela yake ikiingia benki hata kugusa.

Ni muda kwa watanzania kubadilika.
 
Watu walikuwa wanamlaumu MAXIMO sasa mambo yanajidhihirisha
 
wakuu nimewasoma, ukweli inasikitisha sana na ninamuonea huruma BOBAN, kutoka timu iliyo qualify kushiriki michuano ya UEFA na kuamua kurudi ligi yetu ya nyumbani ni anguko kubwa sana kimaendeleo, nafikiri hii inadhihirisha kukosa mshauri wa karibu, huenda kisaikologia hayuko fine, maana haiingii akilini hata kidogo,
..Unajua mkuu kuna wakati aliyekuwa katibu mkuu wa Simba Mwina Kaduguda aliwahi kusema redioni kuwa wachezaji wa soka Tanzania wanahitaji kwenda shule...Watu wengi hawakumuelewa Kaduguda na baadhi ya wachezaji walifikia hatua ya kumshutumu kuwa amewadhalilisha.

Ok, wengi tunaamini shule lazima uwe ndani ya chumba cha kuta nne na mwalimu amesimama pale mbele anafundisha, lakini kumbe kuna mambo mengine ambayo mtu unaweza kujifunza kutokana na kukubali kuwa karibu na watu wenye maono ya mbali na ukaweza kufanikiwa. Kilichomtokea Boban licha ya mibangi yake ni kukosa maono na utambuzi kuwa kuna mambo ambayo ili ufanikiwe lazima ukubali kutoka jasho sana na pia ikibidi ukubali kuwa hujui kitu ili uweze kujifunza (Please refer to my signature down here!!).

Sasa kama yeye aliamini kuwa anaweza kupata pesa kupitia kucheza soka alitakiwa atambue kuwa ili kufikia mafanikio basi analazimika kufanya kazi ya ziada. Na kwa kweli alitakiwa kumshukuru sana Ndumbaro kwa kumpatia nafasi ya kucheza soka ulaya na ilikuwa ndio nafasi yake ya kupiga bao.

Nonda Shaaban alipotoka burundi na kuja Tanzania tulikuwa tunamuona tu kama wachezaji wengine tuliowazoea akichezea Yanga, lakini yule mtu alikuwa na malengo alitoka hapa akaterezea South Afrika, then Switzerland mara France na tulimuona katika michuano ya UEFA 2006 akiwa Monaco. Nasikia baadae alienda Italy lakini ndio hivyo tena ni mbele kwa mbele.

Kuna siku tulikaa na Edibily Lunyamila maeneo ya Sinza pale nikamwambia Lunya hivi ulijisikiaje ulipokuwa unamuangalia Nonda kwenye runinga anapiga soka ulaya..jamaa alibaki kimya na akawa mnyonge akajibu kuwa kila mtu na bahati yake..nilimshangaa sana kwenye soka kuna bahati bila juhudi na malengo??

Sasa Boban yeye wakati akili yake imemtuma kukatisha mkataba akawa anadai gate collection, mara haendi mazoezini anadai anaumwa yaani ni uswazi 100%!!!
 
Hivi wahandishi wetu hawawezi kuwasiliana na hiyo timu kwa ajili ya verifications au mambo ya 'every story has two sides' Tanzania haya-apply?
 
Hivi wahandishi wetu hawawezi kuwasiliana na hiyo timu kwa ajili ya verifications au mambo ya 'every story has two sides' Tanzania haya-apply?

Waandishi gani? Waganga njaa hawa?

They wouldn't see a story if it was right in front of their faces. Hapa inaonekana jamaa kwa njia moja au nyingine kachemsha, sasa anatupa stories nyingi. Na "waandishi" wetu hata kutumia email hawajui.

Mtu aliyesota na mpira wa bongo hawezi kutaka kurudi bongo kirahisi rahisi hivi, labda waseme tu kapigwa chini au kaharibu vingine.
 
...Kwa mujibu wa maelezo ya wakala wake Damas Ndumbaro, Haruna alikatisha mkataba wake na hiyo timu aliyokuwa akichezea huko Sweden kwa sabau kubwa mbili 1. Haoni kama kuna maslahi kuendelea kuichezea hiyo timu kwa nikipato apatacho kwa mtazamo wake ni kidogo 2. Kiwangi cha soka sweden haoni kama ni cha ushindani ingawa kuna maelezo kuwa hiyo timu ime-qualify kucheza kombe la ulaya????!!!!

Lakini kwa maoni yangu nilichoona kwa upande wa Haruna ni upeo mdogo wa kujua mambo na pia kukosa dhamira ya kucheza soka la ushindani. Haruna yeye hataki kukatwa kodi kwenye mshahara wake (pay as you earn), alitafutiwa nyumba lakini akatakiwa alipie kodi mwenyewe.

Nimegundua wachezaji wetu wengi wa soka wana akili finyu sana (sitaki kuzungumzia elimu hapa) maana kama ni elimu akina George Weah walipiga soka ulaya na hawakuwa na elimu sana au akina Kanu, Toure. isipokuwa wanakosa dhamira ya kweli kutaka kucheza soka ulaya na pia kukosa malengo. Hivi kwa timu kuweza kupata tiketi ya kucheza ubingwa wa ulaya si ndio ilikuwa njia ya yeye kuonyesha umahili wake ili aonekane na hatimaye kupata timu kubwa zaidi na hatimaye kupata mkataba wenye maslahi zaidi??

Kwa hiyo Haruna ameona bora kurudi simba...Kweli akilini nywele!!!
A%20S%2039.gif
A%20S%2039.gif
:frusty::frusty:
timu yake imeshika nafasi ya 10 ktk ligi haijafanikiwa kucheza kombe lolote ulaya,nenda ktk Gefle IF - Wikipedia, the free encyclopedia
 
mnapoteza muda kumjadili huyu *****,tuachane naye sasa kasharudi basi alivute hilo bangi mpaka limkome kisha akapigane na makocha na vibabu vilivyotawala soka la bongo.:mad:
 
Waandishi gani? Waganga njaa hawa?

They wouldn't see a story if it was right in front of their faces. Hapa inaonekana jamaa kwa njia moja au nyingine kachemsha, sasa anatupa stories nyingi. Na "waandishi" wetu hata kutumia email hawajui.

Mtu aliyesota na mpira wa bongo hawezi kutaka kurudi bongo kirahisi rahisi hivi, labda waseme tu kapigwa chini au kaharibu vingine.

...Nimeipenda hii! :pound:
 
...Plus wamezoea kutetemekewa na mashabiki wa Yanga au Simba. akiingia hoteli msosi bure, akiingia Bar bia za bure huku vimwana wakimpapatikia. Akifika Ulaya anashangaa kila mtu na hamsini zake. Kweli mashabiki wanaweza kukupapatikia kama utaonyesha mpira wanaopenda lakini hakuna atakayeklununulia msosi ama bia za bure, labda 'viburudisho' unaweza ukapata, maana hata huko wako mabinti wengi tu wanaopapatikia wachezaji!

Hili la kutotaka mshahara wake usikatwe kodi, tumsamehe bure. kwanza ni suala la upeo. lakini tukumbuke kuwa anatoka nchi ambayo kukwepa kulipa kodi ni bonge la ujanja halafu ghafla anajikuta kwenye nchi ambayo kulipa kodi ni ufahari maana wananchi wanafundishwa toka utotoni wajibu wa kulipa kodi.

Hii ya kutaka kupata fedha kutoka kwenye gate collection tusimlaumu sana. Ndio malezi aliyopata kutoka 'Baba' Simba na Yanga ambazo pamoja na kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 mpaka leo hii hazina miradi ya kuwaingizia pesa na zinategemea mapato ya getini ambayo nusu yake inakwenda kwa makomandoo!
Kaaaz kweli kweli.
 
Kule Sweden bangi imehalalishwa. Huyu jamaa alikuwa anachukua kwa bill ikifika mwisho wa mwezi hana hela! Kwa mujibu wa watu waliokuwa wanafuatilia nyendo zake akiwa huko>
 
UKWELI:

Tanzanian star Haruna Moshi returns home from Sweden

By Emmanuel Muga
BBC Sport, Dar-es-Salaam

Tanzanian international Haruna Moshi has returned home to doubts and questions after failing to impress in the Swedish first division.

Moshi had signed a two-year contract with Swedish premier league side Gefle IF last year but the deal was brought to an end earlier in July.

He said he found life in Sweden difficult and had no option but to terminate his contract and return home.

But the player's agent Damas Ndumbaro has attacked his client for squandering a superb chance.

"He had an opportunity to excel and play in the [European] Champions League, which he has now squandered," Ndumbaro said.

Ndumbaro said that one reason Moshi had come back to Tanzania was because he did not wanted to pay Swedish taxes.

But the Gefle IF coach denied that there had been any problems with Moshi.

"Moshi has many good qualities but he found it difficult to adjust to our system," Per Olsson told the BBC.

"We have both agreed that this [terminating the contract] was the best solution, and there were no hard feelings," he added.

Tanzanian fans are disappointed that Moshi's career in Europe is apparently over.

There are no Tanzanians playing at a high level in Europe.
 
kule sweden bangi imehalalishwa. Huyu jamaa alikuwa anachukua kwa bill ikifika mwisho wa mwezi hana hela! Kwa mujibu wa watu waliokuwa wanafuatilia nyendo zake akiwa huko>
wewe acha kuleta story za vijiweni wewe
na kwanza bangi sio sababu haijahalalishwa ila ukitaka unapata iko bwerere.
 
Back
Top Bottom