SoC01 Nini kifanyike kuimarisha Demokrasia ya Tanzania ?

Stories of Change - 2021 Competition

Abiri

New Member
Jun 20, 2021
3
1
Neno Demokrasia linamaanisha utawala wa watu (chanzo ; kamusi huru). Ili demokrasia iwepo wanahitajika watu wenye kuanzisha utawala wao ambao utawaongoza kwenye nyanja mbalimbali katika jamii husika.

Demokrasia ya Tanzania
Tanzania ni kama nchi nyingine zenye kufata demokrasia hii ni kwa kutumia demokrasia shirikishi (kuchagua wawakilishi wa wananchi). Katiba ya Tanzania inafahamu uwepo wa bunge, vyama vingi kama nguzo muhimu ya demokrasia nchini.
Kama mtanzania mwenye nia nzuri na nchi yangu ukweli usiofichika ni kwamba demokrasia ya Tanzania kwa sasa inazidi kuzorota hii ni kwa sababu :

1:Watu wanakosa imani na baadhi ya mihimili muhimu kama vile jeshi la polisi,bunge,tume ya uchaguzi na mahakama.

(a)Bunge: tukiachana ushabiki wa vyama vyetu vya siasa ,wana nchi hawa wachukii wabunge bali wanachukia kile atakacho fanya mbunge wake hasa kikiwa hakina maslahi kwake, wakati wananchi wanalala moja hali ngumu na pesa hazipo serikali inaahidi kuacha pesa kuja kwenye mzunguko na watu wakapata matumaini kabla pesa izi hazijafikia mwananchi kule chini mwananchi tozo ama kodi ndo kitu cha kwanza kumfikia, kitendo hiki kunamfanya mwananchi apoteze imani na mbunge wake kwakua kashindwa pigana ije pesa kwanza kabla ya tozo au kodi
 
Back
Top Bottom