Nini kifanyike Jeshi la Polisi lianze kutenda haki?

Wanayaona Wanayasikia wana agiza
Mahakama KUU Mbeya emwachia MDUDE wa CHADEMA kwa kuwekewa MADAWA ya KULEVYA na POLISI ni DOSARI KUBWA kwa JESHI nilitarajia RPC MBEYA ANGEWAJIBIKA kwa Kulitia Dosari JESHI kuwa Linawafanyia hivyo RAIA lakini Yupo anachapa kazi

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Ubambikiaji umekuwa sera rasmi ya wanakijani na wasaidizi wao.
 
Shida siyo polisi, shida siyo CCM, shida siyo CHADEMA, shida siyo serikali wala siyo Katiba, shida ni sisi watanzania (Waafrika) hata leo tuletewe katiba mpya ya aina gani bado uzandiki wetu ni uleule...hata Mh Mbowe akiwa Rais leo bado uchafu ni uleule, hata Mh Samia aendelee kuwa rais uchafu ni uleule...Sisi waafrika ni viumbe wa ajabu sana, tuna ubinafsi, tuna chuki za ajabu, ni wenye tamaa, ni wezi, wala rushwa, upendeleo umetutawala, leo hii nchi hata iongozwe na CHADEMA, CUF, TLP, ADA-TADEA, ACT nk hakuna chochote tutapata viongozi wataendelea kujishibisha wao, ajira watapeana wao, watoto wao kwanza wataingia BoT, TANAPA, BANDARI, NSSF, BUNGENI, IKULU, TRA, na sehemu zote zenye mboga saba watatawala wao. Mnataka katiba mpya nawashangaa hakuna kipya kitatokea, mnao ikataa katiba Mpya nawashangaa pia hamna la maana la kutueleza. Mtanzania unayejitambua unaweza kuamua kuachana na upuuzi wa kufikiria ni jinsi gani taifa lako linaendeshwa, ukashika jembe ukalima maisha yatakuwa ya kadri....unavunjwa miguu eti unadai katiba mpya...ni ushenzi kama ushenzi mwingine maana hata iwe mpya haitakusaidi chochote bali wana siasa wataendelea kuneemeka.Mbowe, Zito, Msigwa, Mdude, Lisu nk wanahangaika ili wawe kwenye mfumo, wakisha ingia kwenye mfumo hizo kelele hutazisikia tena...wako wapi akina Esta Matiko, wakoa wapi akina Halima Mdee,(covid19) nk. Mbona hawadai katiba mpya kwa sasa, je unafikiri wangekuwa hawakupewa keki na akina Ndugai na Magufuli sasa hivi si na wao wangekuwa rumande kwa harakati za kudai Katiba Mpya? Ampherey Polepole sasa hivi anatembelea kwenye uzi mwembamba unaona yuko kinyume na serikali lakini sababu ni kwamba umeshatemwa na mfumo, je kipindi cha Magufuli hata usiku angeuita mchana ili mradi aendelee kula mema ya nchi. Mfano mzuri tukumbuke ya akina Lowassa (2015), kumbuka yule kijana Patrobas Katambi, kumbuka MWITa Waitara, kumbuka Vicent Mashinji, kumbuka Joshua Nassari, kumbuka Silinde, nk kuna watu walivunjwa miguu kwa sababu tu ya hao wazandiki niliotaja hapo juu, kuna watu wamewekwe rupango, kuna watu wameacha wajane na yatima kwa ajili ya Wapuuzi hao, kuna watu wamepoteza mwelekeo wa maisha kisa wanadai haki kwa kupitia migongo ya hao.....leo akina Mwita Waitara wanakula keki ya Taifa lakini waliowavujia damu na jasho wanawaona wapuuzi tuu. Vijana achaneni na siasa, shida sisi waafrika ni viumbe wa hovyo sana....mnaopoiga kelele leo mkipewa keki mnanyamaza....oooh kumbe hamdai haki bali ni njaa za Uafrika zinawasumbua...fanya kazi zako tafuta pesa utaishi kwa raha sana ukiyafikiria ya Serikali basi utaishia kuumia kila siku.
Kunyamaza sii dawa,kukatatamaaa sii dawa,kushima jembe na kwenda kulima bado sii dawa,ila mabadiliko ya kweli yenye kujenga mifumo imara,na yote ni kupitia katiba mpya tu.Mengine yatanengwa kutokana na hapo.
 
Siku wakiacha tu kutumiwa na si si emu kama 🦮🐕‍🦺 , ndiyo siku ambayo wataanza rasmi kutenda haki. Hata lile jina lao la polisisiemu huenda likaishia hapo.
 
Japo ni kweli, kunapomwagika machozi, jasho na damu kwa ukosefu wa haki, karma huingilia kati, la hata naniliu ni karma, lakini kwenye hili, nasema hapana, Mungu apishilie mbali,
Ushauri wangu ni huu
P
Mungu apishie mbali - hayo ni maombi yetu sote!
 
Back
Top Bottom