M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Siyo rahisi mahali popote duniani kwa mtu awaye yote kuweza kuzuia athari hasi (consequences) za machozi ya watu zaidi ya milioni 50. Never!
Watanzania walilia sana mwaka 2020 kuhusu serekali yetu (hususani rais wa wakati huo Magufuli) kuona kuwa ipo kwenye denial state dhidi ya gonjwa baya la korona (COVID-19).
Hata wataalamu wa afya nguli kabisa nchini tunaowajua (sitaji majina - ni wengi) nao hawa walikuwa wameingia kati kulicheza hili sebene la wanasiasa (aka Magufuli).
Watanzania walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa "Hivi afe nani hapa nchini ndipo serekali yetu ianze kuchukua hatua madhubuti dhidi ya korona?".
Kilio cha uchungu wa Watanzania kikafika kunakohusika, likatokea la kutokea, na sasa hadi chanjo tumekubali kuchanjwa!
Machozi ya Watanzania bado yanatiririka dhidi ya madhira mengine mengi yanayohusiana na serekali yetu kwa sasa kuendeshwa kijeshi. Police State.
Raia wema wanapotoa hisia juu ya maisha yao yanayowazunguka na ambayo ni serekali pekee ndiyo yenye wajibu wa kuyapatia ufumbuzi au kuyasemea - kinachotokea ni majeshi yenye silaha kali dhidi ya raia wasio na hatia. Hoja za kisiasa zinajibiwa kwa mtutu na mabomu. Hoja za kijamii majibu yake ni kubambikiwa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi, nk.
Chama tawala kiko likizo - jeshi la polisi ndilo lililoshika hatamu na kufanya siasa kwa niaba ya chama tawala (kumbuka yule askari polisi aliyemwambia Mbowe kule jimboni Hai wakati wa uchanguzi wa 2020 kuwa hata afanye nini hawezi kushinda ubunge, na hapa juzi kati amenukuliwa tena akisema Mbowe kwenye kesi ya ugaidi hachomoki).
Udongo wa ardhi ya mama Tanzania umekuwa "tear-logged" (water-logged) kwa mafuriko ya machozi ya Watanzania zaidi ya milioni 50 wanaolilia haki na uhuru wao.
Ni machozi haya haya ndiyo yaliyolowanisha ardhi ya mama Tanzania mwaka 2020 dhidi ya serekali kutochukua hatua stahiki dhidi ya korona, machozi yaliyopelekea yatokee yaliyotokea na hatimaye sasa hata chanjo ya korona tumeikubali.
Machozi ya Watanzania ya sasa mwaka huu wa 2021 dhidi ya serekali ni "Je, katika huu mvutano uliopo kati ya raia na jeshi la polisi kuhusu masuala ya haki na uhuru - serekali inataka kuona nani wanakufa ndipo ichukue hatua za kuhakikisha jeshi hili linatenda haki kwa Watanzania?". Machozi yatapelekea litokee la kutokea. Litatokea.
Mimi ni mtu niliaye kutoka nyikani.