Dkt. Biteko: Polisi zingatieni haki katika utendaji wenu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutenda haki wakati wote wa utendaji wao wa kazi, wachukie rushwa na wajikite katika kutatua matatizo ya watanzania kwani usalama wa watanzania upo mikononi mwa Jeshi hilo.

Amesema hayo, leo Novemba 16, 2023 wakati wa kilele cha mahafali ya kufunga mafunzo Namba 1/2022/2023 ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi Tanzania iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi jijini Dar es Salaam.

"Tendeni haki, kwani haki hulistawisha Taifa, anayestahili haki apate na anayestahili adhabu apate, anayestahili kwenda mahakamani aende kwa haki, msibambikie watu kesi pia chukieni rushwa kwani rushwa hupofusha akili ya Binadamu," amesisitiza Dk.Biteko.

Aidha, Dk. Biteko amelitaka Jeshi la Polisi kutoona fahari ya vyeo wanavyopata, bali fahari ya kazi itokane na huduma wanayotoa kwa watanzania hivyo wajikite kwenye kusikiliza mahitaji ya wananchi kwani wananchi wanachohitaji ni uwepo wa Jeshi la Polisi imara litakalohakikisha usalama wao.

Kuhusu ujenzi wa majengo ya Utawala katika Chuo hicho ambayo bado hayajakamilika, ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani isimamie utekelezaji wa suala hilo kwani Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan ameshatoa sh. bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi majengo katika chuo hicho.
 
Siku ingine awaongezee kwa kuwaambia waache tamaa ya mali/fedha za watu hadi wafikirie kuua kabisa.Refer: Abdallah Zombe and his partners in crimes.
 
Siku ingine awaongezee kwa kuwaambia waache tamaa ya mali/fedha za watu hadi wafikirie kuua kabisa.Refer: Abdallah Zombe and his partners in crimes.

Watu kama polisi,walioaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya maisha ya watu,halafu serikali ya kihuni kuamua kuwalipa inavyowalipa.

Nyinyi wananchi mtaendelea kuwa wahanga sana wa matukio ya ajabu ajabu kutoka kwa polisi,watu kama akina biteko wanajua sababu ya hayo ila wanajibaraguza na ushauri.
 
Kwa vyeo wanavyopanda polisi , kufikia 2030 Hadi nyota mbili atashika smh kwenda LINDO.
 
"Tendeni haki, kwani haki hulistawisha Taifa, anayestahili haki apate na anayestahili adhabu apate, anayestahili kwenda mahakamani aende kwa haki, msibambikie watu kesi pia chukieni rushwa kwani rushwa hupofusha akili ya Binadamu," amesisitiza Dk.Biteko.
Kila mtu anawalalamikia Polisi, kila siku Polisi hahahhaa hawa jamaa hawawezakaniki
 
Back
Top Bottom