Nini kifanyike Jeshi la Polisi lianze kutenda haki?

Ushauri wangu ni kwamba Jeshi hili la Polisi livunjwe lisukwe jeshi la Polisi jipya liwe na asilimia kubwa ya Wasomi wa Forensics

Tuwe na Polisi walioenda Shule ambao wakiamrishwa kufanya mambo ya ajabu wanahoji amri hizo na wanakaa upande wa Wananchi ambao ndio waajiri wao kwa Kodi zao.
Askari waovu ni wachache sana ukilinganisha na wengi waadilifu.
Njia rahisi ni kuwapa elimu ya uraia wananchi, kuwatambua wale askari wabaya na kuweka makosa yao hadharani.
Hali hiyo itawafanya waone aibu, familia zao pia zitaona aibu na hivyo kujirekebisha.
Kosa kubwa linalolea watu waovu nchini ni kutoa lawama za jumla kwa serikali, polisi, CCM n.k.
Lawama za jumla zinatumika kama kichaka cha kujificha waovu.
Ni rahisi sana kumshughulikia mtu mwenyewe kuliko kundi, hii ni kanuni ya asili, hata wanyama wawindao wanalijua hili.
 
Siyo rahisi mahali popote duniani kwa mtu awaye yote kuweza kuzuia athari hasi (consequences) za machozi ya watu zaidi ya milioni 50. Never!

Watanzania walilia sana mwaka 2020 kuhusu serekali yetu (hususani rais wa wakati huo Magufuli) kuona kuwa ipo kwenye denial state dhidi ya gonjwa baya la korona (COVID-19).

Hata wataalamu wa afya nguli kabisa nchini tunaowajua (sitaji majina - ni wengi) nao hawa walikuwa wameingia kati kulicheza hili sebene la wanasiasa (aka Magufuli).

Watanzania walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa "Hivi afe nani hapa nchini ndipo serekali yetu ianze kuchukua hatua madhubuti dhidi ya korona?".

Kilio cha uchungu wa Watanzania kikafika kunakohusika, likatokea la kutokea, na sasa hadi chanjo tumekubali kuchanjwa!

Machozi ya Watanzania bado yanatiririka dhidi ya madhira mengine mengi yanayohusiana na serekali yetu kwa sasa kuendeshwa kijeshi. Police State.

Raia wema wanapotoa hisia juu ya maisha yao yanayowazunguka na ambayo ni serekali pekee ndiyo yenye wajibu wa kuyapatia ufumbuzi au kuyasemea - kinachotokea ni majeshi yenye silaha kali dhidi ya raia wasio na hatia. Hoja za kisiasa zinajibiwa kwa mtutu na mabomu. Hoja za kijamii majibu yake ni kubambikiwa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi, nk.

Chama tawala kiko likizo - jeshi la polisi ndilo lililoshika hatamu na kufanya siasa kwa niaba ya chama tawala (kumbuka yule askari polisi aliyemwambia Mbowe kule jimboni Hai wakati wa uchanguzi wa 2020 kuwa hata afanye nini hawezi kushinda ubunge, na hapa juzi kati amenukuliwa tena akisema Mbowe kwenye kesi ya ugaidi hachomoki).

Udongo wa ardhi ya mama Tanzania umekuwa "tear-logged" (water-logged) kwa mafuriko ya machozi ya Watanzania zaidi ya milioni 50 wanaolilia haki na uhuru wao.

Ni machozi haya haya ndiyo yaliyolowanisha ardhi ya mama Tanzania mwaka 2020 dhidi ya serekali kutochukua hatua stahiki dhidi ya korona, machozi yaliyopelekea yatokee yaliyotokea na hatimaye sasa hata chanjo ya korona tumeikubali.

Machozi ya Watanzania ya sasa mwaka huu wa 2021 dhidi ya serekali ni "Je, katika huu mvutano uliopo kati ya raia na jeshi la polisi kuhusu masuala ya haki na uhuru - serekali inataka kuona nani wanakufa ndipo ichukue hatua za kuhakikisha jeshi hili linatenda haki kwa Watanzania?". Machozi yatapelekea litokee la kutokea. Litatokea.

Mimi ni mtu niliaye kutoka nyikani.
Dawa ni katiba itakayo sababisha c.c.m watoke madarakani.
 
Mleta mada pole kwa kujifanya unauchungu zaidi na Mbowe kuliko viongozi wa chadema, akiwemo Lisu, Mnyika, Sugu, Msigwa na familia yake kwa ujumla. Hivi unafikiri hao kukaa kwao kimya ni kwa bure?

Ukweli ni kwamba viongozi karibu wote wameshamchoka Mbowe ndan ya chama, na ni hao hao walioenda kupeleka taarifa kwa vyombo vya usalama, navyo bila kusita wakachukua hatua.

Mbowe angekuwa na maono baada ya kucheza boko ya kumleta Lowasa ndan ya chama mwaka 2015 angejiuzuru kulinda heshima yake, au angeachana na tamaa yake ya kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti wa chadema ambao unamruhusu yeye kukalia kiti hicho kwa muda usiojulikana.

Na uamuzi wake huo ndio una mcost leo. Acha kusingizia polisi wao wanafanya kazi yao kwa mujibu wa sheria.
Pathetic!
 
Sawa!
 
Dawa ni katiba itakayo sababisha c.c.m watoke madarakani.
Tatizo siyo CCM, ni wachache ndani ya CCM na serikali.
Hizi lawama za jumla ndizo huwatengenezea kichaka cha kujificha waovu.
Katiba mpya haina maana yoyote kama wananchi hawawezi kuilinda iliyopo.
Asilimia kubwa ya wanaCCM ni raia wema wasiotaka wengine waumizwe na wanatambua kuwa wote ni ndugu na taifa moja.
Uovu hauna chama, watanzania wote wanatakiwa kuungana kuupinga.
 
Siyo rahisi mahali popote duniani kwa mtu awaye yote kuweza kuzuia athari hasi (consequences) za machozi ya watu zaidi ya milioni 50. Never!

Watanzania walilia sana mwaka 2020 kuhusu serekali yetu (hususani rais wa wakati huo Magufuli) kuona kuwa ipo kwenye denial state dhidi ya gonjwa baya la korona (COVID-19).

Hata wataalamu wa afya nguli kabisa nchini tunaowajua (sitaji majina - ni wengi) nao hawa walikuwa wameingia kati kulicheza hili sebene la wanasiasa (aka Magufuli).

Watanzania walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa "Hivi afe nani hapa nchini ndipo serekali yetu ianze kuchukua hatua madhubuti dhidi ya korona?".

Kilio cha uchungu wa Watanzania kikafika kunakohusika, likatokea la kutokea, na sasa hadi chanjo tumekubali kuchanjwa!

Machozi ya Watanzania bado yanatiririka dhidi ya madhira mengine mengi yanayohusiana na serekali yetu kwa sasa kuendeshwa kijeshi. Police State.

Raia wema wanapotoa hisia juu ya maisha yao yanayowazunguka na ambayo ni serekali pekee ndiyo yenye wajibu wa kuyapatia ufumbuzi au kuyasemea - kinachotokea ni majeshi yenye silaha kali dhidi ya raia wasio na hatia. Hoja za kisiasa zinajibiwa kwa mtutu na mabomu. Hoja za kijamii majibu yake ni kubambikiwa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi, nk.

Chama tawala kiko likizo - jeshi la polisi ndilo lililoshika hatamu na kufanya siasa kwa niaba ya chama tawala (kumbuka yule askari polisi aliyemwambia Mbowe kule jimboni Hai wakati wa uchanguzi wa 2020 kuwa hata afanye nini hawezi kushinda ubunge, na hapa juzi kati amenukuliwa tena akisema Mbowe kwenye kesi ya ugaidi hachomoki).

Udongo wa ardhi ya mama Tanzania umekuwa "tear-logged" (water-logged) kwa mafuriko ya machozi ya Watanzania zaidi ya milioni 50 wanaolilia haki na uhuru wao.

Ni machozi haya haya ndiyo yaliyolowanisha ardhi ya mama Tanzania mwaka 2020 dhidi ya serekali kutochukua hatua stahiki dhidi ya korona, machozi yaliyopelekea yatokee yaliyotokea na hatimaye sasa hata chanjo ya korona tumeikubali.

Machozi ya Watanzania ya sasa mwaka huu wa 2021 dhidi ya serekali ni "Je, katika huu mvutano uliopo kati ya raia na jeshi la polisi kuhusu masuala ya haki na uhuru - serekali inataka kuona nani wanakufa ndipo ichukue hatua za kuhakikisha jeshi hili linatenda haki kwa Watanzania?". Machozi yatapelekea litokee la kutokea. Litatokea.

Mimi ni mtu niliaye kutoka nyikani.
Afe amiri jeshi ndio kutakuwa na mabadiliko manake pengine makamu wake ni msikivu zaidi.
 
Katiba mpya itawafungua police kulinda chama badala ya nchi.
Eti police anampigia saluti mwanasiasa ambae ni raia ,hali saluti ni salamu ya kijeshi.
Muundo wa police ni mfumo wa kijamaa kulinda chama.
 
Mleta mada pole kwa kujifanya unauchungu zaidi na Mbowe kuliko viongozi wa chadema, akiwemo Lisu, Mnyika, Sugu, Msigwa na familia yake kwa ujumla. Hivi unafikiri hao kukaa kwao kimya ni kwa bure?

Ukweli ni kwamba viongozi karibu wote wameshamchoka Mbowe ndan ya chama, na ni hao hao walioenda kupeleka taarifa kwa vyombo vya usalama, navyo bila kusita wakachukua hatua.

Mbowe angekuwa na maono baada ya kucheza boko ya kumleta Lowasa ndan ya chama mwaka 2015 angejiuzuru kulinda heshima yake, au angeachana na tamaa yake ya kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti wa chadema ambao unamruhusu yeye kukalia kiti hicho kwa muda usiojulikana.

Na uamuzi wake huo ndio una mcost leo. Acha kusingizia polisi wao wanafanya kazi yao kwa mujibu wa sheria.
Hadithi hizo wapelekee channel ten,tbc na gazeti la uhuru/mzalendo ndio zinawavutia sana. Utalipwa t shirt na kofia zenye picha ya Bi Ushungi.
 
Uwezi kuwa huru kwa njia za kidiplomasia HV HV au kuchukua madarakani HV HV at yakobo alipambana kuweza kuchukua uzaliwa wa Kwanza kwa hujuma. Hvyo bila kiwafanyia hujumaa Haki aitapaikana
 
Shida siyo polisi, shida siyo CCM, shida siyo CHADEMA, shida siyo serikali wala siyo Katiba, shida ni sisi watanzania (Waafrika) hata leo tuletewe katiba mpya ya aina gani bado uzandiki wetu ni uleule...hata Mh Mbowe akiwa Rais leo bado uchafu ni uleule, hata Mh Samia aendelee kuwa rais uchafu ni uleule...Sisi waafrika ni viumbe wa ajabu sana, tuna ubinafsi, tuna chuki za ajabu, ni wenye tamaa, ni wezi, wala rushwa, upendeleo umetutawala, leo hii nchi hata iongozwe na CHADEMA, CUF, TLP, ADA-TADEA, ACT nk hakuna chochote tutapata viongozi wataendelea kujishibisha wao, ajira watapeana wao, watoto wao kwanza wataingia BoT, TANAPA, BANDARI, NSSF, BUNGENI, IKULU, TRA, na sehemu zote zenye mboga saba watatawala wao. Mnataka katiba mpya nawashangaa hakuna kipya kitatokea, mnao ikataa katiba Mpya nawashangaa pia hamna la maana la kutueleza. Mtanzania unayejitambua unaweza kuamua kuachana na upuuzi wa kufikiria ni jinsi gani taifa lako linaendeshwa, ukashika jembe ukalima maisha yatakuwa ya kadri....unavunjwa miguu eti unadai katiba mpya...ni ushenzi kama ushenzi mwingine maana hata iwe mpya haitakusaidi chochote bali wana siasa wataendelea kuneemeka.Mbowe, Zito, Msigwa, Mdude, Lisu nk wanahangaika ili wawe kwenye mfumo, wakisha ingia kwenye mfumo hizo kelele hutazisikia tena...wako wapi akina Esta Matiko, wakoa wapi akina Halima Mdee,(covid19) nk. Mbona hawadai katiba mpya kwa sasa, je unafikiri wangekuwa hawakupewa keki na akina Ndugai na Magufuli sasa hivi si na wao wangekuwa rumande kwa harakati za kudai Katiba Mpya? Ampherey Polepole sasa hivi anatembelea kwenye uzi mwembamba unaona yuko kinyume na serikali lakini sababu ni kwamba umeshatemwa na mfumo, je kipindi cha Magufuli hata usiku angeuita mchana ili mradi aendelee kula mema ya nchi. Mfano mzuri tukumbuke ya akina Lowassa (2015), kumbuka yule kijana Patrobas Katambi, kumbuka MWITa Waitara, kumbuka Vicent Mashinji, kumbuka Joshua Nassari, kumbuka Silinde, nk kuna watu walivunjwa miguu kwa sababu tu ya hao wazandiki niliotaja hapo juu, kuna watu wamewekwe rupango, kuna watu wameacha wajane na yatima kwa ajili ya Wapuuzi hao, kuna watu wamepoteza mwelekeo wa maisha kisa wanadai haki kwa kupitia migongo ya hao.....leo akina Mwita Waitara wanakula keki ya Taifa lakini waliowavujia damu na jasho wanawaona wapuuzi tuu. Vijana achaneni na siasa, shida sisi waafrika ni viumbe wa hovyo sana....mnaopoiga kelele leo mkipewa keki mnanyamaza....oooh kumbe hamdai haki bali ni njaa za Uafrika zinawasumbua...fanya kazi zako tafuta pesa utaishi kwa raha sana ukiyafikiria ya Serikali basi utaishia kuumia kila siku.
 
Back
Top Bottom