Nini kifanyike endapo nyumba yako imeshika moto usiku mkiwa ndani

Sikumbuki nilifungua channel ipi nikakuta mfanyakazi wa fire anatoa maelezo alipoulizwa kuhusu hizi nondo tunazoweka alisema kabla hujaweka hizo nondo unatakiwa ukawaone fire wakupe ushauri jinsi ya kuweka, alisema hawezi kuelezea pale kwa vile anayetakiwa kujua ni muhusika tu kwa usalama. Nadhani Kwa wawekaji nondo ingekuwa vizuri kuwaona fire kabla hujaanza maandalizi
 
Hivi si unaweza kuweka emergence door, tunawekeza kwenye mambo mengi tunasahau hata fire detectors
Katika madirisha yako ya grill unayopachika, dirisha moja au mawili liwe la kufunguka incase mnasepea dirishani, fundi mmoja alinishauri hivyo na mimi nimefanya hivyo
 
Katika madirisha yako ya grill unayopachika, dirisha moja au mawili liwe la kufunguka incase mnasepea dirishani, fundi mmoja alinishauri hivyo na mimi nimefanya hivyo
Hiyo kweli ni jambo la maana, umeongea jambo ambalo sikuwa nimefikiria you're a genius.
 
Siyo kwamba tunapenda, kwanza nondo zinaharibu show ya nyumba, ila sasa vibaka yani tunaweka nondo bado wanazikata sasa assume hakuna nondo si watageuza nyumba guest kabisa achilia mbali kukuibia
Ramani za nyumba nyingi zinaruhusu watu kuikimbia ajali ya moto yaani zina mlango wa mbele na wa nyuma tatizo ni aina gani ya lock ulzotumia kwenye milango hiyo Mimi ni fundi grill mzoefu huwa nawashauri wateja wangu milango Yao ya grill kuwa na na bati nusu nzima ya mlango halafu kwa ndani kunakuwa na makomeo yanayo funguka kwa urahisi,

vitasa vina tumika kufunga mnapokuwa mmeondoka nyumbani lakini usiku mnapoe da kulalala mnafunga makomeo ambayoehayatumii kufuli wala funguo kiasi kwamba hata mtoto anaweza kufungua,kikawaida ajali ya moto katika nyumba huwa inaanza eneo moja na kuambukiza maeneo mengine kwa hiyo ni wajibu wenu kujua ni mlango upi unaunafuu wa usalama muutumie kujiokoa.
 
Kitu kingine ni kuweka mlango wa dharura kwenye dirisha. Unaweka kamlango kadogo kwenye grili labda la chumba cha baba na mama na unalifunga na kakufuli kadogo ambako kakipigwa hata nyundo kanaachia.Watu wote wambiwe ikitokea dharura wakimbilie kwenye hicho chumba.
Huu ushauri mzuri. Ila jambo la muhimu naona tuache mazoea ya kuezeka na bati tuanzeni utamaduni wa kuweka zege hata kama mtu hataki kujenga ghorofa. Zege haishiki moto tofauti na paa la bati. Halafu watu wengi hawajui ukiweka zege unapata varanda ambayo unaweza kufanyia mambo mbali mbali kama kuanikia nguo kuweka bustani ya kupumzikia na sehemu ya kuchezea watoto.
 
Nenda kwenye maplastic unayoifadhia maji kajimwagie yote afu wakati moto unapambana kukausha maji uliyojimwagia we unapita kininja katikati ya moto
Hayo maji hayatasababisha "mvuke" mkali sana uungue kwa joto lake?
 
Hayo maji hayatasababisha "mvuke" mkali sana uungue kwa joto lake?
Sasa hapo itategemeana na distance ambayo utatembea ukiwa ndani ya moto

Kama kutakua na umbali kidogo kutoka sehemu yenye moto kwenda sehemu salama ni bora ukajifunika blanket zito uliloloanisha na maji wakati huo na wewe umejimwagia maji

Binafsi naona kwa mazingira hayo hiyo ndio njia pekee
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
pia tuondoe magril maana yakigusa moto yanachemka.
 
Kwenye majengo wenzetu unakutaga wametundika shoka kwenye korido.
Zile hazipo kwa bahati mbaya. Ni mahususi kwa ajili ya dharura kama moto. Hasa ni kwa kuvunjia milango.
 
unapojenga nyumba yako binafsi jaribu kuweka escaping root ya siri ambayo ni wewe, mkeo au yeyote mkubwa ndani ya nyumba ndio mtakuwa mnaijua...
Wenzetu wanakuwaga na vifaa kama shoka maeneo kama koridoni. Nikawa najiuliza ya kazi gani? Kumbe ni kwa ajili ya dharura kama hizo. Kuvunja milango, madirisha.
 
Huu ushauri mzuri. Ila jambo la muhimu naona tuache mazoea ya kuezeka na bati tuanzeni utamaduni wa kuweka zege hata kama mtu hataki kujenga ghorofa. Zege haishiki moto tofauti na paa la bati. Halafu watu wengi hawajui ukiweka zege unapata varanda ambayo unaweza kufanyia mambo mbali mbali kama kuanikia nguo kuweka bustani ya kupumzikia na sehemu ya kuchezea watoto.
Ila nyumba inakua haina muonekano mzuri kwa nje
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
Ujenzi wa siku hizi kama mtu atakutana na fundi bora wa hizi grilles atamshauri kitu,unachagua dirisha moja wanaweka kitu wenyewe wanaita “escape window”,ni kimlango ndani ya dirisha cha kutumia wakati wa hatari na huwa kinakuwa na kikomeo na hushauriwa zaidi kuwekwa mnapolala nyie wazazi ila familia nzima wajue funguo ya kufuli yake ilipo.
 
fire detector na smoke detector ni muhimu sana, inasaidia sana... alarm zikianza kulia angalau mnaweza kuanza kujiokoa..
hii ilisaidia sana kutuokoa na janga la moto shuleni,bweni letu liliwekewa smoke detector
 
Kubwa kuomba mungu atuepushe na majanga hayo. Moto unatokea wewe umelala unaamshwa na joto Kali. Kabla hujajua Nini ufanye Moto ushazingira sehem zote za kutoa unapagawa usielewe Nini Cha kufanya
 
Mungu mwenyezi mwingi wa rehma atuepushe na majanga kama haya na amfanyie wepesi majeruhi apone haraka na awape pumziko jema marehemu.[/QUOTE]

Aamin
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom