Nini kifanyike endapo nyumba yako imeshika moto usiku mkiwa ndani

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Jan 19, 2020
285
1,449
Habari wa jf.

Kuna jambo hapa naomba tushirikishane kwa wenye ufahamu, nimeona kwenye habari leo kwamba nyumba moja huko Mwanza imeungua moto. Na ndani yake kulikua na watu 7. Watu 6 kati yao walifariki on spot na mwingine kalazwa hospitali akiendelea na matibabu. Sababu za moto ni hitilafu ya umeme.

Habari zinasema kutoka kwa timu ya uokozi zinasema baada ya wale watu kugundua kuna moto, watano kati yao walikimbilia katika chumba kimoja nadhan kilichokua na nafuu, na moto ulipofika hapo pia, wakakosa option.

Sasa natafakari, hii ajali inaweza mpata mtu yeyote, nini cha kufanya ambacho mnadhani kinaweza saidia kuokoa maisha, ikiwa upo ndani ya nyumba iliyoshika moto.

Binafsi nnachojua ni kimoja tu, usije jaribu kufungua mlango ambao umefunga na funguo au makomeo maana hautafunguka so utakua unapoteza muda. Sababu ni vitu vyote vikishika moto hutanuka. So funguo, komea hata mlango wenyewe huwa vimetanuka sana. So ile kuhangaikia mlango ni bora kufanya kitu kingine tuu.

Halafu kwanini tunasisitizwa kuwa na fire extinguisher kwenye magari, kwenye fremu za biashara, lakini hatujawahi himizwa kuwa nazo majumbani. Hili nadhani ni muhimu pia kwa tahadhari, mtu kama unao uwezo, nunua hii kitu, then unakaa nayo tuu home

Uzi tayari
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebuleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni

Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
 
unapojenga nyumba yako binafsi jaribu kuweka escaping root ya siri ambayo ni wewe, mkeo au yeyote mkubwa ndani ya nyumba ndio mtakuwa mnaijua..

Jitahidi nyumbani kwako kuwa na fire extinguisher kubwa na medium na hakikisha watu wote kuanzia dada wa kazi na watoto wanajua namna ya kutumia, jitahidi kufanya fire drills nyumbani kwako na kuwatrain namna ya kutumia fure extinguisher.

Ukiwa uko vizuri funga fire suppression system ndani, joto likifika degree kadhaa vinafyatuka na kuanza kuuzima huku wazimamoto wanasubiriwa..

Kwa wale wenye madirisha yetu haya ya nondo au hizi grills, jitahidi ndani kuwe na hydraulic jack na ikitokea dharula piga jack dirisha okoa walio ndani kwenye hiyo njia..

Kama unaweza kujilinda na vibaka achana na hii minondo na machuma kwenye madirisha yako weka vioo tu kwenye dharula kinavunjwa tu, milango tuachane na hii mininga na mageti baadala yake tumieni MDF kwenye dharula teke moja unatoka nao tu..

Mungu mwenyezi mwingi wa rehma atuepushe na majanga kama haya na amfanyie wepesi majeruhi apone haraka na awape pumziko jema marehemu.
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
Labda huko posta au masaki ndio usiweke nondo, huku kitaa tunaweka nondo lakini bado wakushi wanazipitia na jeki.

Solution yako hii inaweza kuzuia moto kisha ikampa mwanya kibaka akashinda kiraisi kama simba kwenye mechi ya jana
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
Hizi grills hatuzipendi lakini tutafanyaje huku uswazi kulivyojaa vibaka! Ila huwa nashangaa hata nyumba za Masaki zimejaa grills.
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
Siyo kwamba tunapenda, kwanza nondo zinaharibu show ya nyumba, ila sasa vibaka yani tunaweka nondo bado wanazikata sasa assume hakuna nondo si watageuza nyumba guest kabisa achilia mbali kukuibia
 
Siyo kwamba tunapenda, kwanza nondo zinaharibu show ya nyumba, ila sasa vibaka yani tunaweka nondo bado wanazikata sasa assume hakuna nondo si watageuza nyumba guest kabisa achilia mbali kukuibia
Sasa hapa dawa ukijenga nyumba weka milango mitatu minimum. Na milango miwili itokee vyumbani. Maana kesi nyingi za moto, moto umeanzia sebuleni.
 
mimi nadhani badara ya kutafuta namna ya kujiokoa na moto, njia rahisi ni kuzuia kabisa mazingira ya moto kutokea.

mfano kuweka mitungi ya gesi mbali kabisa na maeneo hatarishi, nje au uwani na si ndani ya nyumba(makazi bora)

kuachana na mfumo wa wiring juu kwenye mapaa ya majengo(singbodi) , badara yake sasa nyaya zipitie ndani ya kuta na kutokea nje kabisa huko ndiko kuwe na main socket sio ndani,hii itafanya kukitokea moto udeal na nyaya tu mpaka ziishe si kuhamia kwenye mbao na paa kisha nyumba nzima.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom