Nini kifanyike endapo nyumba yako imeshika moto usiku mkiwa ndani

Mimi nadhani ni muoga sana, chumbani kwangu tuliacha nafasi ndogo ya mtu kupita tukaweka mlango usio na komeo na tukapaka rangi vizuri hata ukiwa nje huwezi jua kama pale ni mlango ambao likitokea lolote mtu anapiga teke unafunguka.

Vyumba vyote nimetoa funguo na nimewaambia watoto likitokea lolote wakimbilie chumbani kwangu.

Mwisho wa yote tusisahau Muomba Mungu atuepushe maana kama ilipangwa ufe kwa moto haijalishi umechukua tahadhari gani utakufa tu
 
Mbona sisi tuliopanga chumba na sebule, hatujapewa ushauri pale linapotokea janga la moto, maana ili utoke ni lazima mlango uko sebuleni, na wakati huo moto umeanzia sebuleni, maji nayo yako sebuleni ambako moto umeanza, kwa hiyo hata njia ya kuloweka ma blanket hapa imegoma, naona dalili za kifo tu iwapo moto utatokea kwa sisi wa chumba na sebule.
 
mimi nadhani badara ya kutafuta namna ya kujiokoa na moto, njia rahisi ni kuzuia kabisa mazingira ya moto kutokea.

mfano kuweka mitungi ya gesi mbali kabisa na maeneo hatarishi, nje au uwani na si ndani ya nyumba(makazi bora)

kuachana na mfumo wa wiring juu kwenye mapaa ya majengo(singbodi) , badara yake sasa nyaya zipitie ndani ya kuta na kutokea nje kabisa huko ndiko kuwe na main socket sio ndani,hii itafanya kukitokea moto udeal na nyaya tu mpaka ziishe si kuhamia kwenye mbao na paa kisha nyumba nzima.
wazo zuri!
 
Ikitokea moto na uko ndani ya nyumba chakufanya kama kuna ndoo za maji chukua mashuka mazito au blanketi chovya kwenye maji,halafu jifunike omba Mungu katisha kwenye moto!
Asante sana ila sasa shida Milango imefungwa na imeshatanuka haifunguki.
 
Katika njia zote za kujikinga na moto tuwe pia ndani kuwe na shoka zuri lililonolewa haswa ili kuwezesha kupasua Milango. Pia uwe na msemeno wa kukata vyuma mzuri ili ukishavunja mpango uwezesje kukata nondo za gate. Pia kama ukiwa nayo mingi utapitisha didishani ili jirani wasaidie kukata grills nje. Nyingine kama blankets kuwa nazo ili kusaidia kuloweka kwenye maji kunifunika wakati mnataka nje.
 
Mimi nadhani ni muoga sana, chumbani kwangu tuliacha nafasi ndogo ya mtu kupita tukaweka mlango usio na komeo na tukapaka rangi vizuri hata ukiwa nje huwezi jua kama pale ni mlango ambao likitokea lolote mtu anapiga teke unafunguka.

Vyumba vyote nimetoa funguo na nimewaambia watoto likitokea lolote wakimbilie chumbani kwangu.

Mwisho wa yote tusisahau Muomba Mungu atuepushe maana kama ilipangwa ufe kwa moto haijalishi umechukua tahadhari gani utakufa tu
Hii nayo nzuri. Ninaomba picha pm please nione mfano wake.
 
Kitu kingine ni kuweka mlango wa dharura kwenye dirisha. Unaweka kamlango kadogo kwenye grili labda la chumba cha baba na mama na unalifunga na kakufuli kadogo ambako kakipigwa hata nyundo kanaachia.Watu wote wambiwe ikitokea dharura wakimbilie kwenye hicho chumba.
Very good, hata nyumba yangu nina dirisha lenye dirisha mlango ndani yake. FUNDI wangu alinipa hiyo mbinu, nitaweka maandisha ya kuelekeza ijurikane mlango wa dharura ndani hapo. Maana kweli Mutungi ya gesi tunayo ndani ya Nyumba. nafikiri kutumia MKAA is best
 
Tatizo zile nondo kwenye madirisha. Nadhani ni muhimu nyumba iwe na milango mitatu. Moto ukianzia sebleni mnatokea milango mingine. Milango mingine isitokee sebleni.
Pia huu mfumo wa kuweka nondo madirishani inabidi tuache.
Maana ukitokea moto kutoka ni haiwezekani.
Kwa Tanzania na nchi zingine masikini ni vigumu kwasababu ya wizi unaosababishwa na umasikini
 
Hii imekaa poa angalau
mimi nadhani badara ya kutafuta namna ya kujiokoa na moto, njia rahisi ni kuzuia kabisa mazingira ya moto kutokea.

mfano kuweka mitungi ya gesi mbali kabisa na maeneo hatarishi, nje au uwani na si ndani ya nyumba(makazi bora)

kuachana na mfumo wa wiring juu kwenye mapaa ya majengo(singbodi) , badara yake sasa nyaya zipitie ndani ya kuta na kutokea nje kabisa huko ndiko kuwe na main socket sio ndani,hii itafanya kukitokea moto udeal na nyaya tu mpaka ziishe si kuhamia kwenye mbao na paa kisha nyumba nzima.
 
Nyumba kuwa na milango miwili huo ni usalama tosha, kutokuweka nondo kwenye madirisha ni kuhatarisha usalama wako pia
 
Nyumba kuwa na milango miwili huo ni usalama tosha, kutokuweka nondo kwenye madirisha ni kuhatarisha usalama wako pia
Mimi nimeweka milango mitatu. Mmoja ndio main door living room. Miwili ni emergency doors ambazo ndani huwezi kujua kama hii ni milango.
Hii miwili mmoja uko master bedroom kwa nje ni mlango unaonekana ila ndani nimeweka gysum board ikapigwa rangi kama ukuta mpaka uugonge ndio utajua ni board tu. Mwingine uko upande wa nyuma ya nyumba kutokea living room wa style hio hio. Dharula ikitokea napasua board tu naufungua natoka bila kupitia sehemu nyingine za nyumba.
 
Nenda kwenye maplastic unayoifadhia maji kajimwagie yote afu wakati moto unapambana kukausha maji uliyojimwagia we unapita kininja katikati ya moto
Umerahisha kama kumeza togwa. Moto unapowaka ndani kitu hatari hata kuliko moto wenyewe ni ule moshi na mvuke wa moto. Huo ndiyo huwaua wengi kabla hata moto haawaunguza.
 
Hapo ndo mtihani. Ila niliona nchi nilizokwenda ulaya madirisha hayana nondo. Ukifungua dirisha unatoka nje kirahisi kabisa.
Shida yetu bongo,ukiweka hivyo watu watozoea kupitia madirishani.

Si unakumbuka primary...mtu anajisikia tu kupitia dirishani hata kama yupo jirani na mlango.
 
Mimi nimeweka milango mitatu. Mmoja ndio main door living room. Miwili ni emergency doors ambazo ndani huwezi kujua kama hii ni milango.
Hii miwili mmoja uko master bedroom kwa nje ni mlango unaonekana ila ndani nimeweka gysum board ikapigwa rangi kama ukuta mpaka uugonge ndio utajua ni board tu. Mwingine uko upande wa nyuma ya nyumba kutokea living room wa style hio hio. Dharula ikitokea napasua board tu naufungua natoka bila kupitia sehemu nyingine za nyumba.
Mkuu hongera mno mno. Umefanya jambo la maana sana. Hili mimi huwa nawaambia watu mara nyingi. Unapojenga nyumba kuna vitu muhimu sana vya kuweka. Strong room (panic room) ya kujifungia unapovamiwa na wezi na escape root, ya kisiri unayoweza kutumia kama nyumba imeshika moto. Ni rahisi sana kuweka mlango ambao ni wewe na wana familia tu mtakuwa mnaujua na watu wengine wasijue pale kuna mlango. Mwazisha thread ameuliza mtu anatakiwa afanye nini moto unapowaka kwenye hizi nyumba zetu zilizosilibwa na nondo kila mahali? Jibu sahihi nadhani itakuwa ni too late! Hili swali unatakiwa ujiulize wakati wa kujenga.
 
Hizi grills hatuzipendi lakini tutafanyaje huku uswazi kulivyojaa vibaka! Ila huwa nashangaa hata nyumba za Masaki zimejaa grills.
Bongo grills zimeshakuwa kama fasion. Ni kama ''maua'' ya kupendezesha nyumba. Lakini hata hizo grill bado mtu unaweza kuweka baadhi ya madirisha zikawa rahisi kufungua kwa ndani. Badala ya kuchomelea madirisha yote grill zishikane na frame ya dirisha ukaacha eg dirisha moja kwa nje likaonekana kama limechomewa ila kwa ndani unaweza kufungua kama mlango.
 
1 of the best thread ,
Habari wa jf.

Kuna jambo hapa naomba tushirikishane kwa wenye ufahamu, nimeona kwenye habari leo kwamba nyumba moja huko Mwanza imeungua moto. Na ndani yake kulikua na watu 7. Watu 6 kati yao walifariki on spot na mwingine kalazwa hospitali akiendelea na matibabu. Sababu za moto ni hitilafu ya umeme.

Habari zinasema kutoka kwa timu ya uokozi zinasema baada ya wale watu kugundua kuna moto, watano kati yao walikimbilia katika chumba kimoja nadhan kilichokua na nafuu, na moto ulipofika hapo pia, wakakosa option.

Sasa natafakari, hii ajali inaweza mpata mtu yeyote, nini cha kufanya ambacho mnadhani kinaweza saidia kuokoa maisha, ikiwa upo ndani ya nyumba iliyoshika moto.

Binafsi nnachojua ni kimoja tuu, usije jaribu kufungua mlango ambao umefunga na funguo au makomeo maana hautafunguka so utakua unapoteza muda. Sababu ni vitu vyote vikishika moto hutanuka. So funguo, komea hata mlango wenyewe huwa vimetanuka sana. So ile kuhangaikia mlango ni bora kufanya kitu kingine tuu.

Halafu kwanini tunasisitizwa kuwa na fire extinguisher kwenye magari, kwenye fremu za biashara, lakini hatujawahi himizwa kuwa nazo majumbani. Hili nadhani ni muhimu pia kwa tahadhari, mtu kama unao uwezo, nunua hii kitu, then unakaa nayo tuu home.

Uzi tayari
 
Usiseme hamjasisitizwa, Watanzania mnaishi kwa kukariri na kufuata historia, Taasisi mojawapo inayojukumu hilo ni Jeshi la zimamoto na uokoaji, hiki chombo mnakiona cha hovyo na mnakidharau, Iko hivi mnapowaona hawa watu watoapo elimu msiiibeze na muwe makini kusikiliza elimu hio kwani haibagui wapi kwa kuitumia, All in all portable fire extinguisher ni muhimu sana kwa moto wa awali. Suala la milango kizimamoto inashauriwa mlango wa kutokea ufungukie pande zote nje na ndani. Je hili mwitikio wake ukoje kwa mtu anayejenga jengo jipya, ? Kuna mengi sana ila kama hutojali tufungue uzi wa kupeana abcd kuhusu elimu ya motto
 
Nenda kwenye maplastic unayoifadhia maji kajimwagie yote afu wakati moto unapambana kukausha maji uliyojimwagia we unapita kininja katikati ya moto
Ina itwa cooling process japo hujaiweka sawa but husev pia ila sio full decay mzee hapo ni kuanzia stage 1,2 na 3
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom