MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Mkuu usemayo ni kweli, lakini je hao wapinzani wenyewe mbona hawana umoja, kila mmoja anacheza kivyake... unategemea nini? Nilitegemea wao wangekuwa wamoja ki harakati katika kuwaelimisha wananchi haswa kule vijijini, lakini nao hawaonekani mpaka karibia na uchaguzi.Mwanafalsafa1
Mbona unakwepa sababu moja muhimu ambayo inafanya upinzani usishinde Tanzania? Tutaikwepa hii sababu mpaka lini? Angalia yaliyotokea Kenya 2007 na sasa wanavyojizatiti kuiondoa sababu hiyo: Tume ya Uchaguzi. As long as tume ya uchaguzi inaundwa na serikali ya CCM, as long as UWT wanaruhusiwa kuingilia zoezi la kuhesabu kura, as long as polisi wote wanakuwa CCM na madiwani kutishiwa kuwa maeneo yao yakipoteza kura wamepoteza kazi upinzani hauwezi kushinda katu. Tusisahau hilo. Unadhani kwa nini Mkwere kawatishia wafanyikazi kwamba he can win without their votes? Kwa sababu anajua kuwa CCM ni hodari ku manufacture kura.
X-Paster,Mkuu usemayo ni kweli, lakini je hao wapinzani wenyewe mbona hawana umoja, kila mmoja anacheza kivyake... unategemea nini? Nilitegemea wao wangekuwa wamoja ki harakati katika kuwaelimisha wananchi haswa kule vijijini, lakini nao hawaonekani mpaka karibia na uchaguzi.
Lakini mkuu mbona watu kama kina Mrema wanajulikana, hii ngoja ngoja mpaka lini... ni miaka ishirini na zaidi sasa tangia vyama vya upinzani vikubaliwe kikatiba... wanacho subiri ni kitu gani...!?X-Paster,
Hilo la umoja ni muhimu. Hata Kenya walifanikiwa hatimaye kukiondoa KANU mamlakani kwa umoja. Lakini utaunganaje na mtu kama Mrema?
Ngoja akina Mrema wajitokeze uhalisia wao, wale wapinzani halisi walio na uchungu wa nchi watadhihirika. Bado tuna mwendo mrefu mbele, lakini naamini hatimaye tutafika tu.
Mwanafalsafa1
Mbona unakwepa sababu moja muhimu ambayo inafanya upinzani usishinde Tanzania? Tutaikwepa hii sababu mpaka lini? Angalia yaliyotokea Kenya 2007 na sasa wanavyojizatiti kuiondoa sababu hiyo: Tume ya Uchaguzi. As long as tume ya uchaguzi inaundwa na serikali ya CCM, as long as UWT wanaruhusiwa kuingilia zoezi la kuhesabu kura, as long as polisi wote wanakuwa CCM na madiwani kutishiwa kuwa maeneo yao yakipoteza kura wamepoteza kazi upinzani hauwezi kushinda katu. Tusisahau hilo. Unadhani kwa nini Mkwere kawatishia wafanyikazi kwamba he can win without their votes? Kwa sababu anajua kuwa CCM ni hodari ku manufacture kura.
2. Kabla ya kuruhusu vyama vya upinzania, CCM, chama kilicho kuwa madarakani kilikua na muda wa kujiandaa. Katiba ya kuruhusu vyama vya upinzani iliandikwa na wao na muda wa kujiandaa na mabadiliko wa mazingira ya kisiasa walikuwa nao.
Upinzani haushindi kwa sababu Tanzania hamna upinzani wa kweli. Watanzania wengi wana jiuliza kwa nini mpaka leo hii miaka karibia ishirini tokea uingie mfumo wa vyama vingi bado vyama vya upinzani havifui dafu kwa CCM. Ni kwa sababu ya mazingira ambao yaliambatana na kuanzishwa kwa vyama hivi. Ni vigumu kwa vyama hivi kuondokana na mzigo wa historia ya uanzishwaji wao. Nita fafanua mtazamo wangu.
1. CCM ndiyo kilikua chama pekee Tanzania kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo CCM ilikua na muda zaidi wa kujijenga kiuongozi, kirasilimali na kiumaarufu. Watanzania wengi hawana vyanzo vya kuaminika na vya haraka vya kupata habari kama wengi wetu humu JF. Kwa hiyo bado kuna Watanzania wengi (amini usiamini) wanaishi "jana".
2. Kabla ya kuruhusu vyama vya upinzania, CCM, chama kilicho kuwa madarakani kilikua na muda wa kujiandaa. Katiba ya kuruhusu vyama vya upinzani iliandikwa na wao na muda wa kujiandaa na mabadiliko wa mazingira ya kisiasa walikuwa nao.
3. "Personalities" nyingi zilizo unda vyama vya upinzani ni wana CCM wa zamani. Ukimuangalia Mrema Sharif Hamad, Mtei wote ni watu waliokua ndani ya mfumo wa CCM. Hata Ibrahim Lipumba ambae sina uhakika kama alikua CCM au la alikua mshauri wa Mwinyi kipindi fulani. Je hii ina wezaje kuwa tatizo kwa vyama vya upinzani?
a) Baadhi ya viongozi waliongia upinzani ina wezekana walikua mamluki ambao walikua hawana mpango wowote wa upinzani wa kweli.
B) Baadhi ya viongozi walioingia upinzani ni watu ambao walikua hawana future CCM kwa hiyo walihama kwa ajili ya kujaribu bahati yao. Hiyo ni kusema upinzani ilipokea watu ambao hawakua nyota wa kisiasa bali "has beens" wa CCM.
c) Baadhi yao ni watu waliyo ondoka CCM kwa maana hiyo mfumo wa fikira ulikua huo huo. Hauwezi kumshinda mwalimu kwa kumpa mtihani wake mwenyewe.
4. Wengi wa viongozi waliounda vyama vya upinzani kwa sababu moja au nyingine ita kuwa wali fikiria kwamba CCM ita shindika kiurahisi. SI ajabu baadhi yao wakadhani kwamba 1995 wange kiondoa CCM madarakani. Kwa maana hiyo basi vyama hivi vya upinzani vilivyo anzishwa vilikua havina mipango ya muda wa kati au mrefu kwa maumaini kwamba uchaguzi una kuja na wao wata shindda. Mpaka leo hii sioni mipango ya kueleweka ya muda mrefu wa chama chochote cha upinzani.
Kwa hiyo basi kama vyama vya upinzani kweli vina taka kushinda basi ni lazima kuwepo na mabadiliko. Lazima waletwe vijana ambao watakua katika mfumo wa vyama vyao. Lazima walete watu ambao hawaku wahi kuhusika na CCM ili kuleta mawazo na fikira tofauti. Ni lazima waji tazame na wajiunde upya. Kusema ukweli sioni chama cha upinzani kati ya hivi vilivyopo sasa kufanya mabadiliko yoyote ya kisiasa labda vyama vipya vita kapo anzishwa au viongozi wa sasa waliotoka kwenye mfumo ule ule, mawazo yale yale na mafunzo yale yale wakija kuondoka.
Ndugu wana JF tuna muda mrefu bado mpaka upinzani wa kweli Tanzania uibuke. Leo hii hatuna wapinzani bali wasindikizaji. Kwa maana kila kabla ya uchaguzi tayari imesha julikana chama gani kita shinda uraisi na chama gani kita kuwa na wabunge wengi Bungeni. Huo si upinzani.
Sababu nyingi zilizotolewa ni kweli lakini kuna jambo lingine. Vijana. Chama chochote au movement yoyote ya kuleta mabadiliko lazima ichochewe (siyo lazima iongozwe) na vijana wa wakati huo. Vijana wa Tanzania hawana tofauti na wazazi wao. Ni vigumu kuwa-animate kwa issue yoyote. Kwao mambo ni "shwari', 'hamna noma', 'fresh' hata kama hana uwezo wa kupata chips dume. Hiyo mindset inawafanya waridhike kwa mambao madogo na kukosa thubutu. Siyo katika siasa tu bali na katika nyanja zingine za kimaisha. Ukitaka mabadiliko lazima ukubali na kuonja joto ya jiwe.Lakini mkuu mbona watu kama kina Mrema wanajulikana, hii ngoja ngoja mpaka lini... ni miaka ishirini na zaidi sasa tangia vyama vya upinzani vikubaliwe kikatiba... wanacho subiri ni kitu gani...!?
Waache kuuza sura bana.
mkuu tupo pamoja, pamoja na lawama zote tunazo wapa CCM lakini hata huku wapinzani bado kuna kitu tuna miss kuwashawishi wananchi kuwa wapo imarakitu kikubwa walichokosea ni kutojenga msingi imara wa wanachaama waaminifu,vyama vingi vya upinzani vipo mjini tu,walitakiwa wajikita katika kutafuta wanachama kwanza kabla ya kuaanza ulafi wa madaraka na ubinafsi uluowjaa.
ukiangalia mfano CCJ, kimeanza hivi karibu kinataka kusajiriwa, kinapita mitaani kutafuta wananchama kwa nguvu, hapo lazima upate mamluki wengi na wanachama wasiona sifa thabithi na mawazo chanya ya mabadiliko.
Sababu nyingi zilizotolewa ni kweli lakini kuna jambo lingine. Vijana. Chama chochote au movement yoyote ya kuleta mabadiliko lazima ichochewe (siyo lazima iongozwe) na vijana wa wakati huo. Vijana wa Tanzania hawana tofauti na wazazi wao. Ni vigumu kuwa-animate kwa issue yoyote. Kwao mambo ni "shwari', 'hamna noma', 'fresh' hata kama hana uwezo wa kupata chips dume. Hiyo mindset inawafanya waridhike kwa mambao madogo na kukosa thubutu. Siyo katika siasa tu bali na katika nyanja zingine za kimaisha. Ukitaka mabadiliko lazima ukubali na kuonja joto ya jiwe.
Si kweli huo mlolongo ulioandikwa na Mwanafalsafa1 aidha inawezekana ni kuanza harakati za kuchomekea ili ionekane CCM bado ni strong ina nguvu na hili na lile, nasema nikutaka kuwajaza watu kasumba.
Kwa ufupi sikubaliani na hayo kwa upande wangu na kwa vile sio lazima kuyakubali najiona nipo huru kuchangia vile nionavyo au nikionacho.
Watu au viongozi wa upinzani kuwa walikuwepo ndani ya Chama Cha CCM ,kwa maana kuhusika au kutohusika na CCM ,sio sababu ya kukosekana viongozi shupavu.Vyama vya siasa vyaa upinzani naamini kabisa vina viongozi na uongozi shupavu tena ulioimara.Na siamini kabisa kuwa CCM inashinda uchaguzi kwa kishindo cha kuzoa kila kitu na kugawia pale kinapotaka.
Vyama vyetu bado vipo katika transit period ambacho kinatumika kuweka misingi mbalimbali itakayowawezesha kuimarisha mfumo wa kuwepo kwa vyama vingi vinavyotumia katiba mpya,kwa maana tatizo moja tulilokuwa nalo ni kukosekana kwa KATIBA inayojitosheleza katika kuongoza nchi yenye vyama vingi.
Vyama hivi vinahitaji muelekeo wa kuibadilisha KATIBA ya NCHI hii na sio kulipua mabomu ya ufisadi kwani yaliolipuliwa yote naona yamedumaa.Imani yangu CCM haijawahi kushinda uchaguzi hata mara moja ,kwa maana ya ngazi tofauti mpaka ya Uraisi kwani matokeo wanayotangaza yana utata na kwa ufupi ni ya uongo ,ni viongozi wangapi wamekosa kura hata moja ,kwa maana hata kura yake mtu haioni ,afu unanambia CCM inashinda uchaguzi.
Tujaribuni kuwa wa kweli jamani,tuache hypocrisy...Tatizo ni UDINI na CCM....Tanzanians are fed-up with CCM..ila watu wanaangalia wapi dini yao itapata maslahi kwanza..na hii ni kwa sababu watu wanaendesha maisha yao chini ya vivuli vya dini zao...taasisi za dini ndio source za kuendesha life.
Kila kipindi cha Urais....kuna kundi moja la dini linafurahia wakati lingine linahuzunika..kwa hiyo kuipenda au kutoipenda CCM inategemea na interest ya mtu.
Nina uhakika kwamba wakristo wengi hawapendi CUF kwa sababu ya labda viongozi wake wengi ni muslims ama wafuasi wake wengi ni muslims,the same applies to muslims....hawaikubali sana CHADEMA ama wasingeikubali sana CCJ based on the same reasons.
Angalia CUF zenji,kwa sababu hakuna mgawanyiko wa fikra za dini,utaona CUF kila uchaguzi inashinda,na wengi hulalamika kuwa mkono wa udini wa bara ndio unaowanyima ushindi wao kwa nguvu za dola.Almuhimu ni kuwa vuguvugu la kisiasa Zenji liko makini kuliko bara.
CCM wanajua hii hali,na ndio maana wanaweza kuzinchanga karata zao vizuri,mtaona sasa hivi unafiki utakavyojidhirisha hata kwa hao viongozi wa dini....ni maslahi tu.
Vyama vya upinzani wanajitahidi sana hata kama si vyote, tatizo ni ninyi mnaojua ikweli lakini njaa inawasumbua kiasi kwamba hamwezi kuzungumzia ukweli huo mbele ya umma, zaidi ya kupamba CCM kwa maneno ya ajabu ajabu. Kuna maeneo CCM huiba sana au hutisha watu kwa vitisho vingi lakini hamtaki kuzungumzia hilo. Kwanini kuivumilia CCM? wakati wameboronga katika mambo mengi. Wabunge wa chache wa upinzani mchango wao ni mkubwa kuliko lunduko kubwa la wabunge toka CCM, wafanye nini ili watu waone mchango wao ? Mabadiliko ya kweli hayaletwe na chama au viongozi ila huletwa na wananchi wenyewe waliochoshwa na taabu ya chama tawala.
Kuna vijana wasiotambua nchi inaenda wapi chini ya CCM badala ya kushiriki kuleta mabadiliko wanajihangaisha kumchangia JK aliyedhihirisha kushindwa kuleta maendeleo ndani ya miaka miatano. Nafikiri si muda wa kulaumu vyama vya upinzani, ila ni muda muafaka wakujiuliza nimetoa mchango gani kwa vyama makini ilikuleta mabadiliko. Unafiki tuweke kando, tuchukue hatua ya kuiambia CCM wazi wazi kuwa imeshindwa na tuwaambie viongozi wa vyama vya upinzani kuwa tuko tayari kuungana nao kuleta mabadiliko katika nchi hii.
Binafsi naamini nina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi hii. Akili yangu haijaharibiwa na CCM hata kidogo, niko tayari kutoa maisha yangu kwa kusimamia ukweli. Si muda wa kuiogopa CCM as if it is God,