Nini hatima ya Halima Mdee na wenzake baada ya bunge kuvunjwa?

Nini hatima ya Halima Mdee na wenzake baada ya bunge kuvunjwa?

Hiyo imani sijui anaitoa wapi kwa Hawa viongozi. Hao akina Mdee si ndio tulikuwa tunawaona Makamanda wa hatari, lakini wakafanya Mambo ya ajabu? Nimempa mfano wa Lowassa, alipokelewa na viongozi wachache na akapitishwa kugombea urais akiwa na wiki chache ndani ya chama. Je Lowassa alipokelewa bila viongozi kadhaa kupewa hela?

Kwa Sasa Lisu anapiga kelele kuwa kuna fedha chafu kwenye uchaguzi ndani ya chama, ni kundi gani limeshika hizo fedha chafu? Katika mazingira ya pesa chafu, anatoa wapi nguvu ya kutoa mishipa ya shingo?
Kama huyo Lowassa alipokelewa baada ya viongozi fulani wa chadema kupewa hela Serikali iliyoundwa na CCM ilikuwa wapi kutumia Takukuru kuwakamata hao viongozi waliokiuka sheria za uchaguzi makusudi?Kwanza kufanya hivyo kungesaidia kudhoofisha harakati za uchaguzi wa 2015 ambao CCM waliona kila rangi
 
Kama huyo Lowassa alipokelewa baada ya viongozi fulani wa chadema kupewa hela Serikali iliyoundwa na CCM ilikuwa wapi kutumia Takukuru kuwakamata hao viongozi waliokiuka sheria za uchaguzi makusudi?Kwanza kufanya hivyo kungesaidia kudhoofisha harakati za uchaguzi wa 2015 ambao CCM waliona kila rangi
Takukuru ni baadhi ya taasisi za umma zenye uwezo mdogo wa kufanya Kazi Yao.
 
Sijaja hapa kuwasema viongozi wa Chadema, mimi nimeandika ukweli ulio wazi kwetu sisi sote.
Hakuna kikao chochote cha Chadema kilichowahi kukaa ili kubariki harakati haramu za kina mdee wala hakuna kiongozi yoyote wa Chadema aliyewahi kusimamia kuwaunga mkono wale malaya ya kisiasa wa Covid 19.
Kama wewe unajua tofauti na hapo njoo hapa useme ili tujue.
Sasa usicho elewa ni nini, kwamba hakuna anayezungumzia vikao hapa, au akili zimekuruka kichwani? Wewe huna uwezo wa kumsemea kila kiongozi wa CHADEMA, uhakika huo unautoa wapi?
 
Natetea ukweli uliowekwa wazi (Facts) kwetu sote na sio porojo, propaganda na ujinga wa kutengenezwa gizani.
Sasa ndio unazidi kujichanganya kabisa. Inaonekana hata unachokitetea hukijui. Wewe hupo CHADEMA, maswala yao ya ndani, hasa kwenye uongozi wao utayajuaje, hadi uyaite "facts"?

Hata sikushauri ukachukue kadi yao, maanake hata bila kadi umekuwa shabiki asiye ambilka kabisa, ukiwa na kadi sijui itakuwaje?
Yaani unataka sisi hapa JF tuamini kuwa, uwepo wa covid 19 mpaka sasa ni matokeo ya ushawishi na nguvu ya kigogo fulani ndani ya Chadema. Sasa sisi tumekuuliza how? Who? Why? Bado huna majibu.
Nionyeshe niliposema haya maneno, "kuwepo COVID ni matokeo ya USHAWISHI NA NGUVU YA KIGOGO" ndani ya CHADEMA? Kumbe unasoma halafu unajibu usichoelewa?
 
Suala la Lissu liko wazi, amesema kuna pesa zimeingizwa na CCM ili kuvuruga chaguzi ndani ya Chadema. Full stop.
Sasa angalia 'contradictions' hizi unazoziongeza kwenye 'facts' zako. Hivi huoni unavyojichanganya mwenyewe?
Hao viongozi wanaoruhusu kuingizwa pesa haramu kuvuruga chaguzi za ndani ya chama, wana tofauti gani na wale ambao wanaweza kuwa walishiriki katika maswala ya akina Mdee?
Hizi 'fact' zako ni 'fallacy.'
 
Ni kweli kabisa mkuu, pesa na madaraka ndio vilitumika kuhamisha wanacdm wengi kwenda kuunga juhudi. Linapokuja suala la fedha huwezi kumuani mwanasiasa yoyote.
Na mimi watu wa aina hii nasita sana kuwaita "wanasiasa". Hili neno hapa kwetu tumelipa maana mbovu kabisa. Wachumia tumbo sasa ndio tunaowaita wanasiasa., kwa vile tu wapo kwenye vyama vya siasa! Hiyo ndiyo sifa pekee inayowapa cheo hicho kiharamu.
 
Wadau nawasabahi.

Uchaguzi ndio huo unakaribia. CHADEMA wameshinda pambano lao dhidi ya Halima Mdee na kundi lake kwa kuishawishi Mahakama Kuu kuthibitisha uhalali wao wa kuwafukuza Halima Mdee na kundi lake uanachama.

Pia, CHADEMA wametekeleza wajibu wa kikatiba kulijulisha Bunge na Tume ya Uchaguzi kuwa Halima Mdee na kundi lake sio wanachama wao kikatiba, hivyo hawastahili kuwa bungeni. Lakini bunge, serikali, na tume ya uchaguzi kwa pamoja wameamua kuvunja katiba kwa makusudi kwa kuendelea kuwalipa mishahara na posho kinyume na sheria kwa mujibu wa katiba. Kwani katiba inasema moja ya sababu za mbunge kupoteza ubunge wake ni "kufukuzwa uanachama na chama chake".

Hakika, bunge letu limeweka historia ya kuwa "Bunge lenye wabunge wasio na chama".
Najiuliza, nini hatima ya Halima Mdee na kundi lake baada ya bunge kuvunjwa?
Je, watajiunga na CCM?
Je, watajiunga na vyama vingine ila sio CHADEMA?
Je, CCM itawateua kama wabunge wa viti maalum?
Au watastaafu siasa?

Ngoja tusubiri 2025.
Sijui kama Mbowe ataweza kumtimua Mdee mazima kwenye chama, labda Lissu ndiyo akaze. Vinginevyo, Bunge likiisha wanarudi kwenye ukamanda.

Ova
 
Kwanza achana nao want ukwasi wa hali ya juu,na wanapatam M 350.Halima alishakuwa ccm zamaaani na atapita ubunge na atakuwa naibu waziri na baadhi ya wenzake.
Kwani ccm watarudi madarakani tena ?
 
Sijui kama Mbowe ataweza kumtimua Mdee mazima kwenye chama, labda Lissu ndiyo akaze. Vinginevyo, Bunge likiisha wanarudi kwenye ukamanda.

Ova
Akili za kuvukia bara bara naona umezileta hapa JF.
Watu wote tunajua, Madee na wake malaya wengine ukurasa wao ndani ya Chadema ulishafutwa, kuchanwa na kuchomwa moto, hata kuwazungumzia haiwezekani tena. Sasa wewe unaleta hadithi gani?
 
Akili za kuvukia bara bara naona umezileta hapa JF.
Watu wote tunajua, Madee na wake malaya wengine ukurasa wao ndani ya Chadema ulishafutwa, kuchanwa na kuchomwa moto, hata kuwazungumzia haiwezekani tena. Sasa wewe unaleta hadithi gani?
Wakati ni shahidi mzuri. Tubaki kimya, tusubiri wakati.

Ova
 
Sasa angalia 'contradictions' hizi unazoziongeza kwenye 'facts' zako. Hivi huoni unavyojichanganya mwenyewe?
Hao viongozi wanaoruhusu kuingizwa pesa haramu kuvuruga chaguzi za ndani ya chama, wana tofauti gani na wale ambao wanaweza kuwa walishiriki katika maswala ya akina Mdee?
Hizi 'fact' zako ni 'fallacy.'
Ndugu kichwani uko timamu?
Mbona unalazimisha porojo za kutungwa za kina mdee kuwa agenda ndani ya Chadema?
 
Wakati ni shahidi mzuri. Tubaki kimya, tusubiri wakati.

Ova
Hapa umejibu vyema.
Siongezi neno.
Hakuna sababu ya kulazimisha tuamini jambo la kipuuzi la kufikirika wakati muda unatosha kulifanya linyewe lijionyeshe.
 
Nimecheka kwa nguvu, nani hapa anawatetea akina Mdee?! Ninachosema viongozi wa cdm hasa mwenyekiti hawana uadilifu huo. Usishangae hao akina Mdee wakapokelewa chamani kwa utetezi kama ule wa Lowassa. Lowassa hakuwa na nguvu usemayo Bali alikuwa na hela, kama alikuwa na nguvu hiyo angeenda TLP hiyo nguvu yake ikaonekane.
Agenda yako ni nini hapa?
Hoja yako ni ipi hapa?
Kwanini unalazimisha fikra zako potofu tuziamini?
Haya mwenyekiti wa Chadema hana uaminifu, kwa hiyo wakina Mdee watarudi Chadema? Una akili sawa sawa?
 
hakika leo unatafuta ugomvi nami usiokuwa na sababu. Umeona wapi nilipoandika kwamba kulikuwa na vikao ndani ya chama kuhalilisha hao wabunge waingie bungeni?
Haya siyo maneno yako ya kujitungia tu mwenyewe?
Huna hoja, unakomalia vitu visivyo na msingi! Umeshindwa kujibu hoja unahamia kwenye ugomvi! Ni ngumu sana kuwatetea Covid 19 na bado ukaonekana una akili timamu!
 
Wataenda CCM, ACT na NCCR.
Wengine watakuwa wakuu wa mikoa, wilaya na ma DED.
 
Magufuli amehitimisha political career ya Mdee na Bulaya kirahisi sana
Bulaya atarejea ccm, Kishoa, Nusrat na Matiko atahamia ccm.

Tunza Malapo atahamia ACT, Conchester Rwamlaza, na yule wa Rungwe watarejea CDM, yule Anatropia na yule wa Shinyanga watahamia ACT.

Tuupe muda nafasi.
 
Back
Top Bottom