Unachokijua wewe mwanachama wa CHADEMA siyo lazima ndiyo iwe 'fact' ya watu wengine kuichukulia kuwa kweli. Wewe umepofushwa na mahaba juu ya chama chako kiasi kwamba fikra zako hazikuruhusu tena kuona tofauti na wanayoona wengine.
Sikiliza, sisi wengine tunaandika haya hapa, siyo kwamba hatuwatakii mema CHADEMA, hata kama siyo wanachama wa chama hicho. Tunapenda sana, hata kesho, CHADEMA ingeweza kuwaondoa CCM, tutawashangilia.
Kinachotukatisha tamaa, ni watu wa aina yako mliolewa kabisa damu ya chama kiasi kwamba kuhoji chochote juu ya matendo ya baadhi ya viongozi wenu, mnatufanya tuwe maadui. Nyinyi ndio maadui wenyewe, siyo wa chama chenu tu, bali wa taifa hili.
Mnafanya kazi tuliyotegemea mngeweza kuifanya ionekane kuwa haiwezekani. Rudi nyuma kidogo, tulizana. Viongozi wenu siyo malaika. Wahojini ili muweze kuwa na uhakika, na kuwa na hizo 'facts' unazozizungumzia hapa. Kuwahoji viongozi siyo dhambi.