Vuta subira mkuu, hakuna lisilowezekana; wakati utakapofika historia itajinyoosha yenyewe.You really believe that? Ulielewa jinsi vitisho vya Magufuli vilivyokuwa enzi zile? Jinsi vilivyobadili mazingira ya kisiasa ndani na nje ya CCM na kuuweka mustakabali mzima wa taifa mikononi mwa mtu mmoja?
Halafu hiyo “consultation ndani ya chama” ilikuwa na uzito gani kuzidi vitisho vya Magufuli na manufaa ya aina gani kiasi cha kuwa na ushawishi kwa kina Halima kutupilia mbali legacy na hatma zao za kisiasa?
Unajua, hata Lowassa kwenda CHADEMA stori hiyo hadi leo ina utata; sasa hii ya hawa mabinti unadhani kila kitu kitafunuliwa ili kukuridhisha tu udadisi wako?
Ni mambo gani mengine yanayotokea ndani ya chama, hata kule CCM lakini watu hawajui lolote juu yake.