Nini hatima ya Halima Mdee na wenzake baada ya bunge kuvunjwa?

Nini hatima ya Halima Mdee na wenzake baada ya bunge kuvunjwa?

M
Unaweza kunipa 'fact' yoyote unayodhani nimekaririshwa? Kwa sababu umekwishadai wewe ni mtu wa 'facts'.
Mimi nimeshasema, dhana ya kudai kuwa wabunge wa Covid 19 wako mpaka leo bungeni kwa sababu ya kubebwa na kigogo fulani wa CHADEMA mbali na kukosa ushahidi wowote (hata wa kimazingira) haijawahi kuwa na mantiki yoyote tangu ilipoanza kusemwa mpaka leo. Yoyote yule anayeibuka na kusema hilo, tukimwambia embu tupe facts katika hilo anaishia kusema wewe amini tu iko hivyo.
Hata wewe hapa, umeshindwa kuitetea, imebakia kukaririsha fikra zile zile za wale wale.
 
Halima Mdee anapotential ya kufanya nini?
Mtu mwenye real potential anawezaje kung'ang'ania ubunge wa viti maalum vya mchongo wa umalaya wa kisiasa?

Yes ila katika kufanya intellectual analysis lazima utazame uwezo wa MTU mmoja mmoja she is weak but she is smart too
 
Mkuu 'Erythro', umesikia nikilihoji hili leo? Miaka yote umenisoma humu, uliwahi kusikia nikisema popote kuwa hao wabunge walibarikiwa na CHADEMA?
Nionyeshe sehemu yoyote ndani ya JF nilipowahi kusema CHADEMA ilibariki jambo hilo!
Sasa huyo Kiongozi wa Chadema aliyewatoa wafungwa na kuwapeleka kuapishwa ni nani na ana nguvu gani za kuvunja katiba ya nchi kiasi hiki?
 
Nyuma ya pazia la wapi?
Magufuli alikuwa anaweza kuweka mapazia pale Chadema?
Mtu aliyekuwa anataka kuiua Chadema na viongozi wake, ana muda wa kuweka weka mapazia?

Tuonyeshe sasa hayo mapazia ili tukuelewe?
Tunajua wapi ushenzi wa magu ulipoanzia na kuishia, na wapi mwenyekiti wa cdm alitoa baraka zake. Subiri tu kidogo utaona Nini kinaendelea na utetezi wa kina Mdee kwenye cdm.
 
Yes ila katika kufanya intellectual analysis lazima utazame uwezo wa MTU mmoja mmoja she is weak but she is smart too
Halima is smart to what?
Smart person always protects his/her legacy in each step. Halima alishapoteza legacy yake (trust&resist), Halima amenunulika kirahisi mnoo. Ukishakuwa msaliti huwezi tena kuwa trusted na huwezi tena kuwa stable.
 
M
Mimi nimeshasema, dhana ya kudai kuwa wabunge wa Covid 19 wako mpaka leo bungeni kwa sababu ya kubebwa na kigogo fulani wa CHADEMA mbali na kukosa ushahidi wowote (hata wa kimazingira) haijawahi kuwa na mantiki yoyote tangu ilipoanza kusemwa mpaka leo. Yoyote yule anayeibuka na kusema hilo, tukimwambia embu tupe facts katika hilo anaishia kusema wewe amini tu iko hivyo.
Hata wewe hapa, umeshindwa kuitetea, imebakia kukaririsha fikra zile zile za wale wale.
Utofauti wangu na wewe, naona upo katika kumbukumbu. Ninaposoma mawazo ya mtu najaribu kujikumbusha nilivyowahi kumsoma mtu huyo huko siku za nyuma, historia yake ipoje. Sirukii tu na kudai mtu 'kakaririshwa" wakati nikijuwa msimamo wake upo vipi siku zote. Wewe nakufahamu sana, tukirudi nyuma humu humu utakuta kwamba mara nyingi huwa hatupishani sana katika maswala muhimu kama hili la CHADEMA na hawa wabunge wao. Kwa hiyo leo, unapokuja hapa na kunibandikia lugha chafu vile, inanifanya nikumbuke tulivyowahi kukutana sehemu zingine humu humu. jukwaani.

Kuna mambo mengi sana yasiyokuwa na 'facts' kama unazozitaka, hata huko CHADEMA; lakini hilo halizuii mtu kutumia akili na kufanya 'deduction' ya kufikiri uwezekano wa kuwepo na hali anayoielezea huyo mtu.
Uwepo wa hao wabunge ndani ya Bunge toka mwanzo halijawahi kuwa na maelezo yalaiyonyooka na kulifanya liwe na 'facts' za kutumia kama ushahidi unaodai hapa.; kwa hiyo ni halali, 'deductions' zikitumika kueleza hali hiyo isiyo elezeka.

Kifupi: sijawahi kuona 'Facts' za viongozi wote ndani ya CHADEMA kutokuwa nyuma ya swala hilo.
 
Their careers are over like Mike anyone Tyson ,Jackson ,Jordan.

2025 ndiyo mwisho wa kufanya siasa hao covid 19 hawatoaminika sehemu yeyote.

Walikuja bila gadi jiwe na mkuu ndugai wakawapa kwa wastani kwa idadi.
 
Tunajua wapi ushenzi wa magu ulipoanzia na kuishia, na wapi mwenyekiti wa cdm alitoa baraka zake. Subiri tu kidogo utaona Nini kinaendelea na utetezi wa kina Mdee kwenye cdm.
Baraka za Mwenyekiti ziko wapi na zinawezaje kuvunja Katiba ya Nchi? na ili iweje? Maana hata ruzuku za vyama hazitokani na Wabunge wa viti maalum, Ni dhambi mbaya mno kusingizia mtu jambo kama hili
 
Sasa huyo Kiongozi wa Chadema aliyewatoa wafungwa na kuwapeleka kuapishwa ni nani na ana nguvu gani za kuvunja katiba ya nchi kiasi hiki?
Sijui kwa nini inakuwa ngumu kueleweka hapa. CHADEMA ingeweza vipi kuwatoa gerezani hao wafungwa wakati hawana madaraka hayo?. Lakini hujasema kama palikuwepo na kiongozi aliyekuwa na ufahamu wa jambo hilo, na pengine kulinyamazia na hata kuliruhusu liendelee mbele. Wewe unajuwa kila kitu kinachofanywa na viongozi binafsi, na hasa akiwa kiongozi wa juu kabisa?
 
Tunajua wapi ushenzi wa magu ulipoanzia na kuishia, na wapi mwenyekiti wa cdm alitoa baraka zake. Subiri tu kidogo utaona Nini kinaendelea na utetezi wa kina Mdee kwenye cdm.
Unachokiandika hata hakielewi, wala hakina mantiki, ni propaganda zako tu za kuunga unga mitandaoni kwa maslahi yako binafsi.

Sote tunajua suala la kina Halima na genge lake CHADEMA walishalifunga, kulizika na kupigilia misumari ya inchi sita kwenye jeneza lake. Wale malaya wa kisiasa walishavuliwa uanachama na ngazi zote za kikatiba za CHADEMA kubariki uamuzi ule wa kuwafuta uanachama, haitatokea tena iwe agenda ya msingi yq kujadiliwa popote ndani ya vikao vya Chadema.

Chadema wako busy na mambo yao ya msingi ya kusonga mbele kisiasa na kuwakomboa watanzania, hawana muda wa kujadili blah blah za malaya wa kisiasa.
 
Sasa kama hakukuwa na Mchakato wa Chama maana yake jambo hilo ni Batili, hii ni kwa sababu wabunge hao hawawezi kuwa wa Chadema, Sasa je ni wa Chama gani?
chama cha magufuli, hakikuwa na usajili wala hakikushiriki uchaguzi, kilikuwa na mwanachama mmoja tu aliyeitwa magu, kiliundwa baada ya uchaguzi mkuu 2020, hki chama halielezeki.
 
Sijui kwa nini inakuwa ngumu kueleweka hapa. CHADEMA ingeweza vipi kuwatoa gerezani hao wafungwa wakati hawana madaraka hayo?. Lakini hujasema kama palikuwepo na kiongozi aliyekuwa na ufahamu wa jambo hilo, na pengine kulinyamazia na hata kuliruhusu liendelee mbele. Wewe unajuwa kila kitu kinachofanywa na viongozi binafsi, na hasa akiwa kiongozi wa juu kabisa?
Mbona unazunguka mbuyu, si useme sasa hicho unachokiwaza hapa JF ili ueleweke kama unadhani ni facts?

Watu tumekuuliza, huo mkono wa baraka wa kigogo fulani ndani ya CHADEMA ulikuwa una nguvu gani au umuhimu gani wa lazima kuwepo ili kuwezesha michakato isiyo halali ya kuvunja katiba ya nchi kuweza kufanywa na utawala wa Magufuli katika suala la malaya wa kisiasa wa Covid 19?
 
Halima is smart to what?
Smart person always protects his/her legacy in each step. Halima alishapoteza legacy yake (trust&resist), Halima amenunulika kirahisi mnoo. Ukishakuwa msaliti huwezi tena kuwa trusted na huwezi tena kuwa stable.
Niliwahi kuamini hivyo; na pengine niliwahi kuandika maneno kama hayo hayo uliyoandika hapa kumhusu Halima.
Baada ya muda wote huo, akili inanikataza kutoa hukumu hiyo kwa Halima na wengine wote aliowaongoza kukiasi chama chao.
 
Mbona unazunguka mbuyu, si useme sasa hicho unachokiwaza hapa JF ili ueleweke kama unadhani ni facts?

Watu tumekuuliza, huo mkono wa baraka wa kigogo fulani ndani ya CHADEMA ulikuwa una nguvu gani au umuhimu gani wa lazima kuwepo ili kuwezesha michakato isiyo halali ya kuvunja katiba ya nchi kuweza kufanywa na utawala wa Magufuli katika suala la malaya wa kisiasa wa Covid 19?
Soma uelewe. kama hujaelewa usijibu kitu. Sijakwambia popote kwamba ninakwambia 'facts' kama unavyodai wewe.
Mimi ninatumia akili ku'deduce' mambo ambayo sioni 'facts' zake, lakini naona 'elements' za kujengea 'deductions hizo.
Usikimbilie kuhitimisha kitu katika jambo analosema mtu, mimi sijakwambia popote kwamba 'facts' ni hizi na hizi; sasa wewe unaniambia ni mtu wa "facts", lakini sizioni hizo facts zako. Nikiziona nitazielewa na kuzikubali au kuzikataa.
 
Niliwahi kuamini hivyo; na pengine niliwahi kuandika maneno kama hayo hayo uliyoandika hapa kumhusu Halima.
Baada ya muda wote huo, akili inanikataza kutoa hukumu hiyo kwa Halima na wengine wote aliowaongoza kukiasi chama chao.
Hatuko hapa kuamini au kutokuamini porojo za watu fulani fulani, tuko hapa JF kujadili facts zenye mantiki za kushawishi akili na kueleweka.
Sote tunajua Halima mdee na wale malaya wa Covid 19 wote ni wasaliti na walinunulika, wako pale kinyume cha katiba kwa baraka za CCM kwa 100%. Hakuna logic hata moja mpaka sasa ya kutushawishi vinginevyo.
Kama wewe unayo hiyo logic basi ilete hapa ili utushawishi na sisi.
 
Back
Top Bottom