Kwa maisha ya sasa watu wa namna hiyo wapo kibao mitaani,,, ushafanya kazi au kuishi jirani na dissaporra.. Watu walioishi ulaya miaka mingi kisha wakaamua kurudi nyumbani.. Hao hawanaga shobo sijui za kujuana mara tunafanya kazi ofisi moja, yaani hata lifti atoi kizembe zembe na huko mitaani ndo hivyo geti kali hamjui hata jirani yake yukoje...
Ubepari unaokuja kwa kasi Tanzania unabadilisha lifestyle ya wengi as ujirani wa kuzoeana sana na kupiga umbeya ndo unapotelea... Mi nilipokuwa nakaa majirani kukaa na kuongea hadi utokee msiba au sherehe, na kukutana kanisani tu au jumuia zaidi ya hapo kila mtu kivyake.. Marafiki wa watoto ni playstations na dstv tu.. Kucheza kila mtu kwao labda muazimane video games Cd, mwanzo nilipata shida wakati nahamia hilo eneo as nilitoka maisha ya quarter,,, majirani interaction kibao, watoto mnacheza pamoja hadi usiku na wazaz wanaelewa hawazingui, but tulikuja zoea hayo maisha..
Nimepanga sehem napoish now kuna wapangaji wengi but nina karibu mwaka siwajui hata majiran zangu as kila mtu kimpango wake... Ubepari na resi za kusaka shilingi unatubadilisha maisha watanzania lazima tukubaliane na mabadiliko as kufatana fatana na kujuana juana bila sababu za msingi siku hizi hakuna