Unajua binadamu tunakosea kitu kimoja kikubwa. Tunajali sana mahusiano yetu na binadamu wengine, kuliko mahusiano yetu na Mungu. As a result tunawapa hao wapendwa zetu power kubwa ya wao kutudirect watakavyo kama remote vile. Mtu ukiulizwa kwa nini unakuwa faithful kwa mwenzi wako, unajibu ni kwa sababu sitaki kumuumiza, but jibu lilitakiwa kuwa " sitaki kumtenda Mungu dhambi". Ukimuogopa Mungu kwanza, utaogopa hata kuwaumiza na wengine Kwa kuwatendea mabaya. Ndo maana tunasema uzinzi bila hofu ya Mungu mmh sijui
Kwa sababu ya kuwapa wapendwa wetu power zaidi, ndo ikitokea leo mtu kakuumiza, basi unaamua kuharibu maisha yako in the name of kulipiza. Unamkomesha nani kwa kuharibu maisha yako mwenyewe? ? Kila mtu anapata kitu tofauti huko kwenye kuchepuka. Mwingine atachepuka atapata magonjwa, mwingine ndoa itavunjika, mwingine atafumaniwa atakatwa mguu, mwingine watapigana atauawa aache watoto wake, hujajiharibia maisha yako? Kama partner wako ni serial cheater, better usepe zako, umefanya yote ndani ya uwezo wako na unaona mnapoelekea ni pabaya zaidi, please sepa tu kabla hayajakukuta makubwa ukaacha wanao wanateseka. Mtu asikufanye ukabadilika ukawa binadamu "mbaya", ukawa mtu ambaye hukutaka kuwa, kisa kakuumiza. "Don't become who hurt you". At the end of the day, kila mtu atatoa hesabu yake kwa Mungu separately, je utasema I was a cheat because my wife started cheating on me? Is that even an excuse? ???