Familia Bora: Chanzo cha Mafanikio

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,880
FAMILIA BORA; CHANZO CHA MAFANIKIO

Na, Robert Heriel

Maandishi ya Robert Heriel Kwa Lugha ya Kiswahili.
Haki zote zimehifadhiwa

Huwezi ukafanikiwa kama hujatoka familia bora, na kama umefanikiwa na haujatoka familia bora basi kaa ukitambua kuwa mafanikio hayo hayatadumu ikiwa wewe nawe hautajenga familia bora. Familia bora ndio msingi mkuu wa mafanikio.

Lakini familia bora ni ipi, ikoje, inafananaje, inapatikana vipi? Na kwa nini familia bora iwe chanzo cha mafanikio? Kaa nami Taikon Wa Fasihi katika makala hii, yenye jumbe na panchi za uhakika, zitakazofungua milango mingi iliyojifunga.

Familia bora ni ile yenye muunganiko wenye uwiano sawa kihisia, kimaslahi, kimaumbile, kimtazamo na kiimani baina ya Baba na mama ambao baadaye huzaa watoto.

* Ili familia iwe bora lazima kuwe na uwiano wa kihisia, kimapenzi, upendo, tamaa ya mwili baina ya mwanaume na mwanamke. Mwanaume na mwanamke lazima wapendane. Yaani upendo wao uwe katika kiwango sawa. Hii itafanya wavumiliane, waoneane huruma, wajaliane, wathaminiane, waoneane wivu kwa kiwango kile kile.

* Ili familia iwe bora lazima kuwe na uwiano unaolingana wa Kimaslahi. na hapa nazungumzia uchumi. Baba anapaswa awe anachapakazi na kuzalisha kwa kiwango chake cha ubaba, halikadhalika mama naye afanyekazi kwa kiwango kile kile cha umama. Hii ni kusema, Baba anapaswa amzidi Mama katika utafutaji lakini haimaanishi Baba ni zaidi ya Mama bali ni majukumu kama mwanaume. Mwanaume isije ikatokea mkeo akafikiri kuwa kama yeye ndio angekuwa mwanaume angefanya zaidi yako. Hii inamaanisha kuna sehemu unafeli, kuna mambo huyafanyi kwa ufanisi.

* Ili familia iwe bora lazima kuwe na uwiano wa kimaumbile. Lazima mwanaume na mwanamke walinganane kimaumbile, rangi, na muonekano. Hii itafanya wazidi kupendana na kutokuzarauliana kwani watajijua wao ni jamii moja. Ninashauriwa mwanaume amzidi mwanamke urefu kidogo kama nusu futi au futi moja kabisa. Lakini pia mwanamke kama atakuwa mrefu basi amzidi mumewe nusu futi tuu. Rangi ni muhimu. Rangi nyeusi iende kwa nyeupe au maji ya kunde, rangu maji ya kunde iende kwa rangi yeyote, nyeupe iende kwa maji ya kunde na nyeusi. Lakini sishauri nyeusi kwa nyeuisi, au nyeupe kwa nyeupe. Ila sisemi kuwa kama watu wameshaoana waachane laa, wanaweza kuendelea.

Maumbile ni moja ya mambo nyeti kwenye mahusiano hasa ya ndoa. Wanaume wenye uume mrefu wanapaswa kuchukua wanawake wenye maumbile makubwa, warefu na wenye nyama uzembe nyingi, na hapa ni matako makubwa, mapaja manene.

Wanaume wenye uume wa kati hawa waoe wanawake wa aina yoyote. Hawa hawana masharti

Wanaume wenye uume mfupi na hapa ni chini ya inchi nne. Hawa waoe wanawake wafupi wasio na unene mkubwa, wala matakao, wala mapaja makubwa. Ikiwezekana waoe wanawake katika ubikra wao.

Wanaume wenye uume mrefu wasioe wanawake wafupi sana, na wale wenye uke mdogo.

Kwanini nimeshauri haya?
Ili familia iwe bora lazima pawe na kuridhishana kwenye maumbile hasa ya faradha. Kila mmoja apate saizi yake. Familia haiwezi kuwa bora ikiwa mmoja wa wanandoa hafurahii maumbile ya mwenzake. Ni lazima ndoa iharibike tuu. Usaliti wa mapenzi unaanzia hapa.

Vijana wengi wa siku hizi hupenda wanawake wenye matako makubwa na hipsi kubwa. Wengi huona ufahari kuoa mwanamke mwenye matako makubwa. Lakini ni lazima kabla hujaoa utazame maumbile ya mwanamke unayotaka kumuoa kuwa yanaendana na yako. Sio wewe ni kibamia alafu unachukua mwanamke wa kibantu aliyeshiba. Hakika utamkosesha haki yake ya msingi.

Halikadhalika na wenye uume mkubwa msioe wanawake wenye maumbile madogo, hasa uke mdogo huko ni kutafutana lawama.

* Familia iwe bora lazima wanandoa wawe na uwiano unaolingana wa kimtazamo na kiimani. Hii inasaidia katika malezi., katika utafutaji, katika kipindi kigumu, katika migogoro ya kifamilia ni rahisi kusuluhisha. Familia ambayo mume na mke wanafanana mtazamo na imani ni rahisi sana kufanikiwa. Pia ni rahisi kuwa na umoja. Hata watoto wanakuwa na umoja. Lakini familia inapokuwa na tofauti ya kimtazamo baina ya Baba na mama huleta utengano ndani ya familia.

Baba ndiye anayeunda mtazamo, falsafa na imani kwa mke wake. Ikiwa Baba atafeli katika hili basi atakuwa amefeli kila kitu ndani ya nyumba. Hata watoto watamsumbua tuu Mama. Ni muhimu Baba kumtiisha Mama.
Mama akishamtii Baba, basi watoto lazima watakuwa na adabu. Lakini endapo Mama asipomtii Baba mara nyingi watoto wanakosa adabu, wanakosa focus na wengi huwa kama wana laana.


Familia bora hujengwa na mambo yafuatayo;

1. Upendo.
Ili familia iwe bora ni lazima Mume na mke wapendane kikamilifu. Na wawe na uwiano kama nilivyoonyesha huko juu.
Hamuwezi kupendana ikiwa kimaslahi hakuna uwiano. Yaani kuna mmoja ni mvivu katika uzalishaji mali. Ili mpendane ni sharti kila mmoja afanyekazi ya uzalishaji mali.

NGUZO ZA UPENDO

1.1. KAZI
Msingi wa mapenzi upo katika kazi, kwa maana mwanamke aliumbwa kwa kusudi la kumsaidia mume wake kazi.
Hivyo sio ajabu mwanamke akikuuliza unafanya kazi gani. Hiyo ipo automatic yaani mwanamke yupo kwa ajili ya kukusaidia kazi. Kama huna kazi jua hakuna mapenzi. Wala mtu asikudanganye. Sasa kama huna kazi mwanamke atakuwa msaidizi wako kwa kazi ipi.

Katika nguzo hii ya kwanza, familia inapata manufaa yafuatayo
i. Uchumi kuwa mzuri; hii itafanya mtakula vizuri, mtavaa vizuri na kulala pazuri
ii. Mtawekeza na kuwaandalia watoto urithi
iii. Mtakuwa hamna muda wa kufanya uhuni
iv. Miili yenu itakuwa imara kwani kazi ni sehemu ya mazoezi ya kimwili na kiakili
v. Mtaweza kushirikiana vizuri ndani ya jamii, mkiheshimiwa.
vi. Hata mmoja akitangulia mbele za haki, bado atamuacha mwenzake akiwa na uzoefu wa kazi na kuendesha maisha. Tofauti na mtu ambaye asiyefanya kazi hasa wanawake waliozoea kulishwa tuu. Mume anapokufa inakuwa mtihani kuwalea watoto.

1.2 . TENDO LA NDOA
Mkimaliza kazi za uzalishaji mali mtakuwa mmechoka, sasa miili yenu itahitaji kuburudishana. Hapo mtafanya tendo la ndoa. Tendo la ndoa ni msingi wa pili katika ndoa.
Vijana wengi hutanguliza tendo la ndoa kama namba moja lakini kimsingi upendo kitu cha kwanza ni kazi. Tendo la ndoa halichukua hata robo ya tatu ya muda wetu lakini kazi huchukua karibu nusu ya muda wetu duniani. Kikawaida kufanya mapenzi ni dakika 30 kwa mchezo wa kwanza, ukiunganisha na mchezo wa pili ni lisaa limoja.

Kingine huwezi fanya tendo la ndoa kwa ufanisi kama huna kazi ya kukuzalishia. Ili ufurahie mapenzi ni lazima uwe na kazi inayokuingizia kipato. Mkeo au mumeo anukie vizuri, ashibe vizuri, mfanyie sehemu nzuri, kisha mkimaliza mjipongeze. Zote hizo ni pesa na zinapatikana kupitia kazi

Tendo la ndoa linahusisha hisia, muonekano. harufu na maumbile. Nilisema, lazima umpate mwenzi mnayelingana maumbile, mwenye rangi isiyokinai machoni mwako na hapa zaidi ni ile rangi iliyotofauti na wewe. Uume saizi yako ni muhimu wakati wa tendo la ndoa.

Faida za tendo la ndoa
> Tunapata watoto wa damu yetu
> Tunafurahishana na kuburudika
> Ni sehemu ya kupunguza sumu mwilini ikiwemo misongo ya mawazo, hasira, chuki,
> Sehemu ya kuombeana msamaha
> Sehemu ya mapumziko

Hizo ndio nguzo kuu mbili za upendo, kazi na tendo la ndoa. Ukifanya kazi vizuri na kumcharaza vyema mkeo, au kumpa mumeo mapenzi mazito hakika na kuambia ndoa lazima isimame

Kazi itakufundisha uvumilivu, kusamehe, lugha nzuri, heshima, kuthamini, kujali, n.k Wanasema kazi ni kipimo cha utu.
Tendo la ndoa litakufundisha kudeka, starehe, kuneng'eneka, mahaba n.k.

2. MAADILI
Jambo la pili kwenye familia bora ni maadili.
Mwanaume ndiye chanzo cha maadili ndani ya nyuma, lakini Mama ndiye mratibu wa maadili hayo. Kama hakuna ushirikiano baina ya mume na mke kwenye ishu ya maadili basi familia haiwezi kuwa bora.
Tunapozungumzia maadili tunazungumzia kujua mema na mabaya, na kuyachagua mema peke yake huku mabaya tukiyaacha na kuyapinga.

Aina za maadili kwenye Familia
2.1. Maadili ya kimapenzi
2.2. Maadili ya kiuchumi
2.3. Maadili ya kijamii
2.4. Maadili ya kiutamaduni
2.5. Maadili ya kiimani

* Maadili ya Kimapenzi
Haya ni maadili yanayohusu masuala ya tendo la ngono. Mke au mume anapaswa awe na maadili ndani ya ndoa. Hapaswi kumsaliti mwenza wake.
Familia bora lazima iwe na maadili ya kimapenzi. Faida ya aina hii ni kuwa, familia itazidi kuwa na amani, na furaha kwani kila mmoja atakuwa mwaminifu kwa mwenzake, pia magonjwa ya ngono hayataingia kwa urahisi kama vile HIV, Pia masuala ya kulogwa au kulogana kisa mapenzi ni ngumu kuingia ikiwa kipengele hiki kitazingatia.

* Maadili ya kiuchumi
Familia Bora lazima iwe na maadili kwenye suala la fedha na mali za familia. Lazima kuwe na umoja na ushirikiano katika kuchuma mali na kuzitumia. Wote lazima mshirikiane kuchuma mali. Mali isihesabike ni ya mtu binafsi bali mali ya wote.
Mikakati, mipango na utekelezaji lazima vijadiliwe kwa pamoja baina ya mke na mume.
Haya yote ili yafanyike lazima kuwe na maadili ya kimapenzi, yaani kuwe na uaminifu wa kimapenzi baina ya wanandoa. Mume au mke asiyemwaminifu hawezi kuwa na maadili ya kiuchumi ikiwa anasaliti nje ya ndoa.

Maadili ya kiuchumi ni muhimu katika mafanikio ya familia. Kusiwe na usiri. Ati mume au mke anafanya jambo fulani labda anajenga nyumba sehemu fulani bila kumwambia mke wake. Huo unaitwa uzwazwa, wehu na upungufu wa akili.

Mali mnazochuma ni zenu na watoto wenu, hakuna anayehusika zaidi yenu na watoto wenu. Labda mutoe kwa ndugu kwa hiyari yenu.

Ubinafsi ndio unawaangusha watu wengi. Mwanamke anataka kujenga kwao, na mwanaume anataka kujenga kwao. mwisho mnasahau kujenga kwenu na watoto wenu.

Familia bora haigombanii urithi, haigawani urithi bali inaendeleza urithi ulioachwa na wazazi.

Familia zetu za Kiafrika zinaendelea kuwa masikini kwa sababu tajiri anapokufa watu hugawana mali badala ya kuziendeleza.

Familia bora haziingiliwi na ndugu, ndugu wanamipaka yao ndani ya ndoa yao. Hata mmoja akifa ndugu hawagombe mali za ndugu aliyekufa, bali huwaachia watoto waendeleze mali za wazazi wao. Ikiwa watoto ni wadogo basi utaratibu wa kimahakama utakuwa umeandaliwa kusudi mali zisipotee au zising'ang'aniwe na ndugu wenye tamaa.

Familia bora, mke anajua yeye ndiye msimamizi mkuu wa mali za mume wake. Mke anajua hata mume wake akifa atasimamia yale mume wake aliyoyasimamia kipindi akiwa hai.

* Maadili ya kijamii
Wanandoa wataheshimu sheria na tarartibu zilizopo ndani ya jamii yao. Watahakikisha wanakuwa na sifa njema wao na watoto wao. Warahakikisha wanawalea watoto vizuri ili wawe baraka kwa familia na jamii kwa ujumla.
Hawatasumbua majirani, watashiriki kwenye shughuli za kijamii kama vile misiba, sherehe na misaragambo.

* Maadili ya Kiutamaduni
Familia bora itaheshimu utamaduni wa asili zao, hasa utamaduni wa Baba.
Mke akishaolewa atahakikisha ana-copy utamaduni wa kina mume wake.
Wataheshimu lugha za kwao, chakula, mavazi, mila na desturi, miiko, ngoma na burudani.
Mume atahakikisha mke wake anaupenda utamaduni na kuufundisha kwa watoto.
Familia yoyote isiyoheshimu utamaduni wa asili haiwezi kuwa familia bora. Endapo Baba au mama ataudharau utamaduni wake basi anatengeneza mazingira ya watoto kumdharau hapo baadae.

Sishangai kwa nini watoto wa siku hizi wengi wao hawana adabu, ni kwa sababu wazazi wengi wamewafundisha watoto waoo kudharau utamaduni wa nyumbani, Jamii zote duniani zinazoendekeza utamaduni zote zimeendelea. Lakini zote zilizotupilia mbali tamaduni zao karibu zote zinautumwa na masikini wa kutupwa.

* Maadili ya Kiimani
Familia Bora lazima iwe na Mungu. Haijalishi ni Mungu gani lakini familia yoyote bora lazima iwe na dini.
Ili kuwe na maelewano mazuri ndani ya familia lazima kuwe na maadili ya kiimani.
Tunajua Baba ndiye kichwa cha nyumba, kila anayekosea ndani ya nyumba basi mashtaka hupelekwa kwa Baba, Je Baba akoseapo mashtaka yanapelekwa kwa nani? Jibu la uhakika ni kuwa Yanapelekwa kwa Mungu.

Mwanamke mwenye akili kabla hajaolewa ni lazima ajue wazazi wa mume wake mtarajiwa ni kina nani, kisha lazima ajue Mungu anayeabudiwa na Mume wake ni Mungu yupi. Hiyo itatoa picha kuwa huyo mwanaume ni mume wa aina gani.

Mke anapaswa amfuate Mungu wa mume wake, sio ruhusa mume kumfuata mungu wa mke wake hata kama ni wa kweli.

Mume na mke sharti wawe na imani moja, wamuabudu Mungu mmoja kwa ustawi wa mafanikio ndani ya familia. Kamwe familia haiwezi kuendelea ikiwa kuna miungu wawili ndani ya nyumba moja. Nyumba yenye miungu wawili ni nyumba iliyoukiwa, haina Mungu yeyote. Nyingi huandamwa na mikosi na majanga.

Lakini nyuumba inayonia mamoja, dini moja, imani moja kufanikiwa ni asubuhi kabisa kabla jua halijatoka.

Kwa leo niishie hapo, ikiwa unaswali, maoni basi waweza kujadiliana nami hapo chini, waweza kushare.

Pole kwa andiko refu, na Ahsante kwa muda wako

Ulikuwa nami

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Unasema huwezi fanikiwa kama ujatoka familia bora?????

Nimeishia hapo kusoma.
 
Hapo kwenye issue za kuoa na kuolewa, hilo soma lilipashwa litolewe kwa nguvu kubwa kwenye jamii ili maamuzi sahihi yachukuliwe kwa wote muoaji na muolewaji..
 
Umemaliza kila kitu kwenye hii topic yako hasa swala la watu kuoana kulingana na mitazamo, na maono na ndoto ili mtimiziane
 
wewe wasema.

Hafu wabongo tabia ya kukurupuka na maandiko yenu uchwara huko,hfu mnataka yawe sheria muache.


Kwani nimekuambia hii ni sheria za umedi au uajemi hata zisitanguke?

Nimekuambia tuu kuwa maamuzi uliyoyafanya yanathibitisha andiko langu
 
Na ndoa yoyote yenye amani na upendo ni rahisi kukaa chini na kupanga maendeleo tofauti na ndoa za watu walio na malengo tofauti wanaoishi kwa kuviziana.
 
Na ndoa yoyote yenye amani na upendo ni rahisi kukaa chini na kupanga maendeleo tofauti na ndoa za watu walio na malengo tofauti wanaoishi kwa kuviziana.


Ndoa ikishakuwa na ubinfasi imekwisha, kuwa mali ya mume ni ya mume, ya mke ni ya mke, au moja ya familia nyingine ni binafsi hapo habari imeisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom