Nini cha kufanya kutenganisha kiwanja?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,959
22,156
Jana nilikuwa sehemu vijana walifanikiwa kumalizana mizozo ya viwanja

Sasa wamekubaliana kugawana kiwanja cha mama yao Chenye hati moja


Wanataka msaada jinsi ya kutenganisha hati moja ziwe mbili, kila mtu awe na kiwanja chake

Sijui wenye kupitia haya wapi wanaanzia kuweza kuwa na kila mtu na kiwanja chake

Sikukuu njema
 
Binafsi sijaelewa ulichoandika
Ni kiwanja cha urithi madogo wamegawana

Sasa wanataka kila mtu apate hati yake kutokana na mgao

Kiwanja kina hati moja kifupi kutenganisha hati.....
 
Kiwanja kipo kwenye jina la nani kwa sasa? Jina la marehemu au jina la msimamizi wa mirathi?
 
1. Surrender hati manispaa: andika barua kwa mkurugenzi ya kurudisha hati lengo likiwa ni kutoa fursa ya kugawa kiwanja .

Mchakato utaanza hapo manispaa, kwenda kwa kamishna wa ardhi wa mkoa mpaka kwa msajili wa hati wa mkoa ambae atakupa document inaitwa deed of surrender, hapo mchakato wa kurudisha utakuwa umekamilika.

2. Andika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba kufuta upimaji( survey plan) ya hicho kiwanja, katika hiyo barua ambatanisha na ile deed of surrender.

Mchakato utaanza hapo manispaa ambapo wao watakachokifanya nikuonesha tu wamepokea ombi na hawana pingamizi na mwisho wataforward ombi lako kwa mpima wa mkoa ambae yeye ndie atakayefuta na kuwapa taarifa manispaa kwa barua kuwa amefuta, ( kumbuka kuweka sababu ya kwa nini unaomba kufuta)

3. Andika barua kwa mkurugenzi kuomba kufanya ammendment ya mchoro wa mipango miji wa eneo husika, hapa utaambanisha na mfano wa mchoro wa namna mnavyotaka kugawa.

Ammendment ikipita manispaa itaenda mpaka mkoani na kusajiliwa
4. Tafuta mpima atakayepima kuja kupima viwanja ambavyo ammendment imekubali, mpima atapima na kuwasilisha manispaa, ikipita manispaa itaenda mkoani na kusajiliwa
5. Viwanja vikishasajiliwa unarudi manispaa kuomba hati kwa kujaza form no. 19 pamoja na fomu za kumbukumbu za eneo na mipaka.

Mchakato ukitoka hapo utaenda kwa kamishna wa ardhi wa mkoa na mwisho kwa msajili wa hati,
Hapo kila mtu atakuwa amemiliki kiwanja chake
 
Kiwanja kimepimwa?
Kina hati?
Kina ukubwa gani?

Uwwzekano upo kilingana na majibu hayo. Tupe kazi.
 
Back
Top Bottom