Nini asili na maana ya neno Bongo

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,088
Wengine wamekua waki refer Tanzania kama bongo na wengine waki refer Dar ea salaam km bongo, yote kwa yote, ni ipi asili na maana ya neno hili mpaka tukawa na vitu kama Bongo fleva na bongo movie?
 
Wabongo bwana ukiwauliza swali badala ya kutoa jibu naye anauliza swali :- nani kakwambia !?
 
Baada ya vita vya Uganda hali ilikuwa ngumu sana, Nyerere a kawaambia watu tumieni ubongo kuishi, yaani watumie akili kukabiliana na ukata uliokuwepo baada ya vita, ikawa kila mtu anamwambia mwenzake tumia "bongo" ikawa mwanzo wa neno bongo.
 
Dah asee yani naona zimetoka theory kama 5 iv zote zinaweza kuwa na udhaifu pamoja na strength zake
1. Prof j na jide kwa nyimbo ya bongo dar es salaam
2. Kanda bongo man
3. Nyerere baada ya kusema tumieni ubong kukabiliana na hard life
M naona iyo ya kwanza kidog kama iko pow iv wakuu
 
Wengine wamekua waki refer Tanzania kama bongo na wengine waki refer Dar ea salaam km bongo, yote kwa yote, ni ipi asili na maana ya neno hili mpaka tukawa na vitu kama Bongo fleva na bongo movie?
Bongo zenu zimelala. Mmeaminishwa mwenge unaleta amani..... kwanini hamkuupeleka kwenye vita vya Kagera? Au ile vita ilikuwa ni friend match?

Wakati now mnaimba vibwagizo vya wacha waisome namba wenzenu Kenya 🇰🇪 wanapiga hela kwa katanga kutangaza kwamba Serengeti mlima Kilimanjaro na Tanzanite ni vyao.

Mazuzu nyie bongo lala
 
Bongo zenu zimelala. Mmeaminishwa mwenge unaleta amani..... kwanini hamkuupeleka kwenye vita vya Kagera? Au ile vita ilikuwa ni friend match?

Wakati now mnaimba vibwagizo vya wacha waisome namba wenzenu Kenya wanapiga hela kwa katanga kutangaza kwamba Serengeti mlima Kilimanjaro na Tanzanite ni vyao.

Mazuzu nyie bongo lala
Sikujua kama hii ndio maana ya bongo
 
Bongo asili yake ni kuishi kwa kutumi akili sana kupambanua changamoto za maisha.

Bongo ni Dar es salaam na sio Tanzania.

Jarida la Bongo longtime kitambo kabla ya seasons na series lina akisi hilo

Wimbo wa bongo dar es salaam pia nenda kausikilize

"Aliyeuza cheni kapewa hela ya bandia na aliyetoa hela nae kauziwa cheni ya bandia"
 
Ugumu wa maisha ya Dsm, ujanja janja, utapeli vikahuishwa na utumiaji akili ili ukwepe, uvuke, ushinde, uwepo wa kuchekana maswahibu, kurejea makwao mikoani, namna bora kutusua dsm ni kuchezesha ubongo au kucheza na bongo za watu.

Kuishi dsm mtaji akili zako a k.a Bongo
 
Bongo asili yake ni kuishi kwa kutumi akili sana kupambanua changamoto za maisha.

Bongo ni Dar es salaam na sio Tanzania.

Jarida la Bongo longtime kitambo kabla ya seasons na series lina akisi hilo

Wimbo wa bongo dar es salaam pia nenda kausikilize

"Aliyeuza cheni kapewa hela ya bandia na aliyetoa hela nae kauziwa cheni ya bandia"
😅😅😅 Ngoma ikawa draw au sare. Kwa hiyo hakuna aliyepata hasara......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom