Kapo Jr
JF-Expert Member
- Jan 31, 2011
- 1,003
- 303
Heshima kwa wasanii wote walihusika kufikisha hapa muziki wa kizazi kipya maarufu bongo fleva,pia R.I.P kwa wasanii waliotangulia mbele za haki especially D-ROB.Kwa miaka mingi baad
hi ya wasanii wamejaribu kuleta ladha tofauti na asili yenyewe(bongo fleva) lakini wapo waliosimamia misingi ya asili!pia wasanii wakongwe kutonufaika na matunda ya jasho lao kufikia hatua kuacha kujihusisha na muziki huo,Kuna wakongwe waliojaaliwa ubunifu na vipaji mfano halisi ni Mr.Sugu/Mr.II kuanzisha jukwaa mahsusi kwa wakongwe waliotamba na kutoka fursa ya kuimba kwa kutumia band 'live' na kuvutia mashabiki pande tofauti nje na ndani ya nchi,heshima kwake jongwe. Hivi karibuni Kuna "vibe" limeanzishwa linalojulikana kama miaka 30 ya Bongo fleva lengo kuu ni kuwaleta pamoja wasanii wakongwe kuburudisha na kupata kipato,vema!kumekua na malalamiko kwa baadhi ya wasanii kutoshirikishwa,si dalili nzuri kwa ustawi wa Sanaa ya bongo fleva! Kama lengo ni kuhusu maslahi ya wasanii na misingi ya bongo fleva siasa zingebaki kando na muziki,tofauti inaonekana wazi baada kuanzisha "miaka 30 ya Bongo fleva" kubeba maudhui tofauti na "Bongo fleva Honour". Ili kulinda "brand" umakini unatakiwa ktk jambo kama hili.