Huyu ni binti ambaye alikuja kwangu kwa gia kama ya dada. Ni mfanyakazi mwenzangu.
Kiukweli ni binti mzuri tu Manka wa huko kaskazini. Sasa mimi nilimchana kuwa sijamuelewa so sitaki kumchezea
Ikawa nimetangaza uadui yani ananichukia na sijui sababu, na nina mashaka anaweza nitumia hata majambazi.
Chuki yake kwangu ni kubwa sana, ameahidi kuniharibia, salamu hajibu na kanichunia. Anaeneza sumu mpaka kwa mabosi, uzuri ni waelewa.
Nilimkataa kwa sababu huyu binti ana dharau na mjuaji sana, aliwahi kumkataa kwa madaha jamaa yangu aliyejitosa kumtongoza, tena kwa heshima mno.
Nilichoumia sana ni kuwa jamaa yangu ni mtu mstaarabu sana, ni nice guy mzuri mno sasa kwa nini ajibiwe kwa dharau wakati hakustahili?
Na sio huyo tu, ni tabia zake kwa karibu kila mwanaume anayejitosa kumtongoza. Anajiamini sana for nothing
Napambana naye vipi huyu?
Sent from my A50s using
JamiiForums mobile app