Ninauguliwa na baba watoto wangu

Status
Not open for further replies.



Unachokiongea ndio cha ajabu sasa!

Sijamtolea maneno ya ajabu,nimetoa FACT!

Shida tuonazo wote!Kuumwa tunaumiwa wote!Na kazi au biashara vipato ni hivi hivi kama anavyopata Mamdenyi,mi nachukia pale mpuuzi mmoja anapoona shida yake yeye ina worth kuandikia insha ili wananchi tumbebe mzigo!

Thats what i hate to the core!

Wote tunavumilia shida hapa!Keep it for urself and work it out as human being!
 



Tabia ya kuomba misaada sio tabia nzuri worldwide hadi biblia yenu inakataza!

Sasa tukisema kila mtu aweke shida zake hapa aombe msaada zitakua ni thread elfu kumi kwa siku!Hamna ujinga zaidi ya huo!

Sipendi kabisa mtu anapogeuza tatizo la familia yake ni tatizo la jamiii nzima.Analipakaza kwa jamii nzima kwa kutunga insha nzuri sababu ana platform ya JF!

Personally siamini kabisa mtu asieweza vumilia matatizo yake!

Nauguza sana,naumwa binafsi,napata majanga mengi,in no way nifungue thread nielezee lolote,not on this earth!

Kuna watu hua wana DNA ya kupayukapayuka wanapopata na matatizo hata liwe dogo kiasi gani!Mnaeleweka!
 
Haya umesikika kwa hiyo shida yako kubwa ni ipi kati ya hizi:
>>> Kakulazimisha wewe umpe.
>>> Alishawahi kukutapeli.
>>> Una bifu lako unataka umalizie kwake.
>>> Alishawahi kukuibia.
>>> Alikunyima mwanae.

Ikiwa hakuna hata kimoja ambacho kinakukwaza kati ya hivyo naomba utuache sisi masikini wenzie tumpige tafu.
Maana kama ni bifu naona una lako mwanaume huongea kitu kikapita.
Najua kinachokuuma ninkuona amepata watu wengi wanaomsapot.
Kama unaona una shida sema nikutumie kiasi gani sasa hivi angalau utupungizie kelele.
Na kama unaona tabu kusema hapa njoo PM unambie ntakutumia sasa hivi...ili mradi tuwe na amani kidogo.
 
Mkuu umejuaje kama hana watu anaojuana nao humu? Halafu wapo watu wengi sana kuliko unavyofikili wewe wanapita kimya wengine pesa wanazo ila hawataki kumchangia wana mawazo kama yako wewe ila hawaleti nyodo kama zako.

Usijifanye mjuaji wa kuongea sana wee kama vipi kausha tu sio lazima ubishane na watu.

Wenye moyo wa kutoa watatoa na wasiotaka wamekaa kimya wanasoma tu hawalete kejeli.
 
Pole sana
Kwa kuwa umekuwa ukitueleza ya maishani mwako humu.. ninaamini wengi tutakusaidia bila kukuhoji lolote kama wengine ambao hawajakujulia kukusoma humu na yako.

Mola amponye baba watoto.
 

Acha wivu wa maisha ya watu.
 

Wivu umekujaa unajua na shida zako ulipo ukiomba msaada hautapewa

Hata ikifika pesa ndefu ni yake kapewa na watu walioamua.. wewe inakuwasha nini kama sio ujambazo huo kumuonea wivu..

Usitusemee wengine eti anatubebesha mzigo wananchi.. kwani kaja kukushika shingo ili umsaidie..

Kaa chini jipige vibao vya usoni ulie kabisa.. roho mbaya yako ya wivu na ulivyo umeonyesha hauna furaha maishani na full alosto..

Kalale mbele toa ugwadu wako kwenye huu uzi
 
Mungu akutie nguvu,
Tunachanga, tunaomba pia uwe unatujulisha hali inavyokwenda. "updates* ili kama kuna msaada zaidi ya fedha uweze kusaidiwa.
Nakutakia baraka za Mungu.
 
Joined dec 2017 Angalalia mwombaji amejoin lini na anawafahamu wangapi humu JF? Kitu ambacho wengine hawajui ni kuwa tuna ID fake lakini nyuma ya dirisha tunafahamiana na kuwasiliana ingawa hatujawahi onana.
 
Mamndenyi dada, are you serious umekosa nauli hata kwa ndugu zako? Unajishughulisha na shughuli gani?
Huyo ni mwalimu USA river Arusha...amekaa kidanga danga maana hata cheti chake kina utata coz mwaka juzi wakati naendesha biashara yangu ya kutengeneza vyeti feki kupitia ID fake na yeye alikuwa mteja wangu.

Sasa naona baada ya Magufuli kupigilia msumari wa pili wa kukataza michago shuleni kaamua awe kilietivu.
 
Yote hayp hawezi yajua sababu ya kujifanya tajiri!!.. Hatukatai kuwa sio tabia nzuri kuombaomba lakini kama unaomba kwa ajiri ya matukio makubwa kwanini tusikuchangie!.
Ingekuwa ni ile naombeni nile, naombeni ninunue nguo tungekuja na ushauri tofauti lakini mzazi mwenzie waliezaa nae watoto 4 anaumwa na kapewa taarifa hadi na shemeji kwanini asipige moyo konde aende sikiliza nini anaitiwa.
 
Kuna ombaomba na kukopa!

Hujui tofauti na mvi zote hizo?

Utachekwa ujue!
Ulivyo mjinga ukashindwa connect the dot nilipomalizia na KISA ANA MALI YA KUWEKA BANK. unazani kama angekuwa na mali angeshindwa jaribu iweka bank apate mkopo atajua anaulipaje!?..
Haya friends na family unakuta wana hela ya kula apate wapi, halafu JF kuna watu wamekaa pamoja muda mrefu mpaka wamekuwa kama ndugu wa mbali, kuna watu wamefikia kuwa na wake/mme humu we na roho lako unazani utajua hilo!.
Unapomsaidia mtu msaidie bila kinyongo akikutapeli karma is around!..
Nafunga huu mjadala kwa upande wangu.
 
Jamani wana jamii, wengi ni watoto wangu, wengine ni wahenga wenzangu;
Hivi hao wanaonitukana huko juu hawamwogopi Mungu?

Laiti mngejuwa kuwa ni maisha gani nimeisha tokea huyo baba yenu
tutengane wala msingeenda huko;

Nashukuru kwa michango; pia kuna kijana wangu amesema atanipa tiketi so
niwasiliane naye kesho jumamosi.

Mungu akipenda nitaondoka dar jumapili kwenda huko mbeya
kumwona huyo mgonjwa; na nitakuwa nawajulisha hatua kwa hatua kuhusu hiyo safari.

Kweli nawashukuru sana, watu wa MUNGU mlioguswa hata mkaingiza mikono yenu mfukoni
na kumega mkate wa familia yenu kunipa. Naamini kuna siku Mungu atawakumbusha michango
yenu mliyonitolea;
 
Mamndenyi,
Nakuomba wala usihangaike na hao wajuaji wachache ambao hawafiki hata 1% ya population ya JF, wapuuze tu.

Mungu atakusaidia, michango itaendelea kuja na safari yako itabarikiwa!
 
Achana nao Mama yangu wasikuumize kichwa la muhimu wengi wamekuelewa.
 
Tulioelewa tumekuelewa na kukupa baraka kwa jinsi inavyowezekana, ndivyo Mungu alivyojaalia.
Mshukuru yeye zaidi.
Hao wanaokejeli waache mpaka Mungu atakapo wagusa ndipo wataelewa shida ni nini.
Hata msibani sio wote huwa wanaenda kuomboleza. Wapo wanaokejeli, na wengine kuonesha mavazi nawengine kutafuta wachumba. Likimfika ndipo hujua thamani na maumivu.
Hatukatai ndivyo Mungu alivyotuumba,
Uwe na Amani, mkono wa Mungu hautakupungukia.
Bwana akutangulie.
 
Mama Sabrina sijakuona hapa mtani wangu.
Fanya ulete japo elfu mbili ya ya maji kunywa njiani zile unazopewa na kishemegi changu.
 
Mamndenyi pole...... Maisha yana mitiani yake.... Ukiwa kama mama na nguzo ya familia. Nimekufahamu kipindi kirefu humu... Na bila Shaka Jf ndo familia yako sasa. Usikubali kufa na tai shingoni mama........ Leo wangesikia umeji nyonga kwa hali ngumu ya maisha wangekusema sana....... Pole kwa yote.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…