Hongera sana mkuu kwa kumaliziwa deni. Kuja humu kuomba ushauri kuhusu matumizi ya hiyo pesa inaonesha ni kiwango ambacho haujawahi kushika kabla. Hili si jambo baya ila wengi katika nafasi kama yako hujikuta wanakimbia kufanya maamuzi harakaharaka na kupelekea kutofanya maamuzi mazuri.
Kama una kipato tayari kutoka sehemu nyingine na hauna shida ambayo inabidi itatulike haraka nashauri hiyo 200M itulie katika akaunti kwanza kwa at least mwezi mmoja ili akili na mwili wako uzoee pesa. Usinunue chochote na usimuambie yeyote ambaye si lazima ajue. Huo ni muda wa wewe kuzoea hali yako mpya na kuondoa maamuzi ya papara ambayo nayaona hapa.
Baada ya mwezi au muda wowote ambao utaacha kuangalia balance ya akaunti yako kila saa na ukiangalia hautetemeki hela nyingi basi ndio unaweza kupanga mambo yako.
Interest zako naona ni nne. Moja ni nyumba, pili ni biashara, tatu ni gari na nne ni pesa ya kutumia.
Kwa ushauri kwenye gari iwe hadi 20M max. Hii ni bidhaa inayoshuka thamani utapoinunua tu. Pia wengi wanadhani gharama ni gari tu ila kiuhalisia kuna vitu vingine kama bima, service na mafuta. Ni uamuzi mzuri kuingiza mambo haya gharama yake kwa mwaka wa kwanza katika gharama ya gari pia so kiuhalisia gari yako itacost maximum ya 22M - 24M kwa mwaka mzima hapa ukijumuisha na bei ya kununua. Hii ni asilimia 10 hadi 12 tu ya pesa iliyopo hivyo unabaki na wigo mkubwa wa matumizi mengineyo.
Kwenye nyumba kwa kuwa umeanza tayari na umesema unakaribia kuanzisha familia hamna neno kutumia hiyo 40M kukamilisha jambo hilo. Ila kitu cha kutambua katika ujenzi ni kuwa ni nadra sana vitu kuingia katika bajeti labda kama cost analysis imefanywa na mtaalam ambaye ndie anakujengea pia. Kama hauna huyu basi ni vema kuandaa kiwango cha zaidi kidogo. Kwa hapa tuseme itatumika 50M jumla.
Biashara. Hapa nasisitiza sana usiparamie vitu ambavyo hauvielewi. Chukua muda na fikiria na kama kitu haujui kabisa basi omba ushauri NA USIMAMIZI (mentorship) kutoka kwa mtu ambae anakifanya vizuri tayari. Ila formula yangu ni kutafuta jambo ambalo unalielewa tayari au upo karibu nalo tayari na jenga biashara kulizunguka. Mfano architect akianzisha hardware haitasumbua sana. Logistics manager akinunua daladala au malori atayaelewa haraka na kadhalika kwa formula hii. Kama hauna kabisa kitu kama hiki basi fuata jambo la kwanza ambalo nimelitaja kwa kujifunza na kuanza kwa kiwango kidogo kinachowezekana. Sawa itachukua muda zaidi kufanikiwa ila itakuwa mafanikio ya uhakika. Kulingana na aina ya biashara na iwapo utafeli katikati na ikabidi uanze tena kiwango cha 70M kitafaa.
Hela ya kutumia. Weka 10M katika akaunti ya kawaida, ishi maisha si kwa anasa bali kwa umakini. 200M si pesa nyingi kuliko inavyoweza kuonekana kwa haraka. Inaweza kuisha haraka usipokuwa makini ukizingatia hii ni pesa ya mara moja. Jitahidi usizidi 1.5M kwa mwezi ili upate muda wa kutosha (miezi 6) mpaka mipango yako ya biashara ifanikiwe au iweze kusimama na kukulipa.
Itabaki 50M hii weka katika mfuko wa UTT Amis Liquid Fund. Mfuko unadhaminiwa na serikali na unainvest mainly katika bond za serikali ila unakupa uhuru wa kuingiza interest kwenye pesa yako bila kukuondolea uhuru. Average interest rate kwa mwaka ni 11% hivyo utakuwa unaingiza 5.5M hadi 6M kwa mwaka ambayo ni kama 450k hadi 500k kwa mwezi. Kwa kuwa hauna ulazima nayo basi unaweza kuiacha tu humo iendelee kuzalisha inakuwa kama backup yako. Ukiiacha humo bila kuigusa after 10 years utakuta 150M unagonga 40 years na kibubu kizuri huku biashara zako zinakufanyia mambo mengine. Kumbuka kuwa UTT Amis Liquid Fund interest inaongezwa kila siku na pia unaweza kudeposit na kuongeza pesa muda wowote hivyo kama biashara imetiki unaweza ongeza pesa humo pia kama kwa kupeleka hakuna tena.
Ukicheza karata zako vizuri kwa miaka 10 ijayo utagonga 40 years old na net worth ya 1 billion Tanzanian shillings plus. Hapo ndio unaweza anza kula bata nzuri nzuri kidogo.