Ninaomba ushauri kwa haya mapendekezo ya 200M

Ninaomba ushauri kwa haya mapendekezo ya 200M

Habari wakuu nisiwachoshe naombeni ushauri kwa mpangilio huu nilio upanga baada ya kulipwa pesa zangu nilizo fwatilia kwa mda mrefu kiasi cha shilingi 200M.
Nimepanga kama ifuatavyo
1.40M kujenga nyumba ya ndoto zangu
2.40M nimeweka kwaajili ya kununua usafiri gari
3.20M kwajili ya matumizi binafsi ya hapa na pale
4.100M Biashara ambapo nimegawa kama ifuatavyo
1.30M nataka kufungua Pharmancy mkoani
2.20M wakala Mpesa, tigo, na bank
Then Hii 50M bado inahang hang sijaipatia nini cha kufanya naombeni ushauri na kuboresha wapi na wapi.
Kwa vile wewe ni mstaafu. Usifanye vitu vya kukupa stress. Naboresha kidogo:
1.40M kujenga nyumba ya ndoto zangu
2. 15 M nunua usafiri gari IST inakufaa
3.20M kwajili ya matumizi binafsi ya hapa na pale
4.100M Biashara ambapo nimegawa kama ifuatavyo
41. 60 M Jenga vi apartments vitatu vya machelor master, chumba, sebule, jiko

2. 40M Peleka BOT kanunue Govt Bonds za maturity ya 25 years
 
Anzisha uzi wenye lengo la kutoa zawadi ya 500K kwa kila mtu kwa watu 10 watakaotoa ushauri bora wa namna ya kuzitumia ikiwemo kuwekeza hizo pesa. Toa nafasi kwa wadadu hapa JF wapige kura kuchagua maandiko bora 10 ya kiushauri.

Kutoa 500K kwa kila mtu kwa watu 10 ambapo jumla yake ni 5M ili kupata mawazo bora ya kutumia 195M zilizobakia si jambo sana katika 200M ulizonazo.

I promise you; utapata ushauri bora sana ambao hautajutia.

Hiyo pesa inabidi uikabidhi mfano JF ili usije ukabadili maamuzi ukashindw kuzitoa baada ya shindano hilo.

Mwisho: Ili upate vitu bora sharti utumie gharama ama ya fedha au vyovyote vile. Usitegemee vitu vizuri kwa njia rahisi sana. Simaanishi kuwa haiwezekani kupata ushauri bure ila imewahi kusemwa hata huko nyuma kwamba "ukitaka kula sharti uliwe". Mambo mazuri yana gharama yake Mkuu.
 
Anzisha uzi wenye lengo la kutoa zawadi ya 500K kwa kila mtu kwa watu 10 watakaotoa ushauri bora wa namna ya kuzitumia ikiwemo kuwekeza hizo pesa. Toa nafasi kwa wadadu hapa JF wapige kura kuchagua maandiko bora 10 ya kiushauri.

Kutoa 500K kwa kila mtu kwa watu 10 ambapo jumla yake ni 5M ili kupata mawazo bora ya kutumia 195M zilizobakia si jambo sana katika 200M ulizonazo.

I promise you; utapata ushauri bora sana ambao hautajutia.

Hiyo pesa inabidi uikabidhi mfano JF ili usije ukabadili maamuzi ukashindw kuzitoa baada ya shindano hilo.
Kwa upande wangu only 10M out of 195M zingemtosha na angeishi maisha murua
 
Habari wakuu nisiwachoshe naombeni ushauri kwa mpangilio huu nilio upanga baada ya kulipwa pesa zangu nilizo fwatilia kwa mda mrefu kiasi cha shilingi 200M.
Nimepanga kama ifuatavyo
1.40M kujenga nyumba ya ndoto zangu
2.40M nimeweka kwaajili ya kununua usafiri gari
3.20M kwajili ya matumizi binafsi ya hapa na pale
4.100M Biashara ambapo nimegawa kama ifuatavyo
1.30M nataka kufungua Pharmancy mkoani
2.20M wakala Mpesa, tigo, na bank
Then Hii 50M bado inahang hang sijaipatia nini cha kufanya naombeni ushauri na kuboresha wapi na wapi.
Hamna biashara tamu na haina usimamizi mkubwa Kama biashara ya usafirishaji. Hiyo nyumba Jenga ingawa usiiweke ya kisasa sana kupunguza gharama maximum iwe 30 na si 40 million.
Kwenye usafirishaji unaweza kununua coaster 2 za kawaida kwa milioni 70 had 80 na ukazipa ruti nzuri na Kila siku unapata kipande elfu 80 Hadi laki kwa siku. Kwa magari 2 ni laki na 80 Hadi laki 2. Kila mwez unakula milioni 5 Hadi 6.
Au nunua vigari vidogo Kama vitz, ist au sienta. Bajeti ya milioni 10 had 11 kwa gari kwa gari 8 ni milioni 80 had 88. Kila gari unaisajili bolt na Uber Kila siku inaleta elfu 25 mara magari 8 ni laki 2 kwa siku kwa mwez ni milioni 5 had 6. Usisahau kukatia gari bima kubwa. Hela zilizobaki weka fixed deposit.
 
Kwa huku mkoani hiyo cash inatosha kuanzisha shule yako kbs.Kinachofuatia hapo ni kula miada tu kwa kwenda mbele.Ukivutiwa na wazo Hili waweza uliza zaidi usaidiwe.
 
Unafilisika mkuu Yan huachi akiba ningekua mie ndio ww ml 100 ningeweka fixed ac ya miaka miwili hiyo ngine ningefanyia matumizi mengine

100mil 2yrs fixed account unalipwa tsh ngap?...
 
Chief wekeza kwenye real estate hio pesa faida yake utafanywa vurugu zote mjini na mtaji upo pale utajenga nyumba,utanunua usafiri,utafungua zipu na chupa za bia na ofisi still inatembea huku ukifungua KILA aina ya biashara uitakayo.
Real estate haina hasara Wala pressure we ni kula tu pesa zinaingia.
Hio 200 inazaa bilioni moja kwa mwaka.
Tuelekeze na sisi kidogo kuhusu hio real Estate mkuu?
 
Unafilisika mkuu Yan huachi akiba ningekua mie ndio ww ml 100 ningeweka fixed ac ya miaka miwili hiyo ngine ningefanyia matumizi mengine

Hakuna biashara ya kijinga Kama kuweka fixed mzee bora ununue ata mazao fixed kwa mwaka nliweka 10m nikapata lak tano so kwa 100m ni 5m Sasa si ujinga huo mzee
 
Wazo langu ni kwa yule ambae amepata hela kwa mara ya kwanza na hajawah kushika hcho kiasi

Pesa nyingi ina tabia ya kuzuzua akili na kila wazo utakalopewa utaona linafaa so kwako inabd utulize sana kichwa

Kama sina cha kufanya kichwan kwa Muda huo naweza kuchagua kununua government bonds kutegemea na muda.

Ila kwa kuanzia miaka 10 na kuendlea rate yake inarange kati ya 10% - 15%

So kwa rate ya 15% una uhakika wa kupata angalau 30M kwa mwaka ambayo utalipwa mara 2 kwa mwaka

so unaweza kupokea 15M kila baada ya miez sita ukawa unajipanga tarabu kufanya mambo yako bila presha

Baada ya muda kuisha unaenda kuchukua 200M yako japokua haitakua na thaman sawa na sasa ila haiwezi kuwa ndogo.
 
Me nakushauri fungua duka la vifaa vya ujenzi yani hardware then simama apo mwenyewe hayo mengine yote achana nayo utakuja kunishukuru baadaye.usifungue biashara nyingi kwa wakati mmoja utakula hasara ambayo hujawai iona
 
Hamna biashara tamu na haina usimamizi mkubwa Kama biashara ya usafirishaji. Hiyo nyumba Jenga ingawa usiiweke ya kisasa sana kupunguza gharama maximum iwe 30 na si 40 million.
Kwenye usafirishaji unaweza kununua coaster 2 za kawaida kwa milioni 70 had 80 na ukazipa ruti nzuri na Kila siku unapata kipande elfu 80 Hadi laki kwa siku. Kwa magari 2 ni laki na 80 Hadi laki 2. Kila mwez unakula milioni 5 Hadi 6.
Au nunua vigari vidogo Kama vitz, ist au sienta. Bajeti ya milioni 10 had 11 kwa gari kwa gari 8 ni milioni 80 had 88. Kila gari unaisajili bolt na Uber Kila siku inaleta elfu 25 mara magari 8 ni laki 2 kwa siku kwa mwez ni milioni 5 had 6. Usisahau kukatia gari bima kubwa. Hela zilizobaki weka fixed deposit.
80M ukituliza akili na ukatumia wataalam, utapata tipper moja mbichi sana.. isifanye kazi dar! 300k, 400k ni za kufikia kila siku gari ikiwa barabarani..
 
Hongera sana mkuu kwa kumaliziwa deni. Kuja humu kuomba ushauri kuhusu matumizi ya hiyo pesa inaonesha ni kiwango ambacho haujawahi kushika kabla. Hili si jambo baya ila wengi katika nafasi kama yako hujikuta wanakimbia kufanya maamuzi harakaharaka na kupelekea kutofanya maamuzi mazuri.

Kama una kipato tayari kutoka sehemu nyingine na hauna shida ambayo inabidi itatulike haraka nashauri hiyo 200M itulie katika akaunti kwanza kwa at least mwezi mmoja ili akili na mwili wako uzoee pesa. Usinunue chochote na usimuambie yeyote ambaye si lazima ajue. Huo ni muda wa wewe kuzoea hali yako mpya na kuondoa maamuzi ya papara ambayo nayaona hapa.

Baada ya mwezi au muda wowote ambao utaacha kuangalia balance ya akaunti yako kila saa na ukiangalia hautetemeki hela nyingi basi ndio unaweza kupanga mambo yako.

Interest zako naona ni nne. Moja ni nyumba, pili ni biashara, tatu ni gari na nne ni pesa ya kutumia.

Kwa ushauri kwenye gari iwe hadi 20M max. Hii ni bidhaa inayoshuka thamani utapoinunua tu. Pia wengi wanadhani gharama ni gari tu ila kiuhalisia kuna vitu vingine kama bima, service na mafuta. Ni uamuzi mzuri kuingiza mambo haya gharama yake kwa mwaka wa kwanza katika gharama ya gari pia so kiuhalisia gari yako itacost maximum ya 22M - 24M kwa mwaka mzima hapa ukijumuisha na bei ya kununua. Hii ni asilimia 10 hadi 12 tu ya pesa iliyopo hivyo unabaki na wigo mkubwa wa matumizi mengineyo.

Kwenye nyumba kwa kuwa umeanza tayari na umesema unakaribia kuanzisha familia hamna neno kutumia hiyo 40M kukamilisha jambo hilo. Ila kitu cha kutambua katika ujenzi ni kuwa ni nadra sana vitu kuingia katika bajeti labda kama cost analysis imefanywa na mtaalam ambaye ndie anakujengea pia. Kama hauna huyu basi ni vema kuandaa kiwango cha zaidi kidogo. Kwa hapa tuseme itatumika 50M jumla.

Biashara. Hapa nasisitiza sana usiparamie vitu ambavyo hauvielewi. Chukua muda na fikiria na kama kitu haujui kabisa basi omba ushauri NA USIMAMIZI (mentorship) kutoka kwa mtu ambae anakifanya vizuri tayari. Ila formula yangu ni kutafuta jambo ambalo unalielewa tayari au upo karibu nalo tayari na jenga biashara kulizunguka. Mfano architect akianzisha hardware haitasumbua sana. Logistics manager akinunua daladala au malori atayaelewa haraka na kadhalika kwa formula hii. Kama hauna kabisa kitu kama hiki basi fuata jambo la kwanza ambalo nimelitaja kwa kujifunza na kuanza kwa kiwango kidogo kinachowezekana. Sawa itachukua muda zaidi kufanikiwa ila itakuwa mafanikio ya uhakika. Kulingana na aina ya biashara na iwapo utafeli katikati na ikabidi uanze tena kiwango cha 70M kitafaa.

Hela ya kutumia. Weka 10M katika akaunti ya kawaida, ishi maisha si kwa anasa bali kwa umakini. 200M si pesa nyingi kuliko inavyoweza kuonekana kwa haraka. Inaweza kuisha haraka usipokuwa makini ukizingatia hii ni pesa ya mara moja. Jitahidi usizidi 1.5M kwa mwezi ili upate muda wa kutosha (miezi 6) mpaka mipango yako ya biashara ifanikiwe au iweze kusimama na kukulipa.

Itabaki 50M hii weka katika mfuko wa UTT Amis Liquid Fund. Mfuko unadhaminiwa na serikali na unainvest mainly katika bond za serikali ila unakupa uhuru wa kuingiza interest kwenye pesa yako bila kukuondolea uhuru. Average interest rate kwa mwaka ni 11% hivyo utakuwa unaingiza 5.5M hadi 6M kwa mwaka ambayo ni kama 450k hadi 500k kwa mwezi. Kwa kuwa hauna ulazima nayo basi unaweza kuiacha tu humo iendelee kuzalisha inakuwa kama backup yako. Ukiiacha humo bila kuigusa after 10 years utakuta 150M unagonga 40 years na kibubu kizuri huku biashara zako zinakufanyia mambo mengine. Kumbuka kuwa UTT Amis Liquid Fund interest inaongezwa kila siku na pia unaweza kudeposit na kuongeza pesa muda wowote hivyo kama biashara imetiki unaweza ongeza pesa humo pia kama kwa kupeleka hakuna tena.

Ukicheza karata zako vizuri kwa miaka 10 ijayo utagonga 40 years old na net worth ya 1 billion Tanzanian shillings plus. Hapo ndio unaweza anza kula bata nzuri nzuri kidogo.
 
Dah...ukiungana na mm nakupeleka kwenye u billionaire chap. Fanya kunitimbia inbox!

Hio hela kwa kila mwezi unaweza kuzalisha sh mil 30 net; kwa mwaka unakunja sh mil 360 net

Hajasema anataka Crypto forex mzee[emoji23]
 
Back
Top Bottom