ubuntuX
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 1,977
- 2,200
Heshima kwenu wakuu,
Mimi naomba tutumie Mnakasha huu kutoa mwanga kwa Serikali na Jamii kwa Ujumla nini kifanyike ili kukomesha vitendo Vibaya vinavyoendelea Pwani. Pwani: Wawili wahofiwa kuuawa kwa risasi Kibiti, idadi ya Waliokufa inasikitisha, sasa yatosha
Mimi kwa mawazo yangu, nahisi huenda vyama vya upinzani hapa nchi vinajua kiini cha mauaji yaliyotokea na yanayoendelea huko mkoani pwani hususani mkuranga na kibiti, hii ni kutokana na nature ya matukio yenyewe kwani yanaitikadi za kisiasa wanaouliwa ni watu toka chama tawala na serikali kwa ujumla wake huku vyama vya upinzani vikiwa salama kabisa.
Kamanda Sirro kachukua hatua nzuri kabisa ya awali lakini zaidi ili kupiga hatua kubwa kuyakomesha na kumaliza majambazi haya ni kuushirikisha upinzani tanzania!
Sirro kaa na wapinzani watakuambia kwanini wanauliwa viongozi wa CCM na Serikali kwa ujumla wake!
Hii itakupa abc pa kuanzia hata kama wao sio wahusika wa moja kwa moja.
Mimi naomba tutumie Mnakasha huu kutoa mwanga kwa Serikali na Jamii kwa Ujumla nini kifanyike ili kukomesha vitendo Vibaya vinavyoendelea Pwani. Pwani: Wawili wahofiwa kuuawa kwa risasi Kibiti, idadi ya Waliokufa inasikitisha, sasa yatosha
Mimi kwa mawazo yangu, nahisi huenda vyama vya upinzani hapa nchi vinajua kiini cha mauaji yaliyotokea na yanayoendelea huko mkoani pwani hususani mkuranga na kibiti, hii ni kutokana na nature ya matukio yenyewe kwani yanaitikadi za kisiasa wanaouliwa ni watu toka chama tawala na serikali kwa ujumla wake huku vyama vya upinzani vikiwa salama kabisa.
Kamanda Sirro kachukua hatua nzuri kabisa ya awali lakini zaidi ili kupiga hatua kubwa kuyakomesha na kumaliza majambazi haya ni kuushirikisha upinzani tanzania!
Sirro kaa na wapinzani watakuambia kwanini wanauliwa viongozi wa CCM na Serikali kwa ujumla wake!
Hii itakupa abc pa kuanzia hata kama wao sio wahusika wa moja kwa moja.
Kila jambo lina asili yake(chanzo) kisha mwendelezo.....mauaji mkoa wa pwani kwa upande wa Rufiji hayakuanza leo! Lakini pia yamekuwa ni mauaji ya namna yake. .kwa sehemu kubwa si ujambazi, ni mauaji ya chuki na visasi
Ni kama vile wauaji wana mpango uliokamilika
-walianza kuwaondoa informers wa serikali kujisafishia njia
-wakaingia kwenye uporaji mkubwa wa silaha, sasa wana stock ya kutosha
-wakaingia kusafisha viongozi wa serikali na kisiasa
- sasa ni walinda usalama wetu
-wamechagua uwanja wa vita mzuri sana kwao! Wanaweza kufanya lolote na kuondoka kwa usalama kabisa
Jeshi la polisi lisikurupuke kwenye hili kwa kupeleka majeshi na kwenda kuwaumiza wananchi waso hatia. Wauaji hawaishi kule ,ni wakuja wakafanya yao na kuondoka! Hebu waangalie haya
1. Hakuna kituo cha polisi ukitoka kimanzichana mpaka kibiti(sasa hivi kimejengwa mkiu kwa maslahi ya mwekezaji)
Kunapaswa kuwa na vituo viwili full equipped kimoja kiwe Bungu njiapanda ya Nyamisati na kingine kiwe kabla ya kufika nyamisati (njiapanda ya gezani)
Hili lote ni eneo lenye mapori makubwa na njia nyingi za panya kuelekea baharini kwenye makumi ya bandari bubu
Kunapaswa kuwa na kituo kingine Nyamisati tena chenye mawasaliano ya radar, Nyamisati ni bandari kamili inayopokea na kupeleka watu sehemu mbali mbali kama Zanzibar Pemba Mafia Tanga Mombasa mpaka Madagascar nk NB. Baadhi ya route sio rasmi ..hapo hakuna uangalizi wowote wa maana zaidi ya askari wa marine kwa ajili ya kulinda mikoko na magendo
Eneo la uchumi na biashara pia liangaliwe vema! Wananchi wengi wa eneo la kibiti na maeneo yake kuanzia Jaribu wanaishi kwa uvuvi kilimo na biashara
Kuna uonevu mkubwa rushwa na ubabe unafanywa na viongozi wa serikali na polisi wanapowakamata wananchi na makosa madogodogo wakiwa na bidhaa zao ambazo soko kubwa ni Dar....wanahitajika viongozi wenye upeo na weledi mkui maeneo Yale
Mbaya zaidi mali na bidhaa zao zinapokamatwa huishia kutaifishwa na wao kutoa rushwa na baadae hiyo mali kuuzwa tena na haohao wakamataji na kufanya maendeleo yao! Hii inawakera mno wananchi
Eneo la jiografia na miundombinu. Kuanzia Njopeka mpaka Kibiti kuna mamia ya vichochoro vinavyotokea baharini kwenye makumi ya bandari bubu.
Nyamisati yenyewe imezungukwa na visiwa vidogovidogo si chini ya 20 vingine vinaishi watu vingine haviishi watu ila ni maficho na maghala ya majambazi na magendo. Kuna mamia ya njia za majini kuvizunguka hivyo visiwa ambazo hazina udhibiti wa serikali
Hivi visiwa na hizi barabara kwa sehemu kubwa ni hifadhi ya misitu ya mikoko hivyo kufanya hilo eneo kuwa la kutisha mno. Jeshi la polisi limewataja baadhi ya watuhumiwa kuwa wanatoka visiwa vya Saninga na Simbaulanga....
Simbaulanga ni kisiwa kikubwa na ndio kama mdomo ama njia ya kuchepukia baharini... Hapa kuna boat na majahazi mengi ya kuna na kwenda Pemba Tanga nk daily..View attachment 529115ramani hii inaonyesha visiwa na njia kubwa tu lakini kuna visiwa vingi zaidi na barabara nyingi zaidi
Matatizo ya kisiasa Zanzibar yanaweza kuwa na mkono kwenye hili kutokana na aina ya watu wanaouawa. Jiulize anakuja kuuliwa mtu Bungu Jaribu Njopeka ama Kibiti lakini si Kilwani Gezani Nyamisati nk nk. Kabla ya kupeleka majeshi yetu hebu tutafakari haya
Njia za majini kwenye hifadhi ya mikoko Nyamisati
Habari ya weekend wakuu,natumai tu wazima,haya ni mawazo yangu tu ambayo nafikiri kila siku kuhusu hili swala la mauaji kibiti,
Kwanza kabisa naomba kumpongeza kamanda siro kwa jitahada zake anazozionesha kila siku,lkn akumbuke anacheza na watu wenye mtandao mkubwa sana na hapa ndipo anashindwa kuwakamata kwa connection zao,
Tushajua target ya wauwaji ni ipi,ni wanachama flan na viongozi wa chama na kijiji pamoja na askari wetu,ombi langu kwako kamanda siro,kwanza police wako wa huko kibiti hutakiwi kuwaamini kabisa,inawezekana plan zenu zinavuja kutoka kwao,na si rahisi mauaji hayo yafanyike bila ya wao kuwa na watu wa kuwapa information kua leo doria tupo wap nyie kauweni wapi,
Kama ingekua inawezekana kabisa jeshi lote la police huko litoke kwa muda libadili kituo kwa muda ulipeke hata huko sumbawanga then sumbawanga walete kibiti,au jeshi lote la police kibit lipe likizo hata miezi miwili alaf pachika kikosi kipya na ikiwezekana weka hata makomando wa jw wavalishe sare za police wapige kazi,
Na pale kibiti usiamini mtu yoyote nyie mwende nyatu nyatu tu,hao watu mtashika kama kuku,police mishahara yao laki4, anaambiwa tupe information ya doria yenu then tutakupa kwa kila siku 1m,unadhan police hatosariti? Police wetu na wao ni binadam wanapenda maisha mazur kwa dau kama hilo hawawezi chomoa,
Kingine dau ulilotoa nadhani ungeongeza kidogo,naamini wauwaji wananchi wanawajua Ila police hawaaminiki unaweza kutoa taarifa wakakuchoma na kwa hiyo 10m uliyotoa haiwezi kumpeleka popote mtoa taarifa,weka hata 50m ili hata mtu akitoa taarifa anaondoka mazima kwa usalama wake anaenda kutafuta maisha pengine na kujipanga upya kwa maisha mapya,mikoani million 20 anapata nyumba nzuri na hiyo 30 inayobaki anafanya mengine yakumuingizia kipato.
Kwenye target ya wauwaji wekeni usalama wa kutosha,kila sehemu wekeni hata police wapelelezi,wananchi wanavamiwa na kutekwa sababu hawawezi kujitetea kwenye bunduki,lkn mkipandikiza wanakijiji fake ni rahisi kuwakamata sababu watakua na information yoyote kua Nini kinaendelea,majambaz wanakuja kufanya ambushi wanakipata cha mtema kuni.sasa hivi hali itazid kua ngumu kwenu sababu taarifa zinatoka.
Maisha ya wananchi in zaidi ya hilo dau,kumbuka hao wanao uwawa kuna familia/ndg/watoto wanawategemea,hivyo wanafanya familia kua ombaomba wanakuja na wao kuwa majambazi wa baadae,usiamini mtu kamanda ktk hilo,
NAWASILISHA
Kwa jinsi mauaji yanavyofanyika mkoa wa Pwani nadhani ni ujumbe mzito kwa Serikali toka awamu ya nne.
Wauaji wanaua Polisi,Mgambo,viongozi w Serikali za mitaa na viongozi wa CCM tu na hawagusi kabisa wake zao wala watoto wao wala ndugu wa familia zao.
Kwa mtazamo wangu hapa Kuna kazi kubwa ya kufanya kujua root cause lakini sidhani kabisa kama ni uhalifu kama nilivyoeleza ktk kichwa cha mada.
Wauaji wameamua kuchagua eneo la mkoa wa Pwani kutokana na jiografia yake ilivyo ikiangalia Mkuranga,Kibiti na Ikwiriri ni rahisi sana watu wenyewe nia mbaya kutua kimkakati kufanikisha nia yao.
Serikali Inahitaji intelejensia ya ziada kapata root cause.
IGP kutangaza 10 mil hakuna atakayeichukua kwasababu hakuna atakayekubali kuuwawa kwa 10mil kutokana na wapewa siri kutotunza siri.
IGP tuko Pamoja ila Kuna kazi ya ziada fikiria Nje ya Pwani Kuna uwezekano ndiyo root cause.
Majeshi mengi yaliyopo Pwani hayatasaidia Kitu kwasababu wanapigana na invisible killers.
Kitendo cha CCM kuanza kunadi majukwaani kuwa matukio ya mauaji yanayoendelea huko ni ya kisiasa hakika tumefeli kabisa, na Tatizo hili tutapata taabu kulimaliza.
Tunashindwa kujiuliza hata kama lingekuwa na uhusiano Wa kisiasa iweje yatokee huko Pwani peke yake? inamaana mikoa au maeneo mengine hao viongozi wa CCM hawapo?
Hapa tumeshindwa kumtarget adui, adui wetu katupiga Chenga sasa tutegemee mwendelezo Wa mauaji huko Pwani.
Bila shaka wauaji huko waliko wanashangilia kwa kuwa tunashindwa kudeal nao.
nawasilisha!
Watu wasiojulikana" wapewe fursa kutoa taarifa pwani.
Kumekuwa na changamoto za kiusalama mkoa wa pwani ambapo tumesikia mara nyingi kwenye vyombo vya habari kuwa watu wasiojulikana wametekeleza uhalifu huo na kutokomea kusikojulikana katika pita pita mtaani nimegundua kuna watu wanaweza kuwa na taarifa muhimu za kufanikisha kujulikana kwa hawa watu wasiojulikana ila nao hawataki kujulikana.
IGP alitoa namba zake za mkononi na kuahidi 10m kwa yeyote mwenye taarifa sahihi ila kiukweli kuna watu wanahofia kujulikana kwa sababu watakuwa wanawataja watu ambao hawataki kujulikana.....wenu nisiyejulikana
Kwanza poleni wafiwa wote kwa waliyowakuta.
Mimi ni mtanzania halisi. Kwanza naona mkuu/Magufuli sio mkali. Nashauri Raisi wa jamuhuri achukue maamuzi magumu kuhusu hili suala,kuna mtu mmoja ametoa wazo kuwa kutotangaza nini kinachondelea huko Kibiti,nathani ni wazo safi kabisa.
Pili,Nashauri wasombwe wanaume wote katika vijiji hvyo watasema tu wapi wanaficha silaha na mambo mengine. Serikali itapoteza muda mwingi sana kuinflitrate ndani ya hao magaidi na kujua ajenda yao.
Dawa ni kufagia nyumba baada ya nyumba. Hii ni Tanzania sio Rwanda wala Uganda. Amani tutailinda kwa gharama yoyote ile hata ikiwa damu ya wengi kwa wachache hakuna jinsi. Lazima hawa watu wajue kuw hii ni nchi na tuko imara.
Asanteni.
Ndugu zangu watanzania,
Hili siyo jambo la mzaha tena, kipenga kimelia, wauaji wapo kazini, ni wauaji hatari Sana ambao ni well trained kabisa. Kama ni ugonjwa hii ni cancer iliyokomaa au virus hatari, moto huanza na moshi, na kisha moto mkali hushika kasi, haya mauaji yanatisha na si ajabu yasipothibitiwa mapema yatasambaa nchi nzima.
Kuna tukio la kutisha liliwahi kutokea sehemu moja hapa Tanzania (jina la mkoa naihifadhi) kuna vijana flani walikuwa wakifanya kazi kwenye kampuni flani, kumbe walikuwa na mahusiano na alshababu pamoja na ISS, walikuwa wakisali ktk nyumba moja ya ibada yenye itikadi kali sana.
Siku moja usiku kwa nyakati tofauti wakavamiwa na Maafisa usalama wa serikali na wakati wakitaka kuwatia nguvuni mmoja wao alijaribu kupambana na Maafisa Usalama akijihami kwa karate, lakini walimdhibiti na kuwakamata wote, ndo ujue kumbe serikali inaweza na ipo kila kona.
Maana haikuwa rahisi kuwabaini wale jamaa lakini serikali iliweza, sasa kama waliweza Kwa wale watu ambao hatukuwajua, kwa nini ya pwani yanawashinda? Na Kama mambo yamekuwa magumu kiasi hiki basi Waombe msaada Haraka kutoka mashirika ya kijasusi yaliyobobea, tutauawa hadi lini?
Hakuna aliye salama mikononi mwa wauaji katili wale, hii ni Vita yetu sote na ndo maana nishauri serikali iombe msaada wa haraka, police wengi walipelekwa huko mauaji hayajaisha, kuna tetesi Wanajeshi nao wapo huko, niliwahi kushauri hapa kuwa lundo la askari haisaidii chochote huko kwa wauaji hatari kama hao ambao inakuwa ngumu kuwatambua.
Njooni FBI, MI5, Scotland yard na Mossad mtusaidie tunakwisha huku.
Vyombo vya ulinzi vinahitajika kutulia sana na kutafuta - Moja ! wauaji, sababu za mauaji kwa kina na kukamata watu sahihi sio kama kaiwada ya kutumia upepelezi hafifu au vitisho.
Hawa wauaji wameonyesha kabisa hawaogopi maneno ya vitisho au uwepo wa majeshi na silaha kali mitaani.
Naomba vyombo vya ulinzi na usalama visiwatishe raia wema au kuwaogofya kama ilivyotokea miaka ya nyuma , wakitumia vitisho watasomba wasio na hatia na kuwaacha wauaji mitaani, misituni, baharini etc.
Kazi kubwa ilitakiwa upeplelezi ujue ni kitu gani kinawafanya wauaji kuuwa bila kuiba, kwanini wanaua wengi ni watumishi wa umma au watendaji?
Je wananchi wa sehemu husika wanamahusiano gani na watendaji hawa?
Je waliouwawa walikuwa na ugomvi na watu au wananchi ?
Je utendaji wao wa kazi ulikuwaje?
Je wananchi wanaowaonaje hawa watendaji na watumishi wa umma?
Je kweli wauaji wanatoka kati ya jamii husika ?
Ni kweli mauaji yanauhusiano na jamii husika ?
Ni muda wakutumia akili sio nguvu mabavu wala uwepo wa polisi na wanajeshi wenye silaha mitaani na kutisha raia.
Pattern ya haya mauji ni vigumu sana kuyatatua kwa kutumia mbinu nyepesi za kila siku.
[HASHTAG]#Haki[/HASHTAG] ni tunda la amani
Mimi sio mtaalamu wa maswala ya upelelezi hata hivyo nina ushauri huu mdogo tu kwenu nyini wahusika wa mambo haya.
Nawashauri mchukue askari vijana/wenye umri wa makamu ni kisha muwapeleke katika haya maeneo lakini wakienda katika maeneo hayo kama wananchi wa kawaida wanaotafuta maisha tena ikibidi waende kule wakiwa na muonekana kama watu wenye shida sana kimaisha.
Askari hawa/watu wa usalama waende wakapange na kuishi maeneo ya huko kama watu wanaofanya biashara ndogo ndogo au watu wanaosaka vibarua,n.k.
Wakiwa huko wajenge mahusiano na wananchi wa kawaida then kupitia story za vijiweni,mitaani na hata kwenye vilabu vya pombe wanaweza kupata information zitakazoweza kusaidia kuwabaini wahusika iwapo wauaji hawa wanaishi/wanahifadhwa na raia wengine katika maeneo haya yenye mauaji.
Hii inaweza kuwa ni mbinu mojawapo sambamba na mbinu zingine za kiuchunguzi.
Ni ushauri tu.