Ninakuja Tunduma kuanza maisha upya

Ninakuja Tunduma kuanza maisha upya

Pole sana kwa Changamoto hizo. Vijana Wengi tunaoa Kwa Kufuata Jamii sana zaidi ya Uchunguzi

1. Mtu anaoa kisa kapata Kazi nzuri
2. Mtu anaoa kisa kapata Sehemu ya Kujishikisha hata kama Si permanent
3. Mtu anaoa kisa Kampa Binti wa Watu Mimba
4. Kuna Wanawake/Wanaume wameshalaaniwa na Mababu zao wasifanikiwe na Atakayeishi naye pia Asifanikiwe hivyo hivyo. Sasa Msipowachunguza vizuri ndio hivyo tena unaharibikiwa

Sometimes ni Vyema Tukamjua Mtu tunayemuoa kuliko Kuoa kisa Wewe mambo yako yamekunyookea
Unatakiwa kuoa ukiwa hauna kitu, unalala chini, unapanga akikubali kwa umaskini wako huyo ndio mke
 
Mi mwanamke aliapa kunifunga kbs kuna sku tuliznguana usku akaenda polisi akafungua file eti nimempga na kumjeruhi mkono asubuhi karud na polisi wakanikamata wkt tupo njian akawa anaropoka lazma anifunge tu maafande wakawa wanamwambia aachane na huo mpango akagoma, kufka kwa mpelelez nakuta kesi ya uwongo eti ya kujeruhi wkt hata skumpga wala kumjeruhi akafuta kesi
 
Maisha Yana ups n down napitia kipindi kigumu Sana iko hivi nlifunga ndoa tar 17/11/2020 ndoa takatifu ya kikiristo na mwanamke mmoja ambaye nlishaishi naye kwa muda was miaka 6 kuanzia siku nimemuoa yaani Kila kitu kimeparaganyika Sana yaani Kila nkifanya biashara napata hasara ninadaiwa almost 1.8 na watu tofauti tofauti siishi kwa amani nyumbani kwangu kwakua mambo yameyumba ugomvi hauishi chakula kile kilichonifanya nioe sikipati kwa wakati mke tukikwazana kidogo tu anapiga simu kwao kuwa namnyanyasa simhudumii ( mke ni mfanyakazi) serikalini

Kubwa lililoniumiza nafsi ni maendeleo ya haraka haraka anayoyafanya mke wangu Ana Jenga nyumba ambayo me sijawahi Iona Wala kiwanja sijui kilipo! Nlijua baada ya kushinda nyumban siku moja na kuona diary yake yenye maelezo juu yatofali hell anazowapa mafundi na material ya ujenzi
Inapoelekea nyumba imefikia kwenye lenta
Kutokana na kuwa na hasira nlimpga ikawa ni kama nimeamsha yaliyolala alichofanya kiliniadhirisha Mara 2 ya nlivyokua mwanzoni

Naaandika nikiwa na uchungu mkubwa Sana na machozi yananitoka nahitaji kwenda mbali ambako nitaaanza upya nimwachie watoto vyombo na Kila kitu ninachomiliki hapa nitaondoka tu na pikipiki nguo pamoja na vyeti vyangu vya taaluma Nina stashahada ya ualimu kwa masomo ya geography na kiswahili kwa anayejua nnapoweza kuanza maisha nikiwa na amani anielekeze hata ikiwa kijijini ntashukuru

Nilipendelea Tunduma kwa kuwa Kuna mzunguko mkubwa was biashara kama nnavyosikia lakin kama mtu anaweza kunielekeza sehemu nyingine ntashukuru
pole sana. huyu mwanamke ni muuaji. iponye nafsi yako. as long as wewe si mvivu utatoboa tu. Uamuzi uliochukua ni sahihi kwepa kesi maana ibilisi anaweza akakuingia ukamtendea jambo baya. Tafuta mahali unapoona patakufaa kuanza maisha upya.
 
Back
Top Bottom