Ninakemea uongo, uzushi na fitna kwa Rais Samia. Wote mnaokosoa hamtafanikiwa

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,186
27,231
Leo imenibidi niliongee hili ili niae huru kwa maana moyo unauma kuona uongo uzushi chuki na fitna kwa Mama Samia.

Ninaona ni kama watu wamejipa ajira ya kudumu ya kukosoa maraisi. Kukosoa sio dhambi Ila inategemea na unachokosoa.

Hadi Sasa sijaona kama kuna jambo la kumkosoa Mama Samia, nasema SIJAONA KABISA.

Kuna watu pengine wanalipwa kwa kuikosoa serikali, hivyo serikali ifanye vizuri au vibaya wao wanakosoa tu.

Sasa jiulize unamkosoa mama Samia kwenye lipi? Ni kipi kakosea hadi Sasa hadi muanze midomomidomo?

Mara sijui kwa nini avunje vibanda, sasa kama kaona hawafati Sheria kwa nini asivunje?

Mtu anakurupuka anasema ooh kwa nini sijui kampa mwinyi gari, gari kweli? Tena kwa raisi mstaafu ni issue?

Wengine ooh sijui kasababisha mechi isichezwe? Akili za namna gani hizi? Ikatokea ukakutana na kibaka huko mtaani akakukaba utasema pia Mama Samia ndio kamtuma?

Hakuna mwenye hoja kabisa ya kukosoa zaidi ya ushabiki tu. Tuache ushabiki tuchape kazi.

Wanaojiita wanaharakati na yule jamaa yenu mliekuwa mnamuabudu kule Twitter nao kila siku wanatafuta kwa nguvu la kuzusha ili tu Mama Samia aonekane hafai, sijui wenzetu walisaini mikataba ya kukosoa serikali?

Unamkosoa Mama Samia kwa lipi baya? Acheni hizo, Ila tutaenda sawa maana kukosoa mnasema ni Uhuru wenu Ila hata sisi kuwakemea nyie ni Uhuru wetu.

Mama Samia kanyaga twende!

#kazi iendelee
 
Wewe unaona ni sahihi pesa ya umma kuchezewa? Rais mstaafu anatumia gari na kila kitu cha umma mpk atakapo kufa, kama alikuwa anapata shida gari ni ndefu kwanini asibadilishiwe au kununua yeye mwenyewe ama kununuliwa na mtoto wake?
 
Yeye ameruhusu kukosolewa,wewe shida yako nini? Hatuko enzi zile tena acha watu wamkosoe na utuondolee huo upumbavu uliobaki nao.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mosi Hebu tupe majina ya wanaolipwa kuikosoa serikali.

Pili tupe ushahidi wa kimaandishi kuonesha hayo malipo ya kuikosoa serikali yanatokea kwa nani kwenda kwa nani na kwa njia ipi ya malipo.

Tatu tupe mkataba unaoonesha namna wakosoaji wamepewa namna ya kukosoa na unadumu kwa muda upi maana ukosoaji uko duniani kote na hakuna asiyekosolewa.
 
Wewe unaona ni sahihi pesa ya umma kuchezewa? Rais mstaafu anatumia gari na kila kitu cha umma mpk atakapo kufa, kama alikuwa anapata shida gari ni ndefu kwanini asibadilishiwe au kununua yeye mwenyewe ama kununuliwa na mtoto wake?
Unataka Rais Mstaafu atembelee Carina?
 
Mosi Hebu tupe majina ya wanaolipwa kuikosoa serikali..

Pili tupe ushahidi wa kimaandishi kuonesha hayo malipo ya kuikosoa serikali yanatokea kwa nani kwenda kwa nani na kwa njia ipi ya malipo...

Tatu tupe mkataba unaoonesha namna wakosoaji wamepewa namna ya kukosoa na unadumu kwa muda upi maana ukosoaji uko duniani kote na hakuna asiyekosolewa..
Maswali ya kipuuzi kabisa haya
Kama hawalipwi ni nini kinawawasha kukosoa hata ambavyo havikosoleki?
 
Back
Top Bottom