Ninachukia hiki katika shule binafsi

Ninachukia hiki katika shule binafsi

shamimuodd

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,191
Reaction score
2,119
Great Thinkers,

Nakumbuka enzi zetu heshima ilikuwa kusoma shule za serikali.

Pamoja na uwepo wa shule za binafsi, wazazi wenye uwezo walihangaika kuhonga watoto wao wasome shule za serikali.

Kwenye shule hizi za serikali, tulilima bustani za mchicha, tulijifunza ufugaji, tulifanya kazi za kufyeka, tuliwekeana zamu ya kuhudumia meza zetu za chakula, tulikula maharage wakati mwingine mabovu, yaani ilikuwa fujo fujo mpaka raha.

Shule za sekondari/ msingi za binafsi ni majanga makubwa sana, yaani watato wanashindanishwa kukariri, hawana ubunifu, na wakifika vyuoni wanaongoza kwa kufeli. Shule za binafsi zinaharibu sana kizazi chetu.

Ada kubwa na walimu wa hizi shule za binafsi wanataka kulipwa tuition ili mtoto amuangalie angalie, asimchape, amdekeze dekeze etc.

Ningekuwa na mamlaka ningefanya mbinu shule za binafsi zife!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom