Rais Magufuli hawezi kuwa sahihi katika hili la mikopo chuo kikuu

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
MAGUFULI HAWEZI KUWA SAHIHI KATIKA HILI LA MIKOPO.

Kabla ya kuanza kujadili kauli hii ya Rais kwanza niorodheshe #interesting_facts katika swala hili.

1. Je uliwahi kujua kamba pesa inayotumika kusomesha wanafunzi vyuo vikuu na VETA ni pesa inayotolewa na shule binafsi ikiwemo na makampuni mengine binafsi?

Kodi ya kusomeshea watanzania inaitwa Skills and Development Levy(SDL).

Kodi zingine zote unazozijua na usizozijua hazihusiki kusomeshea wanafunzi chuo kikuu na VETA.

Hii kodi hailipwi na kila mtanzania kama kodi zingine bali inalipwa na private schools pamoja na makampuni mengine binafsi.

Kwa hiyo shule zote binafsi nchini zikishirikiana na makampuni binafsi ndizo zimepewa jukumu la kusomesha wanafunzi chuo kikuu na VETA.

did you know this?

Kwa hiyo wanafunzi wote wanaosoma shule binafsi kimsingi ndio wanalipa pesa ya kusomeshea wanafunzi wa chuo kikuu na VETA.

Pia wanafunzi wote waliowahi kusoma shule binafsi nao walichangia kusomesha wanafunzi vyuo vikuu.

2. Si kila anayesoma private school kwao ni matajiri.

Ni muhimu tukajua sababu za msingi wazazi kupeleka watoto shule binafsi ili tuboreshe shule zetu za serikali kuondoa aibu hii.

wengi wanawapeleka watoto private kwa sababu wana uhakika watoto watapata elimu bora na watafaulu lakini pengine wanasoma kwa shida sana.

Kumpeleka mtoto serikali moja kwa moja anakosa elimu bora na hata kufaulu linabiki swala la kumwachia mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo kusomesha private si kwa sababu ya jeuri ya pesa.

(a):Wapo wanaouza mashamba kusomesha.

(b)wapo wanaouza machungwa na ngogwe kusomesha.

(c)wapo wanaofanya vibarua kusomesha.

(d) wapo wanaofanya umachinga kusomesha.

(e) wapo wanaouza kila kitu nyumbani ikiwemo nyumba ya kuishi ili mtoto aende shule.

Kuna familia zingine mpaka mtoto anamaliza form four wanakuwa wameuza kila kitu nyumbani.

(f) wapo wanaosomeshwa na mashirika, ndugu ama marafiki katika shule hizi za private.

(g) lakini pia kuna private schools zenye gharama nafuu, kiasi kwamba mzazi yeyote aliyedhamiria anaweza kusomesha private kwa kulipa ada kidogokidogo na tena mtoto akawa day.

(h) kuna watoto wengine ambao ni kweli wametoka familia zenye uwezo ndio maana wakasoma private schools.

lakini uchumi wa wazazi ukayumba ama wakafilisika, ama biashara ikayumba, ama mzazi amestaafu ama amefukuzwa kazi nk nk.

Huyu mtoto ambaye amekuwa masikini leo unamnyimaje haki ya kupata mkopo kisa jana alikuwa tajiri?

Ama ndio kutaka matajiri waishi kama mashetani?

Kwa hiyo kusoma private si ushahidi kwamba mtu anapesa nyingi kuweza kujisomesha chuo kikuu.

3. Pia, Si kweli kwamba ukisoma shule za serikali basi wewe ni masikini. Hiki ni kiwango kidogo kabisa cha kufikiri.

Wapo wazazi ambao wana pesa kabisa lakini wanaamua tu kupeleka watoto shule za serikali.

Tena wengine waliposikia ukisoma private hupati mkopo basi huamua kuwapeleke watoto serikalini lakini kwa tahadhari kubwa ya kuhakikisha wameajiri mwalimu wa kumfundisha mtoto ili asipate yale masifuri.

Wengine wanahakikisha wanawalipia watoto tuition za mtaani pesa nyingi wasipate masifuri.

Wanafanya hivi ili mwisho wasije kukosa mkopo chuo kikuu.

Tunahitaji kufikiri zaidi.

4. Wazazi wengi wanapeleka watoto wao private kwa sababu wanaogopa ubovu wa shule za serikali.

Mbunge wa Ulanga Goodlack Mlinga aliwahi kumwita waziri elimu Profesa Ndalichako kuwa ni waziri wa masifuri(maana shule za serikali zilizo chini yake ndio zinatoa division zero za kutosha)

Ndio maana akampachika jina la waziri wa masifuri.

kama tukiondoa matokeo yote ya shule za private basi Ndalichako anageuka kutoka kuwa waziri wa elimu mpaka kuwa waziri wa masifuri.

Haya masifuri ya shule za serikali kila mtu anayaogopa kuanzia mzazi mpaka mwanafunzi.
.
.
Kwa hiyo tusiwahukumu wanaosoma shule za private na badala yake tujikite kuboresha elimu ya shule zetu za serikali ili tuondokane na aibu hii.
.
.
sasa nirudi kwenye hoja kujadili hatari ya hii kauli.

Serikali ya Magufuli inaenda kupanda mbegu mbaya ya ubaguzi na uvunjaji haki za mwanafunzi kupata elimu.

Haiwezekani kwamba pesa yote ya kusomeshea wanafunzi vyuo vikuu itolewe na shule binafsi na makampuni yasiyo ya serikali lakini serikali hiyo hiyo ikatae kuwasomesha wale waliochangia kupatikana kwa hiyo pesa tena wengine ni masikini kweli kweli waliosomeshwa kwa kuuza mashamba yote nyumbani, nyumba ama hizi biashara ndogondogo kama mama ntilie nk.

Hii ni taarifa ya kushitusha sana.

Huu ni ubaguzi mkubwa ambao haupaswi kabisa kufumbiwa macho.

Mathalani Katika ripoti ya CAG ya 2016/2017 iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza,

katika ukurasa wa 373 imeonesha kwamba kodi ya SDL iliyokusanywa kwa mwaka 2016/2017 ilikuwa zaidi ya billioni 280.

Katika pesa zote hizo, billioni 93 ndizo zilitumika kugharamia mafunzo yote ya VETA nchini katika vyuo vyote vya serikali.

Billioni 186 ndizo zilitumika kusomesha wanafunzi chuo kikuu nchini katika mwaka wa masomo 2016/2017. Soma mwenyewe ujionee katika ripoti ya CAG.

Kwa nini iwe dhambi leo kusoma shule binafsi?

Kwanza ilibidi tuzishukuru sana shule binafsi kwa kutusomeshea watoto wa taifa hili kwa kugharamia elimu yote ya VETA na mikopo ya chuo kikuu.

Nini mchango wa shule binafsi nchini?

Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba shule za private ndizo zinachangia upatikanaji wa wataalamu wa sayansi kwa zaidi ya asilimia 90 nchini.

Hivi leo karibu wanafunzi wote wanasoma sayansi waliopo shule za serikali A level ni zao la shule binafsi.

Kama si O level basi A level. Sitaki kuingia ndani sana katika hili.

Kwa lugha rahisi ni kwamba bila shule za private hivi leo tungekosa madaktari na tungekosa wahandisi.

Na vyuo vyetu vya sayansi na uhandisi vingekumbwa na uhaba mkubwa mno wa wanafunzi.

Wanafunzi wasibaguliwe katika mikopo.

Ni mara nyingi sana nimekuwa napinga hata utaratibu wa kupendelea tu wanafunzi wa sayansi huku wale wa kozi za arts wakitelekezwa kana kwamba taifa haliwahitaji.

Wanafunzi wote wapewe mikopo iwe ni wale waliosoma private schools ama masomo ya arts kama waliosoma shule za serikali na masomo ya sayansi.

Nawasilisha

Mshinga JN
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,799
2,000
umejenga sana hoja ila kuna kitu umesahau

una shilingi 1000 wamekuja watu wawili kukuomba hiyo 1000 hawajala chakula wana njaa.. mmoja ni mlemavu na mwingine mzima na wote hawajala wanaiomba hiyo buku.. je utampa nani?
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,608

Hakuna nchi yoyote ile Dunia hii ambapo Serikali hutumia fedha zake kulipia watoto wa matajiri kusoma Chuo Kikuu, nchi zote Duniani Serikali hugharamia masikini kwanza kwani matajiri wana uwezo wakujigharamia!
 
Kwa hiyo aliyesoma private ndiye mzima na aliyesoma serikali ndiye mlemavu.

Nimesema hiki ni kiwango kidogo kabisa cha kufikiri na nimetoa maelezo mengi na ushahidi mwingi kwamba unayemwita mlemavu anaweza asiwe mlemavu na unayemwita mzima anaweza asiwe mzima
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,337
2,000
umejenga sana hoja ila kuna kitu umesahau

una shilingi 1000 wamekuja watu wawili kukuomba hiyo 1000 hawajala chakula wana njaa.. mmoja ni mlemavu na mwingine mzima na wote hawajala wanaiomba hiyo buku.. je utampa nani?
Nampa mtu mzima kwasababu anauwezo wakurudisha haraka iliniweze kumkopesha kilema
 
Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
608
500
Mshinga umenifanya mchozi uninidondoke. Mungu alinijalia wana wanne. Nilijitahidi watatu katika yako toka primary wakafaulu kumaliza chuo kikuu lakini bado wanabangaiza wa nne.nimejitahidi nguvu zimeisha imelazimika kusimama masomo ya degree ya sayansi ya maabara Bugando inauma sana, ninampenda serikali ya JPM lakini hilo linaniuma.
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,569
2,000
Mtaani kwangu nimefatwa na wazazi 2 (hawa ni kwa uchache ninao wajua) wakiniomba niwatafutie kibarua watoto wao ambao wamerudishwa chuo kikuu kwa kukosa mkopo; mmoja alikua anasoma computer science na mwingine sikutaka hata kuuliza alicho kua anasomea; niliwaambia tu, "endapo kutakua na nafasi nitawaunganisha na boss wangu" Huyu aliyekua anasoma computer science O level alisoma shule moja ya ya day ya Roman Catholic, baba yake alikua anauza MAJI kwa watu wa mtaani kwake cause alikua na kisima akajenga na tank, changamoto ipo hivi; kwasasa hiyo biashara sio deal tena kwasababu serikali imeleta maji safi na salama kwenye hilo eneo so hana WATEJA tena; huyu mwingine ambaye sikutaka kujua alicho kua anasomea, yeye baba yake ni KADA mtiifu wa ccm, na ni balozi wa mtaani kwangu, masikini sana. Kijana alikua anasomeshwa na shemeji yake (mume wa dada yake) shule moja ya private (sina hakika na jina la hiyo shule) kwasasa huyo shemeji yake nae ana majukumu na ni mwanajeshi, nadhani watoto wake nae wameanza shule and hence having more responsibility and accountability, ndio hivyo wapo nyumani. Hao ni kwa uchache ninao wafahamu.
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,337
2,000
Hakuna nchi yoyote ile Dunia hii ambapo Serikali hutumia fedha zake kulipia watoto wa matajiri kusoma Chuo Kikuu, nchi zote Duniani Serikali hugharamia masikini kwanza kwani matajiri wana uwezo wakujigharamia!
Kuwa nauwezo wa kifedha sio dhambi na kwanini umhadhibu mtoto wa mtu anae pambana kupata utajiri.......wtznia tuache kuchukia na kubaguwa watu wenye fedha sio kwamba walipewa bure. Natusifanye watu kufikiri eti ukiwa masikini ni neema(kua priveledged) ni fitina na ignorance
 
tokenring

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
268
500
Hata mimi naona hili suala halijakaa vizuri. Maana kama kulipa kodi wanalipa masikini na matajiri. Hivyo naona mkopo utolewe kwa wote cha kuzingatia ni uzito wa historia ya matatizo au shida za mwombaji wa mkopo kutokana na viambatanisho alivyoweka. Hii nikiwa na maana anayeonekana ana shida sana apewe kipau mbele na asilimia ya mkopo iwe kubwa kwake. Hii itasaidia wote wasome mfano tuchukulie ndo hawa wa private wanaotaka kunyimwa basi wanyiwe Ada ( kwa maana ada wajilipie) ila hela ya matumizi na stationery wapewe.Nafikiri kwa njia hii kila mtu atapata stahili yake.
 
tumaini obedi

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
340
250
Hakuna nchi yoyote ile Dunia hii ambapo Serikali hutumia fedha zake kulipia watoto wa matajiri kusoma Chuo Kikuu, nchi zote Duniani Serikali hugharamia masikini kwanza kwani matajiri wana uwezo wakujigharamia!
Hivi ni saidie kwanza tajili ni yupi?,Na madikini ni yupi?....harafu ndipo nitachangie zzaidi.
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,135
2,000
Hakuna nchi yoyote ile Dunia hii ambapo Serikali hutumia fedha zake kulipia watoto wa matajiri kusoma Chuo Kikuu, nchi zote Duniani Serikali hugharamia masikini kwanza kwani matajiri wana uwezo wakujigharamia!
Leo hii private school ni kipimo cha utajiri????????????????????????

Wtf. Mama yangu anamsomesha mtoto wa dada yangu shule ya private kwakua shule za serikali hazina ufaulu mzuri. Unajua anamsomesha kwa pesa zipi??????

Analima mahindi na maharage. Akiuza, ndipo ada ya mpwa wangu inapatikana. Mama yangu anajinyima kwa kua anauhakika anamjengea mazingira mazuri huyu binti hapo baadae maana elimu ndo ufunguo wa maisha.

Leo hii mnakuja mnasema eti kusoma private ni kuwa tajiri. Ama Tanzania imeingiliwa
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,608
2,000
Kuwa nauwezo wa kifedha sio dhambi na kwanini umhadhibu mtoto wa mtu anae pambana kupata utajiri.......wtznia tuache kuchukia na kubaguwa watu wenye fedha sio kwamba walipewa bure. Natusifanye watu kufikiri eti ukiwa masikini ni neema(kua priveledged) ni fitina na ignorance

Ni wapi imesemwa kwamba ni dhambi kuwa na uwezo wa kifedha? Kwanza ninyi ndo mnafanya dhambi kwa maana mna uwezo wa kifedha lkn bado mnataka kushindanishwa kwenye mizani sawa na mtoto wa masikini, hiyo ni dhambi hata Mungu hapendi!

Mtu mwenye uwezo kifedha akikosa mkopo mtoto wake hawezi kuingia mtaani bali Wazazi wake watamtafutia namna ya kusoma, mtoto wa Masikini aliyesoma kwa uwezo tu wa Serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka A-level Serikali isipomlipia ndo mwisho wake!

Hivyo, Raisi Magufuli yupo sawa kabisa Duniani na Mbinguni sema ninyi ubinafsi wenu wa kutaka kufaidika kwa gharama ya masikini ndo unaowasumbua!
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,608
2,000
Leo hii private school ni kipimo cha utajiri????????????????????????

Wtf. Mama yangu anamsomesha mtoto wa dada yangu shule ya private kwakua shule za serikali hazina ufaulu mzuri. Unajua anamsomesha kwa pesa zipi??????

Analima mahindi na maharage. Akiuza, ndipo ada ya mpwa wangu inapatikana. Mama yangu anajinyima kwa kua anauhakika anamjengea mazingira mazuri huyu binti hapo baadae maana elimu ndo ufunguo wa maisha.

Leo hii mnakuja mnasema eti kusoma private ni kuwa tajiri. Ama Tanzania imeingiliwa

Ndiyo private schools ni kipimo cha utajiri, Dunia nzima ni hivyo, mtoto wa masikini hawezi kuchagua akasome wapi bali atasoma Shule za Serikali tu kwani ndizo zilizopo kwake, ile tu kwamba unaweza kuchagua ina maana wewe siyo masikini!
Kwa maana nyingine kesho walimu wote wakigoma hata mwezi mtoto wako wa private ataendela kusoma lkn wa Shule za Kata hatasoma na hakuna kitu atafanya!
 
Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,242
2,000
solution,nadhani..tujadili,jinsi..gani,serikali..igawe,au..kutoa,mikopo..kwa,wanafunzi.
itakuwa,vema..zaidi,kulingana,na..uwezo,pamoja..na,vyanzo,vya..hiyo,pesa..ya,mkopo
 
johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
636
1,000
Naunga hoja yako mkuu. Huu ndiyo ukweli thabiti.
Lakini pia hivi tunavyosema private school, tunachukulia Kwa ujumla wa private" Bila kuangalia Aina ya hizo " private"?
Ni sahihi kuziweka sawa shule hizi kama inyotoza ada ya kuanzia million tatu Kwa mwaka hadi million zaidi ya 15 na zile zinazotoza ada ya milioni Moja Kwa mwaka?
 
KABIDI BODO

Senior Member
Jan 19, 2017
183
500
JPM hajawahi kuongea kitu kwa bahati mbaya, nionavyo mimi ni mkakati wakupunguza fungu bodi ya mikopo, pia ni mkakati wakupunguza idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu..
Wazazi na wazazi watarajiwa tujipange tu kusomesha kwa pesa zetu wenyewe..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom